Nadhani ni jambo lisilopingika kwamba foleni za barabarani ktk jiji la Dar zinaongezeka siku hadi siku.
Ninashauri JK na viongozi wengine wanaopenda sana misafara mirefu waanze utaratibu wa kutumia ELIKOPTA kutoka pale kwenye viwanja vya Magogoni/Ikulu kwenda na kurudi AIRPORT. Vilevile niliwahi kusikia kwamba pale juu kabisa ya TWIN TOWERS palitengenezwa imara sana kwa lengo kama hilo, kwamba Rais anaweza kutoka pale Ikulu akafika kwenye majengo hayo, akapanda lift hadi juu, akaingia kwenye ELIKOPTA akaanza mpaka Air Port na wakati wa kurudi hivyo hivyo.
Je hii itapunguza foleni kwa kiasi gani??????????
Ni ukweli usiopingika kuwa misafara ya viongozi wa kitaifa inazorotesha sana mwendo kasi ndani ya Jiji la Dar es salam. Viongozi wetu wanakuwa na misafara mirefu na pia huchukua muda kuzisafisha njia hadi wanausalama waridhike kuwa hali ni shwari kwa kiongozi mhusika.
Ni bahati mbaya kuwa mipango miji iliyokuwepo ni ile ileiyoachwa na wakoloni, ambayo maendeleao yaliyofanywa kuipanua ni kidogo sana ili kuweza kutoa nafasi zaidi kurahisisha usafir ndani ya jiji. Barabara zinazoingia na kutoka katikati ya jiji ni zile zile za miaka nenda rudi.
Usafiri wa kutumia ndege ikiwa ni pamoja na helkopta nadhani ndio zinzohesabika kuwa salama sana kuliko usafi mwingine, haswa pale vyombo hivyo vinapokuwa na sifa, achilia mbali zile helkopta za jeshi zilizonunuliwa kwa rushwa, sijui zilitengenezwa chini pamoja na taka nyingine nyingi zilizo jaa Tanzania.
Hivyo basi kama Rais na wateule wengine wasiosongamana na watanzania njiani ingekuwa bora sana kutumia vyombo hivyo vya juu japo kutupunguzia adha ya foleni.
Ukweli unabaki kuwa serikali inahitaji kuliangalia suala la usafiri na miundombinu ya Dar es salaam kwa jicho la karibu kwani sasa JIJI LIPO karibuni KUSIMAMA. Pamoja na kuwa na mabasi makubwa na yanayodaiwa kwenda kwa kasi, bado tunahitaji kuwa na njia zenye viwango za kutosha, hususan madaraja (flyovers) katika makutano korofi, kuanzisha miji mipya nje ya jiji ili kuawanya shughuli za kiofisi na kibiashara kutoka Mjini kati na Kariakoo. Pia kuangalia uwezekano wa kuwa na usafiri kama wa treni, sijui kama za chini ya ardhi tutaweza.
Tatizo la usafiri ni kubwa haswa sasa kuanzia Chalinze hadi Dar es salaam. Kuna haja ya serikali kuwa na barabara za viwango tofauti tanzania. Ni ukweli usiopingika kuwa ajali zimekuwa nyingi eneo hili kwa sababu ya magari ni mengi na kila gari linalotokea upande husika linakuwa na njia moja tu. Nadhani Tunahitaji barabara zote kuu zinazoingia dar ziwe angalao Double, na zikifika Dar ziwe 3 hadi 4. Mfano hakuna sababu ya kuongeza double road kutoka Kimara hadi Kibaha kwa sasa, ila hili inatakiwa Kufika angalao chalinze kama sio morogoro. Huu ndio uwe mwendo mdundo kwa barabara zinzounganisha mikoa na iwe hivi hasa zinapoingia na kutoka.