Elections 2010 JK kutangazwa Rasmi Kesho, Kuapishwa Jumamosi!

Elections 2010 JK kutangazwa Rasmi Kesho, Kuapishwa Jumamosi!

Wanabodi,

Matokeo ya Urais kwa Majimbo Tanzania, yanakamilika usiku huu ambapo mshindi JK atatangazwa rasmi kesho saa 10 jioni pale kwenye viwanja vya Karimjee na kuapishwa Rasmi Jumamosi Saa 4:00 asubuhi kwenye Uwanja wa Taifa.

Tegemea kuwaona kina Dovutwa, Mziray, Mtamegwa, Rungwe na Lipumba, wakiwa kwenye colourful dress tayari kumpongeza JK kwa genuine smilling faces.

Dr. Slaa anatakiwa sana awepo. Mlio karibu nae, mshaurini asisusie, kweli asisaini kuyakubali matokeo, lakini awepo mahali hapo kuwasilisha live protest yake kwa wahusika for the sake of umoja wa kitaifa.

Mimi namsikiliza Dr. Slaa. Akinambia niwepo nitaenda akisema usiwepo, siendi maana huyo ndiye Rais wangu. Kwa maoni yangu, asiwepo
 
Slaa hana haja ata ya kwendaaaaaaaa
Atajishushia p yake

Well said,
Eti Slaa aende kwa kulinda umoja wa kitaifa,Umoja upi huo?umoja na akina R.A,Kinana,Makamba na wanafiki wengine.
 
Mwafrika, kama Seif ameweza kukubali, why not Dr. Slaa.

Sherehe ya kesho kutangaza matokeo, washindwa wanapewa fursa ya kuongea, ndipo mshindi anatoa hotuba ya shukrani, Dr anatakiwa aitumie chance hii kutoa dukuduku lake.

Unataka awashukuru CCM kwa kuchakachua??
 
😎Mtakumbuka vizuri kuwa Mashehe, maaskofu na wachungaji walihubiri muda wote wa kampeni na wengine kabla ya kampeni kwa waumini wao kuwa msiwachague viongozi mafisadi, chagueni viongozi wanaojali maslahii ya kitaifa, sasa kipimo cha ukomavu wa kiroho na dhamira njema ya kiungwana watashiriki na kumwombea dua njema kiongozi anayewatetea mafisadi? Changamoto kwenu. Tutaonana uwanjani:A S-baby:

Wanabodi,

Matokeo ya Urais kwa Majimbo Tanzania, yanakamilika usiku huu ambapo mshindi JK atatangazwa rasmi kesho saa 10 jioni pale kwenye viwanja vya Karimjee na kuapishwa Rasmi Jumamosi Saa 4:00 asubuhi kwenye Uwanja wa Taifa.

Tegemea kuwaona kina Dovutwa, Mziray, Mtamegwa, Rungwe na Lipumba, wakiwa kwenye colourful dress tayari kumpongeza JK kwa genuine smilling faces.

Dr. Slaa anatakiwa sana awepo. Mlio karibu nae, mshaurini asisusie, kweli asisaini kuyakubali matokeo, lakini awepo mahali hapo kuwasilisha live protest yake kwa wahusika for the sake of umoja wa kitaifa.
 
Mkuu Pasco, kwa hiyo Kikwete aliwanadi Lowassa, Chenge, Rostamu na Mramba kulinda umoja wa Kitaifa na sasa unamtaka na Dr. Slaa afanye hivyo hivyo eti kulinda umoja wa Kitaifa. Pasco thanx but no thanx, kama kulinda umoja wa Kitaifa ni kubariki dhulma, wizi na ulaghai basi namshauri Dr. Slaa akae nao mbali kwani vitendo hivyo ndivyo tunavipiga vita. Pasco, kitendo cha Seif kilikuwa cha kinafiki na amewasaliti wana mageuzi popote walipo lakini sishangai kwani baada ya kugombea mara nne na kukosa amegundua kuwa hawezi kuwashinda kwa hiyo ameamua kuungana nao. Kwetu wanamageuzi hivi sasa tumemweka kundi moja na mafisadi tunaowapiga vita.
 
chadema wacheni unafiki!!! Mbona mwaka 2005 mbowe alihudhuria kuapishwa kwa jk wakati lipumba alisusia kutokana na kile kilichoitwa ushindi wa kishindo? Sasa tofauti ya uchaguzi ule na huu ni upi? Sasa kama lipumba atahudhuria na slaa akisusia cha ajabu ni kipi hapo?

sasa chadema mnamshangaa lipumba na wapinzani wengine kuhudhuria kuapishwa kwa jk wakati mbowe nae aliwasaliti wenzake kwa kuhudhuria hafla ya 2005?

chadema mna kaunafiki fulani hivi kalikojificha na mnajiona kuwa nyinyi ndio wapinzani halali zaidi ya wenzenu na pale mnapoambiwa hamuwezi kuishinda ccm bila ya kushirikiana na cuf huwa mnakuwa na kigugumizi fulani hivi!!!

sasa hasara yake ndio hiyo mlitamba kuwa mnaweza kuiondoa ccm pekeyenu kwa kumtegemea slaa ambae tayari alikuwa ameshajidhalilisha kwa kashfa mbaya sana ya kimaadili kwa mtu mwenye hadhi kama yake!!!
 
