Elections 2010 JK - Ni matusi kudai sijali wafanyakazi!!! Mh!


Sio wafanyakazi wote wenye kuweza kunyambua kila linalosemwa na sio wote wanaweza kukotoa hesabu za kisanii za serikali hivyo hapa JF watu hatumpigii debe Dr Slaa Professa Lipumba au JK bali tunajaribu kuchambua kila mmoja anasema nini ili mwenye macho afumbuke asiyenayo aendelee kukaa tu kwenye kiza.
 
USHINDI NI LAZIMA
nitakutafuta ROHO ZIKIFIKA siku za mwanzo za November,,wakati huo MNALIA LIA..... patamu hapo...

Kama mshapiga kura tayari sawa kama bado subirini Oktoba
 

Mie sikatai JK kuna mazuri amefanya but kuna mabaya mengi pia amefanya. Unasema amepandisha vyeo (kwa mujibu wa maneno yako) but hivyo vyeo vimepanda sekta gani? Kuna sekta nyengine watu walikuwa wakilia lia mfano Sekta ya afya au umesahau? Ameongeza mshahara hivi wewe nikuulize swali wakati Mkapa anaondoka madarakani mkate ulikuwa unanunua bei gani? au Nauli ilikuwa bei gani? Sasa hivi ni bei gani? Watanzania wengi sasa wanakula mlo moja kwa siku ndio unayaita maendeleo ya nchi haya? Umesema ameajiri zaidi lakini kinachofanyika serikalini ni kwamba ameongeza mzigo wa gharama wa serikali kwa kuajiri watu wengi zaidi kufanya kazi ambayo ingelifanywa na mtu mmoja. Mfano afisa forodha mikoani unakuta ilikuwa kazi ya mtu mmoja sasa hivi unawakuta vijana wanasinzia tu mkoani wote maofisa forodha ndio ameongeza ajira kwa kuajiri watu wasiochangia katika serikali badala yake kuliongezea taifa gharama za uendeshaji???? Kodi imekusanywa zaidi nikuulize unajua kodi imepanda kiasi gani kipindi hicho? Kuhusu mpasuko wa zanzibar ndio kabisa JK hayumo tusimpe sifa asiyostahili
 

Iliwahi kusemwa hapa JF kwamba ndani ya CCM kuna mpasuko mkubwa na wanachama kadhaa watajitokeza kumpinga kikwete ili asipewe kipindi cha pili na baadhi yetu tukadiriki kutaja majina ya akina Sumaye, Lowassa, Mwandosya, Malecela na wengineo. Kikwete hakupata upinzani wowote ndani ya chama chake na siku ya kuteua mgombea urais ndani ya chama kikongwe cha CCM Kikwete akaibuka na ushindi mnono wa asilimia 99.
 

wewe hutetei uongo Dr Slaa?
 
Na wewe kama umeishiwa kalale utamjuaje huyu ni chadema au CUF, ina maana wewe kwa kumtetea Kikwete umekuwa CCM. Usi generalize mambo humu wewe toa hoja basi kama umeshindwa kutetea uongo wa rais wako mwache mwenyewe aendelee kujitetea.

Na wewe unarudia kosa la mwenzio mbona na wewe umekuja juu kama vile Dr Slaa ni chaguo lako? acha kila mmoja atetee wa kwake kama ndio hivyo. Unadhani JF ni ya Chadema tu na wa vyama vingine wamo humu ndani.
 

Tutajuaje na wewe kama sio kibaraka wa Dr Slaa unayetegemea kunufaika na Urais wake kama ilivyo kwa mwenzako unayedai ni kibaraka wa kikwete?
 
Wafanyakazi tutampa Kikwete kura zetu. Tunasubiri tu vilio humu jf pamoja na kampeni chafu dhidi ya kikwete. hatudanganyiki
Kibaraka wa CCM sema mimi nitampigia kura Kikwete sio tutampigia...Ukweli ni kwamba performance ya Kikwete kwenye uchumi wa TZ ni extremely poor, inflation ambayo ni moja ya kigezo imepanda sana toka aingie madarakani (toka 7%-14%). Dar tu haina maji safi na salama, infact maji tu hakuna!! Purchasing power ya mtz imeshuka sana, watu masikini wameongezeka, wizi na rushwa ndo usiseme ikiwa na maana kuwa serikali yake haina strong institutions ya kuondoa tatizo hilo!!
Wewe mpigie kura ila mie hapana kwa sababu i just do not see a better future with Kikwete as a president.
 
