Mkandara,
Sipingani na hoja zako iwapo tu Muungwana ana nia njema ya kutuletea genuine investors nchini mwetu na kwamba mambo ya mikataba na process nzima ya uwekezaji itakuwa ya wazi na si viini macho na siri nzito ambazo hata wabunge wetu hawawezi kujua ni nini kilicho kwenye hiyo mikataba.
Ukiangalia kwa undani wawekezaji wengi tunaowapata wana connections na wana siasa na tena siyo wana siasa uchwara bali ni big shots walio kwenye viti vya enzi. Kibaya zaidi hao wana siasa ndiyo wanawashika mikono wawekezaji na kuwaelekeza namna ya ku-negotiate mikataba na ikigoma wanaingilia kati na kuwaweka pembeni technocrats. Matokeo yake watalaam wetu wanajisikia vibaya kwamba ushauri wao haupewi uzito, mambo yakija kubuma utasikia kwamba Tanzania haina watalaam.
Tuna wawekezaji kutoka Canada kwenye sekta ya madini, naona wanazidi kutumaliza tu. RDC imetoka US imekunywa hela yetu na sasa sijui hata tunachunguza kitu gani. Tatizo ni kwamba genuine invetors hawawezi kuja kwetu kama wanajua kuna rushwa na uswahili mwingi. We need to improve institutions za ndani ndipo sasa tutaweza kupata wawekezaji wa maana, vinginevyo tutaishia kuwapata akina Barrick na Richmonduli. Kabla ya kujenga hilo daraja inabidi turekebishe mambo ya ndani kwanza.
Mkapa alipigia sana kelele globalization, imetufikisha wapi mpaka leo? Kwa hiyo kama ni daraja, sawa! Lakini twende hatua kwa hatua ili tuwe na mahali pa kuanzia, vinginevyo na JK atakuja kutangaza Sullivan na hao wawekezaji watajipenyeza na kumuona privately na kuanza kuomba upendeleo ili waje wawekeze. Sasa hapo tutaendelea kupata mabomu mengine mengi tu. Wawekezaji wenyewe wanasoma kwenye magazeti na kujionea hali halisi, kwa wale ambao ni matapeli wataanza kusaka connections za kuingia Tanzania, lakini kwa kupitia kwa wana siasa wetu au kwa mtu ambaye ana influence kubwa serikalini. Mambo ta RDC, Barrick, Radar, Chopa za Jeshi, na mengineyo si kwamba yanajulikana ndani ya Tanzania pekee, bali yanajulikana na huku nje. Kama JK angekuwa bold enough na kuonyesha kwamba ana lengo la kurekebisha hizo kasoro, nina uhakika wawekezaji wenye nia njema ya kufanya biashara ya kweli na haki watakuja. Lakini vinginevyo tutaendelea kuwaomba waje wawekeze and on top of that tunawaomba na 10% au tunawauliza kwenye uwekezaji wao wako kwenye position ya kutoa kamisheni kiasi gani!