Mkuu Pasco, kwa hiyo Kikwete aliwanadi Lowassa, Chenge, Rostamu na Mramba kulinda umoja wa Kitaifa na sasa unamtaka na Dr. Slaa afanye hivyo hivyo eti kulinda umoja wa Kitaifa. Pasco thanx but no thanx, kama kulinda umoja wa Kitaifa ni kubariki dhulma, wizi na ulaghai basi namshauri Dr. Slaa akae nao mbali kwani vitendo hivyo ndivyo tunavipiga vita. Pasco, kitendo cha Seif kilikuwa cha kinafiki na amewasaliti wana mageuzi popote walipo lakini sishangai kwani baada ya kugombea mara nne na kukosa amegundua kuwa hawezi kuwashinda kwa hiyo ameamua kuungana nao. Kwetu wanamageuzi hivi sasa tumemweka kundi moja na mafisadi tunaowapiga vita.
Something that is much more scarce than ability is the ability to recognize ability.
 
Love you very much Zubeda.

Rais wetu Dr. wa kweli Slaa (PhD) kwenye sherehe ya wizi wa NEC, haji.

Mtabembeleza sana na hamumuoni. Na kampeni kwenye Umoja wa Mataifa na vyombo vya kupigania haki ndiyo utaanza. Mabalozi watapewa kopi ya wizi wenu, Obama atapata, EU nao watapata.

Kwa hili mlie tu maana mtabembeleza na hakuna kitu Mpenzi wangu. Slaa siyo Maalim Seif Hamad, kachumbali la mafisadi. Hapa mnacheza na kitu ingine kabisa na mtajuta milele kumfukuza Slaa ndani ya CCM.

kazi ndiyo inaanza. Kila wakienda nje ya nchi, jamaa watakuwa wanawasubiri.

Ngoja siye tujikalie tu huku Shamba tulime Tumbaku kwa wingi ili mpate hela ya Kodi na mzidishe vitambi.
 
]

“UTAJIRI unaotokana na wizi wa mali ya umma, na wizi wa fedha za kigeni na unyonyaji na uharamia wa aina mbalimbali, hautupunguzii umaskini wetu, bali unauongeza. Chama chetu hakiwezi kuikubali hali hii, na kikaendelea kuwa CCM, na wala kisitazamie kuwa wananchi wataendelea kukikubali” (Mwalimu Nyerere, Oktoba 1987).

MAFISADI KAZI KWENU WATANZANIA WAMEAMKA NA SASA WANATAKA NCHI YAO. SIKU INAKUJA TUTAWAHUKUMU NA MTAFIA MAGEREZANI MLIKOWEKA WANYONGE MLIOWAIBIA UTAJIRI WAO MKAWALAZIMISHA WAIBE KUKU ILI KUJIKIMU. Mungu ibariki Tanzania tupe nguvu ya kuendelea kupambana bila kuchoka na hawa mafisadi wanaoendelea kutuibia bila huruma !! AMEN

Swali langu kwa Mh. Raisi Kikwete: Je ulipoapa na tena ukashika msahafu na pia Katiba ya nchi, je, uliapa kulinda mali na rasilimali za Tanzania au ni kuziweka chini ya wageni na hasa mafisadi ambao sasa wanaendelea kuitafuna tanzania bila kushibisha matumbo yao ? Naomba utafakari haya na ukiendelea kuiweka Tz chini ya mafisadi, miaka 5 siyo mingi. Watanzania tutakuhukumu siku moja kwenye mahakama zetu au zile za kimataifa !!!!

M. Abdallah Salehe
 
sasa ndio mtashuhudia UJEURI WA GHARIB BILAL.............jamaa ni JEURI SIJAPATA KUONA.............
 
wabunge wa chadema .. kama slaa akikataa kumtambuwa RAISI WETU MTEULE DR. J.K ,, Inabidi na nyinyi msuse kula kiapo chini yake msiende bungeni, kama walivyofanya CUF! ..

SERIOUSLY..
CHADEMA HAKUNA KITU , CHAMA MAARUFU KWENYE BAADHI YA MIKOA , BADO MNALILIA KWAMBA NYIE MMESHINDA KITI CHA URAIS! KAMA NI WAPINZA WA KWELI FANYENI KAMA WALIVYOFANYA CUF! MSIINGIE BUNGENI..:tape:
 
Wee kweli njiwa haswa. Kazi kuchukua SALAMU na kuzipeleka kwa bwana wako.

