JK: Huyoooo USA


duh! noma yaani machizi mnavyojua ratiba ya jamaa mpaka nakoma na nyinyi

 
Dizaini anaweza akatia timu Velvet Room au The Compound jumamosi hii. Lazima mazee niibuke nika-kick naye....
 

Pennslyvania Avenue?.. does it bring a bell anybody?
 
Unyamwezini kuzuri acheni mchezo nyie,akifika huku ni kama peponi tuu...nani hataki peponi?
 

Utakuwepo mzee? Kuna urasmi sana ubalozini pale lakini, mungu akipenda nitakuwa eneo la tukio. Natumaini safari hii wale jamaa wa ATA hawatajazana kupiga picha na mkuu wa kaya kama kule NY alafu wanatundika ofisin kwao wanatumia kama reference picha yenyewe hizo hapo chini.

NB Hizi picha niza ziara ya Mh. iliyopita wakati anazindua tangazo la Tanzania the land of Kilimanjaro,Zanzibar & Serengeti.


 
Mtanisamehe nimeingia katikati ya mjadala huu lakini jamani kuja kwake US safari hii hamuoni kama ni muhimu ama mnajua kinachomleta?....
Binafsi, sababu ya msafara huu naiona ni muhimu zaidi ya safari nyingi alokwisha zifanya ikiwa atakuwa na Ujumbe mkubwa unaoweza kutuunganisha. Sijui labda nimekosea na kurukia hoja bila kuifahamu vizuri....
Mimi nina imani kubwa kwamba siku tutakayo weza kujenga daraja kati yetu na hawa jamaa wenzetu wa US na wakaweza kuwa bega nasi wakawekesha nchini basi ndio mwanzo wa kumkomboa mtu mweusi.
Ajabu ni kwamba nimekuwa nikiamini ushirikiano wetu na hawa jamaa kuwa muhimu sana kwa zaidi ya miaka 20 na kila siku huomba Mungu atokee rais atakayeweza kujenga daraja hilo. With their eyes watching our back tunaweza kabisa kukataa mikataba mibaya pamoja na sheria zao, haki zetu zikasikika kama tulivyoweza kusikiwa enzi za Apartheid...
Na kubwa kuliko lote naamini kabisa kuwa hawa jamaa wanaweza kuwekesha Africa ama Tanzania kwa moyo na wanaujua uchungu wa mama Africa. Tatizo kubwa ni pale viongozi wetu wengi wanapowaona hawa jamaa kama tishio kubwa la Utawala wao kwani hawa wenzetu wamesoma na hawana njaa.
Ikiwa Ophrah kaweza jenga shule moja ya dollar million 40 tena kama zaka yake tu hivi huyu mama akiwekesha Tanzania mathlan ktk madini na vito anaweza kulijenga vipi njina la nchi yetu?... leo hii tumpe RUKSA ya kutengeneza vito vyake nchini na asilimia kubwa ya vito vyetu i.e Tanzanite iuziwe kampuni yake, hivi nani huko majuu ataweza kuweka sheria ya kupiga marufuku vitu vyake?...Kwa nini tusimtajirishe ndugu yetu sisi wenyewe kwa kushirikiana kama wanavyofanya wenzetu!... tazameni wahindi, wayahudi na kadhalika hawa watu ni ndugu kila kona ya dunia isipokuwa sisi matumbi!
 
Dizaini anaweza akatia timu Velvet Room au The Compound jumamosi hii. Lazima mazee niibuke nika-kick naye....

Akajirushe na Diddy sio? Umemsikia Arthur Blank anasema MV7 asipokula chicken and french fries kuna possibility za kuruhusiwa kurudi kuchezea dirty bird sio..
 
Pennslyvania Avenue?.. does it bring a bell anybody?

Anaweza kuamua kufanya matembezi ya jioni kuelekea upande wa kaskazini magharibi mwa mtaa huo na kuvuka kale kamto kidogo kupita kwenye park/national mall kuelekea you know where...
 
mwache aje tuu tuapate sababu ya kuja kuchill DC,lakini kama ni kweli next yr mkutano utakuwa Arusha na wanategemea 3000 Americans bora aje atie uzito...kina mangi na mollel mkae mkao wa kula maana harufu ya dola naiskia hapo A town wakija hawa jamaa!
 
