Elections 2010 JK: Ridhiwani hahusiki kuondolewa Bashe

Elections 2010 JK: Ridhiwani hahusiki kuondolewa Bashe

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa, Rais Jakaya Kikwete amesema hana tatizo na wanachama wa chama hicho wanaohamia vyama vingine,lakini wasijaribu kukihujumu.

Kikwete amesisitiza kuwa,walioenguliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), wataelezwa kwa maandishi sababu za kuenguliwa.

Aidha amesema,mwanawe Ridhiwani hahusiki katika sakata la kuenguliwa kuwania ubunge Jimbo la Nzega, Hussein Bashe kama ilivyoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari.

Rais Kikwete aliyasema hayo Dar es Salaam kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, wakati akiwahutubia mamia ya wanachama wa chama hicho mara baada ya kurejesha fomu zake za kuwania Urais kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Alisema,wakati wa kura za maoni, wengi walijitokeza kugombea, lakini lazima mmoja ashinde na wengine washindwe, lakini wapo waliogombea kwa kutaka washinde wao na hao ndiyo ambao sasa wanahamia vyama vingine.

"Katika uchaguzi lazima mmoja ashinde. Tatizo kuna wagombea waliingia katika ushindani ili wao tu washinde, hiyo ndiyo sababu ya kutaka kuhama…anayehamia kwingine sina haja naye, aende anakotaka, mbaya ni kukihujumu chama," alisema Rais Kikwete jana.

Alisema hata kama aliyegombea hakuridhishwa na mazingira ya namna aliyeshinda alivyoshinda, ndiyo ameshapata,hivyo jambo la msingi ni kuacha makundi yaliyokuwepo wakati wa kura za maoni, bali wajielekeze katika kutafuta ushindi wa kishindo huku wakijiandaa kwa kugombea kipindi kingine.

Kikwete alisema,utaratibu huo wa kura za maoni utaendelea ingawa mchakato ulikuwa na changamoto mbalimbali ambazo wamejifunza na kuwahakikishia kuboresha mapungufu yaliyojitokeza ili yasitokee na wanaendelea kuzichambua kasoro hizo na baada ya uchaguzi watazifanyia kazi.

"Pamoja na mapungufu yaliyojitokeza, mamlaka tuliyowapa wanachama wa CCM hatutawanyang'anya, ila jukumu ni kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwani imesaidia kuwapata wagombea wanaohitajika huku wakijitokeza wanachama wengi kugombea nafasi mbalimbali," alisema.

Kuhusu Bashe, Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alisema kuenguliwa kwa kijana huyo kulifanywa na Kamati Kuu ambayo ilifanya hivyo kwa manufaa ya chama.

Alisema Kamati Kuu hiyo ilijitahidi kuheshimu uamuzi ya wanachama wake, lakini kutokana na sababu mbalimbali kama uraia na utovu wa maadili ambao ungesababisha chama hicho kuanguka katika jimbo husika, walimteua wanayeona anafaa.

Alisema kuna magazeti yanasema maneno mengi ili wanachama wa chama hicho wachukiane na yakishindwa kuona mema ya chama hicho kwa mwaka mzima.

Aliwaomba Makamu wake, Pius Msekwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba kuacha kujibizana katika magazeti, badala yake, majibu yatapatikana katika kura baada ya CCM kushinda kwa kishindo.

Bashe ambaye alikuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana (UVCCM), alienguliwa na Kamati Kuu baada ya kubainika kuwa si raia wa Tanzania, na kutakiwa na NEC kuanza mchakato wa kupata uraia. Anadaiwa kuwa raia wa Somalia na alivuliwa uanachama na kupoteza nafasi zote za uongozi.

Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari vilidai kuenguliwa kwa Bashe aliyeongoza kwa kura zaidi ya 14,000 dhidi ya wagombea wengine wawili, Lucas Selelii na Dk. Hamis Kigwangala, kumetokana na tofauti zake na Ridhiwani ambaye kama Bashe ni Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM.

Aidha, Rais Kikwete aliwataka wana-CCM kutoa jasho katika kutafuta ushindi kwa kupita nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba na hata mtu kwa mtu kuwashawishi wananchi watatu wasiokuwa mwanachama wa chama hicho kupigia kura CCM, hivyo kati ya wanachama milioni tano waliopo, kila mmoja akiwa na watatu, watakuwa wamepata kura milioni 15 ambao ni ushindi wa kishindo.

