Elections 2010 JK - Ni matusi kudai sijali wafanyakazi!!! Mh!

Elections 2010 JK - Ni matusi kudai sijali wafanyakazi!!! Mh!

Mimi na mke wangu ni wafanyakazi wa uma na kura zetu ni kwa JK.

Duu ulifikiri uko peke yake??? Sema mke wetu maana tuko wengi hapo..mimi jana tulikubaliana kumpa Dr. Slaa...huyu mke wetu atatuchanganya sana mwaka huu....
 
Wafanyakazi msimamo wetu uko palepale wa kutompa kura CCM na JK wake.

Anazidi kutuudhi, tuna mipango mingi ya kumnyima kura
Ni nyie waanachama wa chadema ambao hamtompa kura Kikwete,wengine 80% tuliobakia tumepenga na kuazimia kumpa kura mkwere amalizie kazi aliyoianza.Sasa nyie na huyo padre wenu mtaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua!Ukichukia chukua sumu ujiueeeee!
 
Ohh wamekwisha anza!!!...mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...nadhani kauli ya JK kila mwenye masikio alisikia na kila mwenye akili timamu alitafsiri kwa upeo wa akili yake . sasa nashangazwa na watu timamu walio makini kulishwa maneno na kutaka jamii iamini kile wanachokiamini wao..ni busara kila mtu apewe nafasi achuje pumba na mchele ni upi. si busara kutaka wote wafanane mitazamo juu ya kauli ya JK coz kila mtu anajua kutafsiri kilichosemwa hivyo si HAKI kumshawishi mtu asimpe kura mgombea yeyote (hata JK) kwa kuwa tu yeye binafsi hakufurahishwa na kitu fulani au kauli fulani (kama mjadala huu ulivyo). nakumbuka alisema yuko radhi kuzikosa kura za wafanyakazi na Mgaya akasema JK kazikataa kura za wafanyakazi...nasi sote tumeingia kwenye malumbano juu ya kauli hizi za JK na Mgaya...kwanini tusitumie busara zetu kuamua mambo?(mf kumpa au kumnyima kura mgombea)...kama hatuwezi basi ijulikane kabisa kuwa hapa kuna namna fulani ya kampeni dhidi ya JK na chama chake..iwekwe wazi ili wachangiaji wajue mada hizi zinatumika kupigia debe chama fulani coz nimeona watu wanachangia kwa ku-base judgement zao kwenye tafsiri moja tu ya kauli ile ( tafsiri ya Mgaya) wakti ambapo kabla mgaya hajazungumza mtazamo huo haukuwepo je ndio kusema watu hawakuelewa kama alivyoelewa mgaya toka mwanzo mpaka alipozungumza? hii inanipa hofu kuwa kuna mengi tutajikuta tunaamua kwa kusikia flani kasema basi nasi tunachukua mtazamo huo kama wetu na kujikuta tunaafanya maamuzi yasiyo sahihi...tubadilike kila mtu awe na mtazamo wake juu ya jambo husika kwa kulifanyia uchunguzi wa kina na ndipo ufanye uamuzi.
So,kila mtu achague kiongozi amtakaye kwa kumsikiliza na kushawishika na sera zake na si kwa kuambiwa na mtu mwingine kama wengine wanavyojaribu kuwaambia wafanyakazi wasimpe kura JK...all in all, maisha yako si ya mwenzako so waweza kushawishi kundi fulani lisimpe kura na mwishowe wakampa nadhani itauma zaidi kwani kura huwa ni siri so huwezi jua, pia unaweza kushawishika kumbe aliekushawishi hana shida kama zako..(ofkoz hatulingani hata kama wote tuna shida)... kila mtu atumie haki yake ya kuchagua kiongozi amtakaye yeye na si kuchagua kwa kuwa wanaJF wachache wameamua huo ndio uwe msimamo wa JF na wafanyakazi walio JF.
 
Lakini whatever the case JK will never succeed on this case na kadri anavyojitetea ndivyo anavyopandisha machungu ya wafanyakazi na ndivyo anavyozidi kuzipunguza kura.

USHINDI NI LAZIMA
nitakutafuta ROHO ZIKIFIKA siku za mwanzo za November,,wakati huo MNALIA LIA..... patamu hapo...
 
Wafanyakazi wamekuwa kama watoto wanavyodeka na kuomba mambo yasiyowezekana kwa baba ndani ya familia.Na JK kama baba anawadekeza na kuwabembeleza huku akiwaambia kuwa uwezo wake ni mdogo kuwanunulia chocolate ila anawaletea pipi za maziwa!Wao wanazidi kudeka na kudai chocolate na hatimaye baba Jk anakasirika,"Kama hamtaki kula pipi,basi shauri yenu"

Watoto wanatishia kutokwenda shule kama hawatapewa chocolate,watatafuta baba wa kufikia ili awapatie wanachokitaka! hadithi ya TUCTA na JK !

