JK: Tanzania kujenga reli ya kisasa ya kimataifa

JK: Tanzania kujenga reli ya kisasa ya kimataifa

jamani hiyo modern railway anayoiongelea kikwete ni kama hii hapa chini, 47?
index.jpg

i wapi?
 
Na zile barabara za juu - flyover kwa mji wa Dar imefikia wapi?

Makubwa haya...Ikiwa mradi wa treni Canada toka Toronto mjini kwenda airport yao umbali wa 30km hivi, wametenga dollar billion tatu, wakati sisi ukarabati wa reli ya zamani tumeshindwa, huo umeme wa kutosheleza tu mkoa wa Dar tunayumba kwa miaka sita na bado tunahesabu kweli hizi ahadi bado mnazipokea?
 
What a coincidence ni jana tu BBC wameonesha uozo wa TAZARA according to the nosey white man it is not fit for purposes, mafuta yanaisha njiani, derailing is not uncommon and delays is part of their pride in services. Misaada inapotea, engine azina spare parts in short ni miujiza on how it is still running and hoh yeah before i forget there are some Chinese bosses who are camera shy.

Jione eni wenye kama kuna mtu ana lisaa lakupoteza.

BBC iPlayer - African Railway
 

Hii ni China mkuu.hizi ni treni mpya ambazo ni fastest in the world kwa sasa,na ambayo ni teknologia ya wachina wenyewe.duniani kwa sasa China inaongoza kwa teknologia ya bullet trains,mpaka sasa hivi wameshapata contract ya kujenga reli kama hizo marekani.na in abt 5 years time,nchi nzima ya china itakuwa na railway network ya hiyo bullet train.kwa sasa the biggest railway station in the world ipo China, kwenye jiji la Guangzhou for these kind of trains.
 
Rais kasema reli inayotumika kwa sasa imeppitwa na wakati kwa hiyo serikali inajiandaa kujenga reli mpya na ya kisasa.
Kukamilika kwa reli hiyo kutaifanya bandari ya dare es salaam kutumika vya kutosha alisema.
Ahadi hiyo itatekelezwa kwa kupitia mkopo wa benki ya maendeleo afrika na nchi tajiri zitatoa misaada mbali mbali.
Mradi hadi kukamilika utatumia dola bilion 5.1 za kimarekani.
Source: ippmedia.com

LINI SASA MZEE?Siku zinaenda yale yalioahidiwa ktk kampeni hata hayajakamilika.labda hizo bajaji sunlg
 
we kamsamba naomba usirudie tena hii kauli yako kabisa katika maisha yako. Sawa?? Unajua maisha ya ulaya yalivyo wewe? Hivi unataarifa kuwa no free lunch in europe? Unajua maana yake? Hivi unajua kuwa watu wanajiua kwa sababu hawana kazi na wanauaga hadi familia zao kwa sababu ya maisha magumu? Na wote hawa wapo ulaya. Usiongee tu kwa sababu fulani kaongea. Sawa?

Hajui alisemalo,lazima atakuwa anamatatizo kwani kwa akili ya kawaida huwezi kuwezi kutamani utu wa mnyama.
 
offcourse bajaji moja wananunua USD 5900. Na watanunua bajaji 400.

:shock::shock: kwa nini wasitumie pesa walizopanga kununua hizo bajaji 400 kununua walau magari kadhaa ya wagonjwa coz hizo bajaji ni miezi tu zitakuwa juu ya mawe. :focus: hiyo reli ya kisasa nadhani itahitaji pia mabehewa ya kisasa sio yale yanayoenda huko mpanda yananepa wakati wote mtu roho ipo juu juu. Kila siku ni kuweka mikakati, lini utafanya hata moja ili tuone?
 
Reli Dar - Kigali kumaliza tatizo la usafirishaji
THURSDAY, 17 MARCH 2011 18:52 NEWSROOM
Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete amefungua mkutano wa wawekezaji wa mradi wa ujenzi wa reli kutoka Dar es Salaam hadi Kigali, Rwanda ambapo amesema hatua hiyo itamaliza tatizo la usafiri na usafirishaji wa njia ya reli nchini. Alisema mpango huo utatekelezwa chini ya miaka minne na kwamba ni mwelekeo wa kumaliza kero ya usafiri katika mikoa inayotegemea reli hiyo kwa usafiri na usafirishaji.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, ujenzi wa reli hiyo utalazimisha serikali kupanua bandari ya Dar es Salaam na kuifanya kuwa ya kisasa na uwezo mkubwa wa kupokea mizigo.

"Hii sasa inaashiria kuwa hata bandari yetu ni lazima tuipanue ili iwe kubwa na ya kisasa itakayoweza kuhudumia mizigo mingi ambayo itaongezeka".

Awali, akifafanua kuhusu ujenzi huo, Waziri wa Uchukuzi Omar Nundu, alisema mkutano huo utapendekeza moja kati ya aina tatu za reli itakayotoka Dar es Salaam kwenda Burundi na Rwanda.