Mgombea Mwenza wa Rais Kikwete kwa chama hicho, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alisema wamemaliza awamu ya kwanza ya kutimiza masharti kikatiba, sasa wanaanza awamu nyingine kuelezea sera ya chama chao hivyo, aliwataka wanachama kujitokeza katika uzinduzi wa kampeni wa chama hicho utakaofanyika kesho katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

Source:
Habari Leo
 
Kikwete said:
Kikwete alisema,utaratibu huo wa kura za maoni utaendelea ingawa mchakato ulikuwa na changamoto mbalimbali ambazo wamejifunza na kuwahakikishia kuboresha mapungufu yaliyojitokeza ili yasitokee na wanaendelea kuzichambua kasoro hizo na baada ya uchaguzi watazifanyia kazi.

Ahadi nyingine hii... Nachelea kusema utekelezaji wake utakuwa sifuri kama zilivyo ahadi nyingine nyingi alizowahi kutoa. Kwanini kusubiri watu waingie madarakani kwa 'changamoto bin rushwa' mbalimbali halafu ndiyo kushughulikia utomvu huo?? GIGO!! Garbage In = Garbage Out! Hao watakaoingia madarakani kwa rushwa wataendeleza rushwa na kujihami msiwashughulikie baada ya kuwa wamepita kinjama kwenye chaguzi!
 
Mbona JK hakueleza kwa nini Seleli ambaye alikuwa mbunge pia kaachwa pamoja na kuwa ndiye mshindi wa pili?..
Uchaguzi ulifanywa na wanachama hivyo majibu ya kumkataa mgombea waliyemchagua ni lazima yarudi kwa wananchi na sio mgombea.
 
eeerrrrm.... ameyasema yafuatayo:
"Pamoja na mapungufu yaliyojitokeza, mamlaka tuliyowapa wanachama wa CCM hatutawanyang'anya, ila jukumu ni kurekebisha kasoro zilizojitokeza kwani imesaidia kuwapata wagombea wanaohitajika huku wakijitokeza wanachama wengi kugombea nafasi mbalimbali," alisema.
In other words, "haitajiki"!!

Sababu nyingine labda yaweza kuwa:
Alisema Kamati Kuu hiyo ilijitahidi kuheshimu uamuzi ya wanachama wake, lakini kutokana na sababu mbalimbali kama uraia na utovu wa maadili ambao ungesababisha chama hicho kuanguka katika jimbo husika, walimteua wanayeona anafaa.

He couldn't be more brunt could he?!! :glasses-nerdy:
 
Alisema kuna magazeti yanasema maneno mengi ili wanachama wa chama hicho wachukiane na yakishindwa kuona mema ya chama hicho kwa mwaka mzima.

Aliwaomba Makamu wake, Pius Msekwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba kuacha kujibizana katika magazeti, badala yake, majibu yatapatikana katika kura baada ya CCM kushinda kwa kishindo.
Kikwete bwana yaani anawaambia Msekwa na Makamba waache kujibizana na magazeti wakati yeye anajibizana nayo, kweli tunalo....
 
Aidha, Rais Kikwete aliwataka wana-CCM kutoa jasho katika kutafuta ushindi kwa kupita nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba na hata mtu kwa mtu kuwashawishi wananchi watatu wasiokuwa mwanachama wa chama hicho kupigia kura CCM, hivyo kati ya wanachama milioni tano waliopo, kila mmoja akiwa na watatu, watakuwa wamepata kura milioni 15 ambao ni ushindi wa kishindo.

Wapinzani, kaeni chonjo!.... Print press around the globe could be busy perfecting just that!!:confused2:
 
For how long JK atakuwa anamtetea mtoto wake kwenye the so called uzushi? Why not UVCCM kuita waandishi wa habari kufafanua hilo? What if this young man was caught on tape somewhere pompously claiming to have done wht he's accused of? Hata kama si kweli kwamba yeye alihusika na hayo maamuzi lakini I see Ridhwani not much different from many Tz youths ambao ku-exaggerate mambo ni hulka ya kawaida especially kwenye social talks?