Akili ni nywele kila mtu ana zake!
 
I think JK is trying to clever by half, I am afraid. Aliyasema mchana kweupe na best course of action is to apologize and I am sure the workers will forgive him and vote for him. Short of that he deserves their wrath. Wakimpa kura bila kutubu akipita watakiona cha mtema kuni. Believe me JK akishinda atakuwa mtu mwingine kabisa katika 2010-2015. Worse than his immediate predecessor.
 
nimemsikia jana mpaka nimetaka kucheka..anakana kuwa hakusema hazitaki kura za wafanyakazi..hahaaaa JK kazi unayo maneno yako ya kuropoka ropoka sasa ngoma ndo hiyo...we si uliwaita wafanya kazi mbayuwayu

Aisee kigogo mie nilicheka sana nilipomsikia ...yaani as if hakutamka hivi watanzania anaona bado hamnazo sana ama?
 
Mimi nashauri Mgaya na viongozi wa TUCTA wanyamaze tu wasijibizane naye wao wameshamaliza jukumu ni letu wafanyakazi tutakutana na JK kwenye sanduku la kura.

Najua JK kuzikataa kura za wafanyakazi lime mtachi sana sasa anatafuta pa kutolea hasira na tageti ni Mgaya ajibu halafu aagize vyombo vya sheria vimkamate ili kuwatisha wafanyakazi.

Lakini whatever the case JK will never succeed on this case na kadri anavyojitetea ndivyo anavyopandisha machungu ya wafanyakazi na ndivyo anavyozidi kuzipunguza kura.
Ana hasira nyingi tena hata ya kunyimwa mwaliko pia inamsumbua. Kura za wafanyakazi kazikosa wacha laielie
asubiri za wale waliopewa elfu kumi ili wahudhurie mkutano pale jangwani
 
Wafanyakazi msimamo wetu uko palepale wa kutompa kura CCM na JK wake.

Anazidi kutuudhi, tuna mipango mingi ya kumnyima kura
.

Wafanyakazi msirubuniwe na wana CHADEMA mahasimu wa CCM. Serikali siyo chama cha siasa Mpatieni KIKWETE kura zenu. Hiyo ni kete ya CHADEMA. Rais amekiri kwamba anahitaji kura zenu na kwamba wanaosema hazitaki ni waongo.
 
sio kweli kwamba mwenye grosari hawezi kulipa mshahara wa 300,000/= mbona wenye grosari hizo wakiwa na vimada au malyoo wao waawanunulia vitu vya thamani n,k kwa fadi hiyo hiyo ya grosari. Kilichopo tabia ya mfanyakzi kutothaminiwa inaanzia serikalini na kurithiwa na wafanyabiashara ambao wengi wao ni wanasiasa, watendaji wa serikali n.k. HIVYO NI UKWELI MTUPU KWAMBA CCM HAITHAMINI WAFANYAKAZI NA WAKULIMA WA NCHI HII. MATHALANI WENYE BIASAHRA NA VIWANDA KUPITIA CHAMA CHA WENYE VIWANDA (CTI) KILA MWAKA HUPATIWA FURSA YA KUWASILISHA MAPENDEKEZO YAO KABALA YA KUANDALIWA KWA BAJETI NA NDIO HUPELEKEA SERIKALI KUPOTEZA MAPATO MAKUBWA KWA NJIA YA MISAMAHA YA KAODI N.K; NI KATIKA MIKUTANO YA AINA HII SERIKALI HUKEMEWA ISIONGEZE MISHAHARA KWA WAFANYAKZI SEKTA YA BINAFSI N.K

kAMA KWELI JK NA CCM WANWATHAMINI WAFANYAKAZI MBONA HAWAWAPATII NAFASI KAMA HIYO? NA HATA WAKIKUTANA NA KUKUBALINA KIMA CHA CHINI KIWE KIAS KADHAA SERIKALI INATANGAZA KIASI TOFAUTI AMBACHO NI PUNGUFU?

SAFARI HII WAFANYAKAZI HAKUNA KUDANGANYIKA NI KUPIGA CHINI!!!!!!! WAIBA KURA LAKINI MOYONI WANAJAU TUMEWAKATAA.