Wafanyakazi tutampa Kikwete kura zetu. Tunasubiri tu vilio humu jf pamoja na kampeni chafu dhidi ya kikwete. hatudanganyiki

Hivi hawa new member wanaotoa statement hizi ndio wanaojiandikisha humu JF kumtetea JK? Anyway safi karibuni but usiseme wafanyakazi sema wewe na akili zako mtampigia JK na sio wafanyakazi. Nakutakia kila la kheri
 

Wapambe wa Rais mtarajiwa Dr Slaa wana matusi sina hakika tukiwapa nchi watatutukana kwa kiwango kipi. Hapo wako nje ya mamlaka ya dola wakipewa je? Ukiona binadamu anashindwa kuzuia hasira zake huko akiimba kwamba yeye ni mtu safi ogopa sana. sio rahisi kusonga mbele kimaendeleo kwa matusi. Wapiga kura kazi kwenu, mimi sidanganyiki. Ikulu ni mahali patakatifu sio pango la matusi.
 
Wafanyakazi tutampa Kikwete kura zetu. Tunasubiri tu vilio humu jf pamoja na kampeni chafu dhidi ya kikwete. hatudanganyiki

Changanya na za kwako. Ukiwa mzima huwezi kumpa aliyekutukana akijua huna umuhimu. Ukimpa basi ujue wewe sio mzima.
 

Kikwete ndiye aliyepandisha mishahara ya madakitari kutoka kima cha chini cha 224,000 hadi 480,000. Hivyo, alipandisha mara mbili (zaidi ya asilimia 100), kiasi hiki si cha kutosha lakini kinajibu nia njema ya Rais kwa wafanyakazi kwamba akipewa muda zaidi atafanya makubwa kwa sekta mbalimbali. Ni makosa kudhani sekta zote za serikali kima cha chini ni 135,000/=. Nenda TRA, Benki Kuu, Ewura, sumatra, tanroads na kwingineko kima cha chini sio hicho. Wapo wafanyakazi wa kutosha kumpa kura kikwete kwa imani kwamba maeneo ambayo hajayafikia kuongeza kima cha chini atafanya hivyo katika kipindi cha pili na alishasema hilo huko nyuma.
 
.

kuhusu suala la maridhiano Zanzibar hata maalimu Seif Shariff Hamad alishakiri na kumpa sifa hadharani kikwete kwamba zanzibar imefika hapo kutokana na kazi na mchango mkubwa wa Rais Kikwete. Wapatanishi wengi waliokomaa duniani hawahitaji kujitangaza lakini vikao vya faragha kati ya viongozi wakuu kitaifa vilifanyika kabla ya kile ulichokuja kukifahamu baadaye. Hebu jiulize kwa nini Rais OBAMA kampongeza sana kikwete kwa hatua hiyo. Hebu jiulize unafikiri Maalim Seif na Karume waliota ndoto ya kukutana Ikulu ya zanzibar bila watu fulani mahali fulani kuwakutanisha kwa siri ili kuinusuru zanzibar? Kumbuka suala la zanzibar lilishindikana katika vikao vya wazi kati ya Seif na Makamba. Usidanganyike kwamba Karume aliamka asubuhi na kumpigia simu maalim Seif kwamba njoo Ikulu ya Zanzibar.
 
Mnaoitwa wafanya kazi amueni la kufanya na rais wenu...maana nyie ndiyo mliokuwa mnaomba kuongezewa mishahara....nyie ndiyo mliokuwa mnasikia hotuba yake kwa hiyo wakisema rais hakusema hivyo mimi ntaripia tv ili watz wasikie tena....
 
Duh! Kwa hiyo wewe na mkeo mmeamua KUMPA JK!
Sio hao tu wengi watampatia kura kikwete huo ndio ukweli wenyewe. Tunaomkubali JK tutawakumbusha ushindi wake. sherehe ya ushindi wa Jk itafanyika kwa siku tatu hapa JF tutaomba wanachadema siku hiyo mjiondoe hewani kwa muda wa siku tatu mkituacha tukijipongeza.
 
Hivi hawa new member wanaotoa statement hizi ndio wanaojiandikisha humu JF kumtetea JK? Anyway safi karibuni but usiseme wafanyakazi sema wewe na akili zako mtampigia JK na sio wafanyakazi. Nakutakia kila la kheri


Hivi hawa members wa zamani hapa Jf ni wa Dr Slaa?
 

wewe ni kibaraka wa nani hapa JF?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…