Mark Mwandosya hawezi kuwa Waziri Mkuu. Sijui wewe ni mshauri wa namna gani? Ndugu Mwandosya ndiye aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano ile ajali spectacular ya treni ilipotokea Msalala,Dodoma.
Kikwete angeniombia mimi nimshauri kuchagua baraza la mawaziri,sijui kama ningeweza,kwani siwafahamu kabisa hawa wabunge. Pale katika orodha ya wabunge namfahamu Mussa Azan Zungu tu,kwa vile alikuwa school mate Tambaza.
Lakini nimeuliza kwa watu tofauti,kuhusu nani anafaa achaguliwe kuwa Waziri,yaani katika kuleta sura mpya katika Cabinet. Hakuna sababu sana ya kuwataja wabunge mashuhuri maka Anna Tibaijuka au Anne Malecela. Hao kazi yao inajulikana na Watanzania. Hao watu wengi wanategemea kuwaona katika Cabinet ijayo. Kama tunaoongelea kuhusu star search,talent hunting,talent spotting. Ukiwauliza watu wanaowafahamu baadhi ya wabunge wakushauri,wanakushauri kwa kutokana na kama wao ni marafiki na Mbunge,kwa hiyo hiyo inakuwa siyo njia scientific ya kumpata Waziri. Ina maana kwamba lazima upate ushauri kutoka kwa watu wengi.
Lakini nimeuliza kidogo kupata majina ya nani ambaye anaweza kuwa Waziri,na haya ndiyo majina niliyoyapata,
Telele wa Ngorongoro,Jenista Mhagama,Donald Max wa Geita Mjini,Mathayo Daudi wa Same Magharibi,Nyalandu wa Singida Kaskazini.