DAWA YA CCM NI KUCHAGUA UPINZANI. TAZAMA MKOA WA KILIMANJARO MAJI HADI VIJIJINI, BARABARA ZA LAMI HADI VIJIJINI, UMEME HADI VIJIJINI NA KILA KITU NI KILIMANJARO KWA SABABU WANA ATBIA YA KUCHAGUA WABUNGE WA UPINZANI HIVYO CCM HUFANYA KAZI YA ZIADA KUREJESHA MAJIMBO HAYO KWA KUWAPATIA HUDUMA LUKUKI.

KABL YA LYATINGA MREMA KUSHINDA UBUNGE JIMBO LA TEMEKE, WILAYA NZIMA YA TEMEKE ILIKUWA NA TATIZO SUGU LA BARABARA, BAADA YA KUMCHAGUA LYATONGA MREMA, CCM ILIFANYA JITIHADA KULIREJESHA JIMBO HILO KWA KUTENGENEZA BARABAR ZA LAMI TEMEKE YOTE NA HADI LEO HII CCM INAWATAZAMA WAKAZI WA TEMEKE KAMA MBONI YA JICHO ILI WASIRUDIE TENA KUCHAGUA UPINZANI. hAYA MAJIMBO MENGINE AMBAYO MIAKA NENDA RUDI WANACHAGUA CCM KWA KISHINDO WAMEPATA NINI?
 
Kwani ahadi anazotoa Dr. Slaa na wanasiasa wengine wa upinzani mmewekeana mikataba?

Siasa sio mkataba wa kisheria ni wangapi wameahidi kwa kauli za mdomo na hawakutekeleza. Mpatie kura yako mgombea ambaye unaona ana sera nzuri na kura iwe siri yako.
 
Ingefaa aeleze mshahara wa kima cha chini umepanda kwa asilimia ngapi, na bei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya taa sukari unga nk. zimepanda kwa asilimia ngapi!
Kwa kifupi huwezi kupandisha mshahara kwa zaidi ya 100% na bei ya bidhaa ipande kwa zaidi ya 300% halafu useme unajali wafanyakazi!

Hata kama Rais Kikwete ana mapungufu yake kama ilivyo kwa Marais wote bado inabaki katika kumbukumbu za nchi hii hadi sasa kwamba ndiye Rais kwa kwanza tangu uhuru aliyeongeza mishahara wa wafanyakazi kwa asilimia kubwa ndani ya miaka mitano.
 
Na hizo dawa anazozungumzia mbona hakuna, ukienda kwenye zahanati na hospitali za wilaya, ni aibu, watu wa chini wanateseka sana jamani

Nenda Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Tukuyu utashuhudia kile ambacho rais anasema. Madawa bwelele, vitanda bwelele na chumba kipya cha kisasa cha kuhifadhi maiti badala ya kile cha zamani kipo tele. hakuna serikali duniani iliyoweza kumaliza matatizo yote ya wananchi wake kwa wakati mmoja hata marekani kuna ombaomba mtaani.
 
Ohh wamekwisha anza!!!...mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...nadhani kauli ya JK kila mwenye masikio alisikia na kila mwenye akili timamu alitafsiri kwa upeo wa akili yake . sasa nashangazwa na watu timamu walio makini kulishwa maneno na kutaka jamii iamini kile wanachokiamini wao..ni busara kila mtu apewe nafasi achuje pumba na mchele ni upi. si busara kutaka wote wafanane mitazamo juu ya kauli ya JK coz kila mtu anajua kutafsiri kilichosemwa hivyo si HAKI kumshawishi mtu asimpe kura mgombea yeyote (hata JK) kwa kuwa tu yeye binafsi hakufurahishwa na kitu fulani au kauli fulani (kama mjadala huu ulivyo). nakumbuka alisema yuko radhi kuzikosa kura za wafanyakazi na Mgaya akasema JK kazikataa kura za wafanyakazi...nasi sote tumeingia kwenye malumbano juu ya kauli hizi za JK na Mgaya...kwanini tusitumie busara zetu kuamua mambo?(mf kumpa au kumnyima kura mgombea)...kama hatuwezi basi ijulikane kabisa kuwa hapa kuna namna fulani ya kampeni dhidi ya JK na chama chake..iwekwe wazi ili wachangiaji wajue mada hizi zinatumika kupigia debe chama fulani coz nimeona watu wanachangia kwa ku-base judgement zao kwenye tafsiri moja tu ya kauli ile ( tafsiri ya Mgaya) wakti ambapo kabla mgaya hajazungumza mtazamo huo haukuwepo je ndio kusema watu hawakuelewa kama alivyoelewa mgaya toka mwanzo mpaka alipozungumza? hii inanipa hofu kuwa kuna mengi tutajikuta tunaamua kwa kusikia flani kasema basi nasi tunachukua mtazamo huo kama wetu na kujikuta tunaafanya maamuzi yasiyo sahihi...tubadilike kila mtu awe na mtazamo wake juu ya jambo husika kwa kulifanyia uchunguzi wa kina na ndipo ufanye uamuzi.
So,kila mtu achague kiongozi amtakaye kwa kumsikiliza na kushawishika na sera zake na si kwa kuambiwa na mtu mwingine kama wengine wanavyojaribu kuwaambia wafanyakazi wasimpe kura JK...all in all, maisha yako si ya mwenzako so waweza kushawishi kundi fulani lisimpe kura na mwishowe wakampa nadhani itauma zaidi kwani kura huwa ni siri so huwezi jua, pia unaweza kushawishika kumbe aliekushawishi hana shida kama zako..(ofkoz hatulingani hata kama wote tuna shida)... kila mtu atumie haki yake ya kuchagua kiongozi amtakaye yeye na si kuchagua kwa kuwa wanaJF wachache wameamua huo ndio uwe msimamo wa JF na wafanyakazi walio JF.

