Mimi na mke wangu ni wafanyakazi wa uma na kura zetu ni kwa JK.
Ni nyie waanachama wa chadema ambao hamtompa kura Kikwete,wengine 80% tuliobakia tumepenga na kuazimia kumpa kura mkwere amalizie kazi aliyoianza.Sasa nyie na huyo padre wenu mtaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua!Ukichukia chukua sumu ujiueeeee!Wafanyakazi msimamo wetu uko palepale wa kutompa kura CCM na JK wake.
Anazidi kutuudhi, tuna mipango mingi ya kumnyima kura
Lakini whatever the case JK will never succeed on this case na kadri anavyojitetea ndivyo anavyopandisha machungu ya wafanyakazi na ndivyo anavyozidi kuzipunguza kura.
nimemsikia jana mpaka nimetaka kucheka..anakana kuwa hakusema hazitaki kura za wafanyakazi..hahaaaa JK kazi unayo maneno yako ya kuropoka ropoka sasa ngoma ndo hiyo...we si uliwaita wafanya kazi mbayuwayu
====
Mbona mke wako kaniambia haimpi JK! Sasa amua wewe nani mkweli kati ya mke wako au mimi niliyeambiwa na mke wako.
Ana hasira nyingi tena hata ya kunyimwa mwaliko pia inamsumbua. Kura za wafanyakazi kazikosa wacha laielieMimi nashauri Mgaya na viongozi wa TUCTA wanyamaze tu wasijibizane naye wao wameshamaliza jukumu ni letu wafanyakazi tutakutana na JK kwenye sanduku la kura.
Najua JK kuzikataa kura za wafanyakazi lime mtachi sana sasa anatafuta pa kutolea hasira na tageti ni Mgaya ajibu halafu aagize vyombo vya sheria vimkamate ili kuwatisha wafanyakazi.
Lakini whatever the case JK will never succeed on this case na kadri anavyojitetea ndivyo anavyopandisha machungu ya wafanyakazi na ndivyo anavyozidi kuzipunguza kura.
.Wafanyakazi msimamo wetu uko palepale wa kutompa kura CCM na JK wake.
Anazidi kutuudhi, tuna mipango mingi ya kumnyima kura
Kwani ahadi anazotoa Dr. Slaa na wanasiasa wengine wa upinzani mmewekeana mikataba?
Ingefaa aeleze mshahara wa kima cha chini umepanda kwa asilimia ngapi, na bei ya bidhaa muhimu kama mafuta ya taa sukari unga nk. zimepanda kwa asilimia ngapi!
Kwa kifupi huwezi kupandisha mshahara kwa zaidi ya 100% na bei ya bidhaa ipande kwa zaidi ya 300% halafu useme unajali wafanyakazi!
Na hizo dawa anazozungumzia mbona hakuna, ukienda kwenye zahanati na hospitali za wilaya, ni aibu, watu wa chini wanateseka sana jamani
Ohh wamekwisha anza!!!...mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...nadhani kauli ya JK kila mwenye masikio alisikia na kila mwenye akili timamu alitafsiri kwa upeo wa akili yake . sasa nashangazwa na watu timamu walio makini kulishwa maneno na kutaka jamii iamini kile wanachokiamini wao..ni busara kila mtu apewe nafasi achuje pumba na mchele ni upi. si busara kutaka wote wafanane mitazamo juu ya kauli ya JK coz kila mtu anajua kutafsiri kilichosemwa hivyo si HAKI kumshawishi mtu asimpe kura mgombea yeyote (hata JK) kwa kuwa tu yeye binafsi hakufurahishwa na kitu fulani au kauli fulani (kama mjadala huu ulivyo). nakumbuka alisema yuko radhi kuzikosa kura za wafanyakazi na Mgaya akasema JK kazikataa kura za wafanyakazi...nasi sote tumeingia kwenye malumbano juu ya kauli hizi za JK na Mgaya...kwanini tusitumie busara zetu kuamua mambo?(mf kumpa au kumnyima kura mgombea)...kama hatuwezi basi ijulikane kabisa kuwa hapa kuna namna fulani ya kampeni dhidi ya JK na chama chake..iwekwe wazi ili wachangiaji wajue mada hizi zinatumika kupigia debe chama fulani coz nimeona watu wanachangia kwa ku-base judgement zao kwenye tafsiri moja tu ya kauli ile ( tafsiri ya Mgaya) wakti ambapo kabla mgaya hajazungumza mtazamo huo haukuwepo je ndio kusema watu hawakuelewa kama alivyoelewa mgaya toka mwanzo mpaka alipozungumza? hii inanipa hofu kuwa kuna mengi tutajikuta tunaamua kwa kusikia flani kasema basi nasi tunachukua mtazamo huo kama wetu na kujikuta tunaafanya maamuzi yasiyo sahihi...tubadilike kila mtu awe na mtazamo wake juu ya jambo husika kwa kulifanyia uchunguzi wa kina na ndipo ufanye uamuzi.
So,kila mtu achague kiongozi amtakaye kwa kumsikiliza na kushawishika na sera zake na si kwa kuambiwa na mtu mwingine kama wengine wanavyojaribu kuwaambia wafanyakazi wasimpe kura JK...all in all, maisha yako si ya mwenzako so waweza kushawishi kundi fulani lisimpe kura na mwishowe wakampa nadhani itauma zaidi kwani kura huwa ni siri so huwezi jua, pia unaweza kushawishika kumbe aliekushawishi hana shida kama zako..(ofkoz hatulingani hata kama wote tuna shida)... kila mtu atumie haki yake ya kuchagua kiongozi amtakaye yeye na si kuchagua kwa kuwa wanaJF wachache wameamua huo ndio uwe msimamo wa JF na wafanyakazi walio JF.
Hata kama Rais Kikwete ana mapungufu yake kama ilivyo kwa Marais wote bado inabaki katika kumbukumbu za nchi hii hadi sasa kwamba ndiye Rais kwa kwanza tangu uhuru aliyeongeza mishahara wa wafanyakazi kwa asilimia kubwa ndani ya miaka mitano.
Anayo haki JK kulambisha maneno alambishayo. Wafanyakazi mmekuwa mkipiga makelele daima dumu, anajua mnataka kubembelezwa na kaamua aropoke aropokayo kwenu, anajua mtampa kura zenu tu. SI mnajua mbwa mkali hapigi makelele bali anang'ata silently? Ukiona mbwa anakubwatukia sana na kukuonyesha meno yake yote mdomoni ujue anakutishia tu, hana lolote la kukufanya. Debe tupu hamjui linavyotika? Mlevi anapiga makelele mengi ili kujihami tu, hata bila kumgusa utamkuta anajifanya kukupiga teke lakini anapiga hewani na kudondoka pasipo kuguswa.
Wafanyakazi mweleweni JK, mnapaswa kumjibu kwa vitendo kwa kumrudi siku ya uchaguzi kama kweli mko serious. Mnajidai watu wa vijijini ndio watakaompatia kura nyingi kwa ujinga wao, sasa tudhihirishieni kama nyie mlio wasomi mtacheza role model wajinga wajifunze kwenu. Kelele za mpangaji hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi, kama vile kelele za vyura kudai maji yote ni yake hazimzuii tembo kunywa maji yale, hata kama chura ataamua kukojolea na kunyea humo humo ili kukomoa.
Wake up wafanyakazi, kulialia hakuleti tija. Will you?