JK kukatiza ziara ili kupokea kifimbo cha malikia

JK kukatiza ziara ili kupokea kifimbo cha malikia

ulimboka

Member
Joined
Aug 23, 2009
Posts
36
Reaction score
0
Jamani jana nimeangalia taarifa ya habari zilizogubikwa na maafa yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini. Cha kunishangaza ni kwamba Mkuu wa nchi eti alikatiza ziara ila sijajua ni ipi na uzito wa hiyo ziara hadi ikatizwe na kuwahi kifimbo cha malkia.
Lakini je kuna mdau yeyote anayeweza kunifumbua mambo juu ya uzito wa kifimbo cha malkia hadi kushinda maafa haya yanayotukuta sisi na ndugu zetu.
Wana JF naomba kuwasilisha
 
Hajakatiza ziara yoyote. Amekatiza mapumziko yake ya mwisho wa mwaka. Hata Pinda yu mapumzikoni. Kuhusu kifimbo cha Mali-kia ni kampeni ya Uingereza ya uhamasishaji wa Michezo ya Jumuiya ya Madola ambayo Malikia wa Uingereza ndie mkuu wake. Hata hivyo mhamasishaji mkuu alitakiwa awe balozi wa Uingereza lakini aliehamasisha ni balozi wa India. Malikia na India ni wapi na wapi?.
 
Ningekuwa na uwezo fulani hako kafimbo ningekavunja vunja na kukatupilia mbali. Next time litakuja gagulo la Malkia!
 
Wewe PASCO acha hizo. Balozi wa India amehusishwa kwa sababu michezo ya Commonwelath 2010 India ni mwenyeji. Hizo ni taratibu za Kiitifaki. Labda ungeuliza michezo ya Commonwealth, Katibu Mkuu wa Tanzania Olympic Commitee kahusika vipi? Hilo swali lingekuwa na hekima. Kwa sababu michezo ya Olympic ni tofauti kwa mbali na hiyo michezo ya C/wealth. Kwa nini isipokewe na kusimamiwa na afisa wa BMT? Au they are too old? Au?
 
Ningekuwa na uwezo fulani hako kafimbo ningekavunja vunja na kukatupilia mbali. Next time litakuja gagulo la Malkia!

Mkuu kwani hii jumuiya ya madola si ukoloni mamboleo tu! Ndo tunasema commonwealth ya waingereza waliotutawala bila ridhaa yetu! kama sio kuzidi kuwakumbatia ndo nini, halafu eti tunapokea kifimbo mi nashangaa kimetinga hadi ikulu..sijui na yenyewe inaweza kupeleke kifimbo cha michuano ya kombe la mapinduzi or something kule B.palace?
 
Ningekuwa na uwezo fulani hako kafimbo ningekavunja vunja na kukatupilia mbali. Next time litakuja gagulo la Malkia!
Hivi hiki kifimbo kina maana gani hasa??? kwamba wazee wetu walitawaliwa kwa viboko au??? Hata hii commonwealth sioni umuhimu wake ndio mana UTUMWA WA KIAKILI hauishi kwenye jamii yetu!
 
Back
Top Bottom