Mbona unafunikwa utashi wako kwa bendera ya CCM? Hotuba ya JK tuliijadili hata kabla Mgaya hajasema kitu na ofcourse tunayo. Kama unataka kumpa support na kusahau mipasho aliyotoa pale Diamond endelea lakini usipotoshe umma.

By the way mbona hili limemuumiza sana wakati aliongea kwa kujiamini? Huko Mwanza hakuwa na jipya zaidi ya suala la wafanyakazi? Kwani ni hilo tu linalosababisha tumnyime kura, yapo mengi tu. Maana naona habari leo wameandika mambo ya wafanyakazi tu, kwa ujumla hotuba zake hazina mvuto na moto kauwasha mwenyewe.
 
Hata kama Rais Kikwete ana mapungufu yake kama ilivyo kwa Marais wote bado inabaki katika kumbukumbu za nchi hii hadi sasa kwamba ndiye Rais kwa kwanza tangu uhuru aliyeongeza mishahara wa wafanyakazi kwa asilimia kubwa ndani ya miaka mitano.

Asilimia kubwa kulinganisha na nini. Nipe figure ya inflation kwa sasa. Toa analysis ya purchasing power ya hiyo 135,000 anayolipa na 48,000 aliyoiacha Mkapa. Mfa maji hata kama hajui sarakasi atapiga tu. Amesahau hata principal ndogo tu za uchumi na amesoma uchumi huo huo? Kazi imeanza. Wafanyakazi hatudanganyiiiikiii!!!!!!!!!!!!
 
Kuongezeka kwa msahara kuna faida gani kama mfumuko wa bei ni mkubwa kiasi cha wananchi kushindwa kumudu gharama za maisha.
Kuongeza mshahara kuna faida gani wakati kodi ni kubwa mno. Mfanyakazi anakatwa kodi zaidi ya mfanyabiashara eti kwa sababu mfanyakazi hawezi kukwepa kulipa hiyo kodi.
 
Mkuu LK, hapa umenifanya nicheke mwenyewe kwa hizi nahau na misemo yako..
Lakini umeongea ukweli mtupu kupitia tamthilia

Anayo haki JK kulambisha maneno alambishayo. Wafanyakazi mmekuwa mkipiga makelele daima dumu, anajua mnataka kubembelezwa na kaamua aropoke aropokayo kwenu, anajua mtampa kura zenu tu. SI mnajua mbwa mkali hapigi makelele bali anang'ata silently? Ukiona mbwa anakubwatukia sana na kukuonyesha meno yake yote mdomoni ujue anakutishia tu, hana lolote la kukufanya. Debe tupu hamjui linavyotika? Mlevi anapiga makelele mengi ili kujihami tu, hata bila kumgusa utamkuta anajifanya kukupiga teke lakini anapiga hewani na kudondoka pasipo kuguswa.

Wafanyakazi mweleweni JK, mnapaswa kumjibu kwa vitendo kwa kumrudi siku ya uchaguzi kama kweli mko serious. Mnajidai watu wa vijijini ndio watakaompatia kura nyingi kwa ujinga wao, sasa tudhihirishieni kama nyie mlio wasomi mtacheza role model wajinga wajifunze kwenu. Kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi, kama vile kelele za vyura kudai maji yote ni yake hazimzuii tembo kunywa maji yale, hata kama chura ataamua kukojolea na kunyea humo humo ili kukomoa.

Wake up wafanyakazi, kulialia hakuleti tija. Will you?
 
Back
Top Bottom