Wanaotukana kwa nguvu zote sijui wana utetezi gani. Kama ni kweli, aliyeowa ni Kikwete, yes! Lakini huyu Kikwete ni Rais wa nchi. Kama anaheshimu urais basi lazima achague matendo ya kufanya hata kama sheria iko kimya.
Lazima achague lugha/maneno ya kutumia, lazima achague mavazi yake, lazima nywele ziwe kwa mtindo unaokubalika, anywe pombe sehemu maalumu na hata urafiki na watu maalumu.
Ni haki yake kuowa lakini ni kuwakosea adabu waliomuweka ikulu kwa kuamua kuowa kila kona ya nchi, umri wowote, nk.
Tena eti kuna watu wanasema Uislamu unaruhusu sijui nini...... Kwani yuko hapo kama kiongozi wa Dini au muumini mzuri? Yuko hapo kama Rais. Akitaka mambo ya Ukristu au Uislamu mzuri aachane na kazi yetu, aingie mtaani. Hata aanzishe mdundiko hakuna atakayeuliza ni kwa nini.