Hakuna mtu anayesema Slaa kashinda. Ila tunashangaa pamoja na Kikwete kushinda kwa asilimia hamsini na kitu (kihalali), kwa nini wamebadilisha ili ionekane kashinda kwa kishindo na Slaa kuzipunguza ili ionekane ni dhaifu? Hapo hapo mnampa umaarufu Lipumba ambaye kama alivyo Seif Hammad, milele hatakuja kuwa Rais hata makamu wa Rais ila ataendelea kugombea Urais wa Tanzania hadi abakize meno mawili mdomoni.

Mngeliweka namba za kweli za Urais, sasa hivi tungelikuwa tunaongelea kuchakachua tu kura za Ubunge na Slaa angelikuja na hizo asilimia 40 na kitu kwenye sherehe.

Mwisho si lazima yeye aje kwenye sherehe. Watakuja wenyeviti wa Vyama. Yeye ni katibu wa chama si lazima aje. Atafika hapo Mbowe kuja kumuwakilisha. Ila ili kuonyesha dharau kwenu, tutamleta Mpendazoe au dada yetu Regia ili kila mkimuona na ulemavu wake, musikie uchungu wa Unyama mliomfanyia. Ila tatizo, Chogo la mwanasiasa halina haya...........

wabunge wa chadema .. kama slaa akikataa kumtambuwa RAISI WETU MTEULE DR. J.K ,, Inabidi na nyinyi msuse kula kiapo chini yake msiende bungeni, kama walivyofanya CUF! ..

SERIOUSLY..
CHADEMA HAKUNA KITU , CHAMA MAARUFU KWENYE BAADHI YA MIKOA , BADO MNALILIA KWAMBA NYIE MMESHINDA KITI CHA URAIS! KAMA NI WAPINZA WA KWELI FANYENI KAMA WALIVYOFANYA CUF! MSIINGIE BUNGENI..:tape:
 
Seif kapewa ulaji.... anaamini kuwa atawasilisha matatizo ya wapemba vizuri right now (chukulia kuwa Shein ni mpemba).

Upande wa JMT, hali ni tofauti.
Walichokifanya ccm na mafisadi wa NEC ni zaidi ya maelezo. Dr Slaa kwenda huko ni ku-dignify upuuzi.

Kama ni kuongea, Dr Slaa anaweza kuitisha mkutano wa waandishi wa habari anytime na akasema chochote kile anachotaka kusema.

BTW- kulingana na sheria za nchi, baada ya NEC kutangaza matokeo kesho, ndiyo imetoka hivyo.

Hakuna appeal au chochote kitakachobadili matokeo.

Ndo maana nimebadili signature yangu from now on

Ni kweli ulivyosema kwani katiba iko wazi kuwa tume ya uchaguzi ikishatangaza matokeo hakuna mahakama yoyote inayoweza kuhoji! Vyama vya ushindani vipiganie kubadili katiba na kuundwa kwa tume huru vinginevyo vitaendelea kuwa wasindikizaji kwenye urais.
 
Naomba niji quote..
Pasco
Mbona unaendekeza unafiki wewe, unalaumu kuwepo kina Lipumba then unashauri na Slaa awepo!!any way kwa mtu mwenye akili anakuelewa uko wapi na una maana gani, umoja wa kitaifa my ass!!!
 
Naomba niji quote..
How can we be united by these thugs? I was expecting such typical Tanzanians hypocricy. WE rigged, their votes, we bombed them; but still they are with us; that is the way we should be doing; we steal their money, they don't eat enough; they don't get better education; but still they forget easily; TYPICAL Tanzanians and Congratulations DR, Amiri Jeshi Mkuu; Dictator Jakaya Mrisho KIKWETE!!!!!!!!!!!!!!!

OHHHHHHHHHHHH typical we are!
 
Pasco
Mbona unaendekeza unafiki wewe, unalaumu kuwepo kina Lipumba then unashauri na Slaa awepo!!any way kwa mtu mwenye akili anakuelewa uko wapi na una maana gani, umoja wa kitaifa my ass!!!
Kiraka, hivi can't we comment on objectivity and impartiality bila kuwa imotional na kuitana 'wanafiki'?. Hivi nimelaumu uwepo wa Lipumba?, I stand to be corrected.

Najua members wengi humu ni wale wa 'either you are with us or against us', hivyo sisi wote tunaosimama on the fance ndio wanafiki?.
 
Sidhani kam Dr. Slaa au Mbunge yeyote wa Chadema anastahili kwenda kwenye kuapishwa; si kwa ajili ya kumpinga JK hasa bali kwa ajili ya kupinga kitendo cha tume kuuvuruga uchaguzi huu. Binafsi naamini yote haya yasingetokea kama tungekuwa na tume huru kweli na ambayo inafanya kazi kwa weledi. CHADEMA wakienda hapo watawapa heshima tume ambayo kwa wakati huu hawastahili na inaonekana hawako tayari hata kufikiria kuwa ni kutokana na wao (tume) nusura taifa liwake moto. Sijaamua kufyatuka bado lakini hawa tutawasema kwa uhakika.
 
Dr Slaa akatafute nini huko aende Kiravu na babu yake Lewis waliovuruga uchaguzi
 
Back
Top Bottom