It is therefore high time kwa JK to be a leader, mambo ya mtoto wake ni ya mtoto wake! Let him deal with it. Sidhani kama hayo magazeti kwa namna yeyote ile yamemtaja JK kupewa habari au kuchochewa na Ridhwani kufanya maamuzi juu ya Bashe.
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa, Rais Jakaya Kikwete amesema,mwanawe Ridhiwani hahusiki katika sakata la kuenguliwa kuwania ubunge Jimbo la Nzega, Hussein Bashe kama ilivyoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari.
Mimi najiuliza leo imekuwaje unajibu magazetii?...Ulikuwa wapi watu walipolalamika ya EPA,KIGODA,RICMOND..etc..ulikaa kimya hukushtuka...je leo unaona bora kumtetea mwanao?...ulikuwa wapi wananchi walpotaka kusikia kemeo lako la fedha nyingi zetu zilzo kupuliwa?...NASIKITIKA SANA...

Kikwete alisema,utaratibu huo wa kura za maoni utaendelea ingawa mchakato ulikuwa na changamoto mbalimbali ambazo wamejifunza na kuwahakikishia kuboresha mapungufu yaliyojitokeza ili yasitokee na wanaendelea kuzichambua kasoro hizo na baada ya uchaguzi watazifanyia kazi.

Huoni kuwa utaratibu huo wenu ni wa kidikteta...Wananchi wanamchagua mtu na nyie mnaweka mtu wa masilahi yenu....je kuna haja gani ya kuara ya maoni?..hamuoni ni ufujaji wa pesa na muda?

Alisema kuna magazeti yanasema maneno mengi ili wanachama wa chama hicho wachukiane na yakishindwa kuona mema ya chama hicho kwa mwaka mzima.

Basi ungetupa hata angalau mema matatu ambacho CCM imefanya kwa mwaka mzima.

Aliwaomba Makamu wake, Pius Msekwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba kuacha kujibizana katika magazeti,

Hapo umejitahidi kwa sababu hawo jamaa wanaongea utumbo tu ni bora wakae kimya
 
maswali yote hayo aulizwe kwenye kampeni,wananchi wenye kufunguka masikio wafunguke
 
JK hiki nacho kichesho, kuwa wahame lakini wasikihujumu chama(CCM).Kama wao mmewahujumu! itakuwaje wao wasiwahujumu pia? Au ni mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu??JK mwache Ridhiwan ajitetee mwenyewe,wewe ni kiongozi wa Taifa; haya unayotoa hayakusitahili kumjibia mwanao,Ridhiwan ni mtu mzima; mwache ajibu yeye.
 
Aliwaomba Makamu wake, Pius Msekwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba kuacha kujibizana katika magazeti, badala yake, majibu yatapatikana katika kura baada ya CCM kushinda kwa kishindo.
Source: Habari Leo

teh teh teh........kumekucha ndo unakumbuka shuka???
 
Aidha, Rais Kikwete aliwataka wana-CCM kutoa jasho katika kutafuta ushindi kwa kupita nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba na hata mtu kwa mtu kuwashawishi wananchi watatu wasiokuwa mwanachama wa chama hicho kupigia kura CCM, hivyo kati ya wanachama milioni tano waliopo, kila mmoja akiwa na watatu, watakuwa wamepata kura milioni 15 ambao ni ushindi wa kishindo.

Hiyo hapo juu: je, mwandishi hajui hesabu au JK; hivi hiyo equation imekaa vizuri kweli? 5,000,000*(1+3)=15,000,000. Yaani hapa amewaambia wana-CCM kila mmoja atafute watu watatu wa kupiga kura halafu aliyewapata hao asipige kura! Kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiri haraka haraka na kwa usahihi kama Dr. Slaa equation ingekuwa hivi: (1+3)*5,000,000=20,000,000. Hiki ndicho alichokuwa akimaanisha bila kufikiria kuwa NEC ina idadi ya wapiga kura 19.67m, sasa hawa 0.33m watatoka wapi. Ni heri angesema 'walau mmoja, wawili au watatu'!! Hivi JK anajua kweli hesabu? Kihesabu amejipa "a word problem" (hesabu za mafumbo) na kushindwa kui-solve! Hivi ndio maana anakimbia mdahalo?! Sasa watanzania mjue kuwa tatizo hili lake ni "just a tip of the iceberg" Kwani hesabu ni logic/ reasoning, hivyo kushindwa kuifanya hesabu nyepesi ni sawa na kushindwa kuona au kutengeneza logic/ ku-reason; sasa mambo makubwa ya nchi anayaweza? Ushahidi tunao hayawezi!!!

