Elections 2010 JK na Standby Generator za Mgodini Nzega

Domhome

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2010
Posts
3,198
Reaction score
3,950
Nimepewa taarifa ya kuwa leo JK, yupo Nzega kwaajili ya Kampeni za kujinadi yeye mwenyewe, Mgombea wao wa Ubunge(Hamisi Kigwangala) pamoja na Madiwani wa CCM.

Mkutano huo wa Kampeni utafanyika kwenye uwanja wa Samora huko Nzega mjini na gari lao la TOT (Captain John Komba) lipo huko toka jana.

Nimejulishwa pia kuwa Mgodi wa Dhahabu wa Lusu umetoa standby generator ambazo zitatumika iwapo tu umeme wa TANESCO utakatika, na kuwa jenereta hizo zilikuwa uwanja wa kampeni toka jana jioni na mmoja wa madereva wa mgodi huo alilala wanjani hapo kuzilinda usiku kucha!!

Je, hivi Lipumba au Dr. Slaa nao wakija hapa Nzega watapewa hizo standby generator kwaajili ya kufanyia kampeni?

Nitaendelea kuwajuza mambo yanavyoendelea huko Nzega kadri nitakavyopata habari!
 

Is there anything wrong with that?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…