Nundu alizitaja aina zinazoshauriwa katika ujenzi huo kuwa ni kujenga nyingine mpya kwa kuweka tuta tofauti na lililopo sasa, litalogharimu dola za Marekani bilioni tano zaidi ya sh. trilioni 7.5 hadi kukamilika.

Nyingine ni kujenga reli pembeni mwa iliyopo itakayogharimu dola za Marekani bilioni 3.54 (zaidi ya sh. trilioni 4.7), na ya tatu ni kuiimarisha iliyopo kwa kujenga laini mbili pembeni mwake kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 3.61 (zaidi ya sh. trilioni 4.6).

Kwa mujibu wa Nundu, aina hizo zinalenga kuifanya reli hiyo kuwa ya kisasa zaidi na kuwezesha kuruhusu kupita treni za kisasa zenye uwezo mkubwa zaidi.

"Ninachosema ni kwamba tukianza ujenzi, wananchi wategemee katika kipindi kisichozidi miaka minne reli itakuwa ya kisasa kabisa," alisema waziri Nundu.

Waziri huyo alisema mkutano huo wa jukwaa maalumu la wawekezaji wadau wa reli hiyo, utachagua moja ya aina tatu itakayokuwa rahisi katika utekelezaji ili ifanyiwe kazi.

Alisema tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeshatoa fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo.

Miongoni mwa walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Waziri wa Miundombinu wa Rwanda, Vicent Karega, Waziri wa Usafiri wa Burundi, Said Kibeya, mabalozi makatibu wakuu na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.
 
1.Mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi

2.Mradi wa treni ziendazo kwa kasi

3.Mradi wa ndege ziendazo kwa kasi

4. Mradi wa meli ziendazo kwa kasi

5.Mradi wa pikipiki za wagonjwa ziendazo kwa kasi

6. Mradi wa baiskeli ziendazo kwa kasi

7.Mradi wa mafisadi uendeshao nchi kwa kasi kwa lengo la kufilisi nchi
 
Deni la nje ya nchi ni zaidi ya U$ 11bill na hili nitokea 1961 - 2011. Leo unataka kuanzisha mradi wa U$ 5bill karibu nusu ya deni la nje! Hii haiwezekani,aidha rais alikuwa kuifurahisha nafsi yake au amedanganywa na washauri wake.
 
Jk bwana kwa vichekesho,ni serikali yake itakayojenga au?maana yule mtu wa mjini lazima tumuelewe,anaweza kusema nilikua na maana ya serikali ya chadema ikishika madaraka!
 
Rais kasema reli inayotumika kwa sasa imeppitwa na wakati kwa hiyo serikali inajiandaa kujenga reli mpya na ya kisasa.
Kukamilika kwa reli hiyo kutaifanya bandari ya dare es salaam kutumika vya kutosha alisema.
Ahadi hiyo itatekelezwa kwa kupitia mkopo wa benki ya maendeleo afrika na nchi tajiri zitatoa misaada mbali mbali.
Mradi hadi kukamilika utatumia dola bilion 5.1 za kimarekani.
Source: ippmedia.com


Dah!!! Huyu jamaa msanii sana!!! Zile barabara za kupita juu kwa juu Dar (Flyovers) ili kupunguza msongamano wa magari zimeishia wapi!?

Awesome%20Flyovers%20(1).jpg
 
1.Mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi

2.Mradi wa treni ziendazo kwa kasi

3.Mradi wa ndege ziendazo kwa kasi

4. Mradi wa meli ziendazo kwa kasi

5.Mradi wa pikipiki za wagonjwa ziendazo kwa kasi

6. Mradi wa baiskeli ziendazo kwa kasi

7.Mradi wa mafisadi uendeshao nchi kwa kasi kwa lengo la kufilisi nchi

Umesahau mradi mmoja,ule wa uchumi unaopaa wa mheshimiwa lowassa enzi zake pamoja na ule wa kununua mvua!hii serikali kweli ya "wapigaji",toka imeingia madaraka 2005 imekaa kipigaji pigaji tu...hapo wanataka kuwapiga jamaa wa world bank tu hamna lolote,lakini sisi ndio tutawalipa world bank vizazi na vizazi bila kuziona faida za miradi hiyo
 
Sasa huyu bwana atakuwa na ahadi ngapi kwa wadanganyika. Lo!
 
Hao Wachina tunaowategemea wametolewa nishai na ajali katika futuristic trains zao mpaka wanazifikiria upya sasa hivi baada ya ajali za eastern corridor yao.

BBC News - China train crash: Signal design flaw blamed

Hapa naona white elephants and confessions of economic hitmen. When will we learn?

Kama unaweza kupata mkopo huo upeleke kwenye kuipa nchi umeme wa uhakika,

Rais rahisi.
 
Back
Top Bottom