Hivi unamjuaje mwanachama wa chama fulani cha siasa mbali na kuongea yeye mwenyewe au mavazi? Kutufuata mpaka chumbani au majumbani (ingawaje inaweza kuwa na maana ya 'kwa udi na uvumba'), je katiba inaruhusu hili? Hivi hakuna float political party members? Yaani kama kwenye wateja wa simu za mkononi - mtu mmoja kuwa na lines mbili. Kama ndio, hao 5,000,000 wanaweza kuwapatia kura 2,000,000 kwani kura haipigwi mara mbili!!! Je, hawajahesabu na kadi feki kwenye hao 5,000,000?

Kama yeye analifahamu hilo la ushindi ni kwa mtu mmoja na washindani kawaida ni zaidi ya mmoja, kwa nini chama chake hakikutaka wagombea wengine wa urais ngazi ya chama wachukue fomu? Na hata kutumia mashetani kuwatisha - Sheikh Yahya?
 
teh teh teh........kumekucha ndo unakumbuka shuka???

Mkuu Kazi anayo, Huyu Mtoto anampeleka pabaya babake, ana kichwa kikubwa mno, Mwinyi alpelekwa na mama Sitti, sasa JMK anapelekwa na Ridhwan

mbayaa
 
Mkuu Kazi anayo, Huyu Mtoto anampeleka pabaya babake, ana kichwa kikubwa mno, Mwinyi alpelekwa na mama Sitti, sasa JMK anapelekwa na Ridhwan

mbayaa
Na mkapa je, alipelekwa na nani?
 
Kwa mtu mwenye uwezo wa kufikiri haraka haraka na kwa usahihi kama Dr. Slaa equation ingekuwa hivi: (1+3)*5,000,000=20,000,000. Hiki ndicho alichokuwa akimaanisha bila kufikiria kuwa NEC ina idadi ya wapiga kura 19.67m, sasa hawa 0.33m watatoka wapi. Ni heri angesema 'walau mmoja, wawili au watatu'!! Hivi JK anajua kweli hesabu? Kihesabu amejipa "a word problem" (hesabu za mafumbo) na kushindwa kui-solve! Hivi ndio maana anakimbia mdahalo?! Sasa watanzania mjue kuwa tatizo hili lake ni "just a tip of the iceberg" Kwani hesabu ni logic/ reasoning, hivyo kushindwa kuifanya hesabu nyepesi ni sawa na kushindwa kuona au kutengeneza logic/ ku-reason; sasa mambo makubwa ya nchi anayaweza? Ushahidi tunao hayawezi!!!

Kama yeye analifahamu hilo la ushindi ni kwa mtu mmoja na washindani kawaida ni zaidi ya mmoja, kwa nini chama chake hakikutaka wagombea wengine wa urais ngazi ya chama wachukue fomu? Na hata kutumia mashetani kuwatisha - Sheikh Yahya?

Nimekukubali ingawa hiyo equation umeirahisisha inaweza kuleta mushkeli kidogo,,, ingekuwa wale watu 3*5,000,000 + 1*5,000,000=20,000,000. Ukiweka mabano unapata equation yako.

Hapo ndio uone upunguani wa hawa jamaa,,,, sasa hizo 0.33 zitoke wapi zaidi ya wizi?
 
For how long JK atakuwa anamtetea mtoto wake kwenye the so called uzushi?, why not UVCCM kuita waandishi wa habari kufafanua hilo? What if this young man was caught on tape somewhere pompously claiming to have done wht he's accused of? Hata kama si kweli kwamba yeye alihusika na hayo maamuzi lakini I see Ridhwani not much different from many Tz youths ambao ku-exaggerate mambo ni hulka ya kawaida especially kwenye social talks?

It is therefore high time kwa JK to be a leader, mambo ya mtoto wake ni ya mtoto wake! Let him deal with it. Sidhani kama hayo magazeti kwa namna yeyote ile yamemtaja JK kupewa habari au kuchochewa na Ridhwani kufanya maamuzi juu ya Bashe.

Like father like Son
 
kikwete bana
yaani hajiamini kabisa

mwaka huu analo, na hivi kawachefua wafanya kazi!!!!

mdomo huo
 
Back
Top Bottom