Mundali
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 749
- 164
Habari nilizozipata kupitia Clouds Fm radio ni kwamba mgombea wa ccm, rais Jakaya Mrisho Kikwete atafanya mkutano na waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya kampeni zake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Iwapo itatolewa fursa kwa waandishi waalikwa kuuliza maswali, naomba niwakilishwe pamoja na watanzania wote wenye mtazamo kama wa kwangu maswali yafuatayo: -
1. Akiwa kampeni kwenye mikoa mbalimbali, mgombea wa kiti cha urais kupitia ccm amekuwa akitoa ahadi kemkem za miradi ya maendeleo yenye kutia matumaini kwa wananchi. Je, akiwa pamoja na timu yake ya kampeni amefanya tathmini ya gharama ya jumla kwa miradi yote aliyoahidi kuitekeleza ndani ya miaka mitano?
2. Ni kiasi gani kwa pesa ya tanzania zinahitajika kukamilisha miradi hiyo yote aliyoahidi?
3. Pesa za kugharamia miradi hiyo zitapatikana vipi?
Mimi na baadhi ya watanzania wenzangu tumekuwa tukijiuliza maswali hayo bila kupata majibu stahili. Tunaomba ndugu zetu waandishi wa habari mtufikishie ujumbe wetu. Shukrani nyingi kwenu.