Akajirushe na Diddy sio? Umemsikia Arthur Blank anasema MV7 asipokula chicken and french fries kuna possibility za kuruhusiwa kurudi kuchezea dirty bird sio..

Yeah...heard it but I don't think he meant any harm. Halafu breaking news kutoka Flowery Branch ni Bobby Petrion kajiuzulu....talk about dysfunctional
 
Mwawado,
Utakuwepo? Nikisikia lolote juu ya ziara nitawabeep.

Mkuu Jasusi na Icadon,Nitakuwepo kwenye Dinner ya Sullivan Foundation,Alhamis jioni.Nafikiri kama mambo yakiwa mazuri tutaonana huko,ni wazi kwamba nitawatambua haswa Mzee wa East Coast,na tuonane huko.Ikiwa kuna matatizo ya kuonana/kutambuana angalieni meza ya "Press"
 
Maybe this an important event, we should not be general in critising all the president's trips, should we?

If this trip has any importance to Tanzanians, do we have the right to know the importance of this trip? The answer is YES.
 
Mkandara,

Sipingani na hoja zako iwapo tu Muungwana ana nia njema ya kutuletea genuine investors nchini mwetu na kwamba mambo ya mikataba na process nzima ya uwekezaji itakuwa ya wazi na si viini macho na siri nzito ambazo hata wabunge wetu hawawezi kujua ni nini kilicho kwenye hiyo mikataba.

Ukiangalia kwa undani wawekezaji wengi tunaowapata wana connections na wana siasa na tena siyo wana siasa uchwara bali ni big shots walio kwenye viti vya enzi. Kibaya zaidi hao wana siasa ndiyo wanawashika mikono wawekezaji na kuwaelekeza namna ya ku-negotiate mikataba na ikigoma wanaingilia kati na kuwaweka pembeni technocrats. Matokeo yake watalaam wetu wanajisikia vibaya kwamba ushauri wao haupewi uzito, mambo yakija kubuma utasikia kwamba Tanzania haina watalaam.

Tuna wawekezaji kutoka Canada kwenye sekta ya madini, naona wanazidi kutumaliza tu. RDC imetoka US imekunywa hela yetu na sasa sijui hata tunachunguza kitu gani. Tatizo ni kwamba genuine invetors hawawezi kuja kwetu kama wanajua kuna rushwa na uswahili mwingi. We need to improve institutions za ndani ndipo sasa tutaweza kupata wawekezaji wa maana, vinginevyo tutaishia kuwapata akina Barrick na Richmonduli. Kabla ya kujenga hilo daraja inabidi turekebishe mambo ya ndani kwanza.

Mkapa alipigia sana kelele globalization, imetufikisha wapi mpaka leo? Kwa hiyo kama ni daraja, sawa! Lakini twende hatua kwa hatua ili tuwe na mahali pa kuanzia, vinginevyo na JK atakuja kutangaza Sullivan na hao wawekezaji watajipenyeza na kumuona privately na kuanza kuomba upendeleo ili waje wawekeze. Sasa hapo tutaendelea kupata mabomu mengine mengi tu. Wawekezaji wenyewe wanasoma kwenye magazeti na kujionea hali halisi, kwa wale ambao ni matapeli wataanza kusaka connections za kuingia Tanzania, lakini kwa kupitia kwa wana siasa wetu au kwa mtu ambaye ana influence kubwa serikalini. Mambo ta RDC, Barrick, Radar, Chopa za Jeshi, na mengineyo si kwamba yanajulikana ndani ya Tanzania pekee, bali yanajulikana na huku nje. Kama JK angekuwa bold enough na kuonyesha kwamba ana lengo la kurekebisha hizo kasoro, nina uhakika wawekezaji wenye nia njema ya kufanya biashara ya kweli na haki watakuja. Lakini vinginevyo tutaendelea kuwaomba waje wawekeze and on top of that tunawaomba na 10% au tunawauliza kwenye uwekezaji wao wako kwenye position ya kutoa kamisheni kiasi gani!
 
Mwawado,
Basi nitakutafuta kwenye hiyo meza. Mimi na memsap wangu tumepewa kadi, alhamdulilah.
 

Ya mananasi umenivunja saaaaaaaaaana mbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…