Kaka u can do better than this mediocrity generalization/conclusions)samahani kwa kutumia maneno mazito).
Kuhus MEDIA unajua wazi kuwa sio JK aliyehusika kwa karibu na hili. Ilikuwa ni shughuli ya LOWASSA na ROSTAM kwa manufaa yao wenyewe. Vilevile sio wote waliokuwa wakimremba JK walinunuliwa. Wapo waliokuwa wakiamini wazi kuwa ndiye anayewafaha na hawakuwa wakifanya waliyoyafanya kutokana na kununuliwa kama unavyodai. Lakini kumbuka JK aliuzika sio kwa uwezo wake lakini kwa kuwa mbadala wa "mwarabu" Salim, "Kikongwe" Malecela "aliyelaaniwa na Mwalimu", "FISADI ama ZERO" Sumaye, "Mlevi na rafiki ya MKAPA" Kigoda na propaganda zengine za kweli na zisizo za kweli....
Kuhusu wasomi na hapa nasema tena kuwa si kweli JK alikuwa na uwezo wa kuwanunua wasomi hasa wale wa MLIMANI. Kama ni suala la REDET mimi nimekuwa karibu na shughuli zao na hata ile opinion poll iliyofanyika kabla ya uchaguzi wa 2005. Si kweli zoezi lile halikufanyika kisomi. Hatua zote za kisomi zilifuiatwa na wala zoezi hii halikumhusisha Prof Mkandala pekee ambaye ndiyo amekuwa kinara wa tuhuma kuwa wasomi walikuwa wanatumiwa na JK. Zoezi la kujua maoni ya watanzania lilifuata hatua zote za kisomi. Tatizo ni ukaribu wa JK na Prof Mkandala (na UKADA wake kama walivyo wasomi wengine) wakati ule na hata hivi sasa ambao ulipelekea kujenga taswira ya kumbeba JK....
Kuna wasomi kama Prof CHACHAGE ambaye alikuwa na mategemeo makubwa na JK. Katu huwezi kuniambia kuwa Prof Chachage niliyemjua mimi naye pia alikuwa amenunuliwa na vijisenti vya JK. Wapo walikuwa wakiamini kwa dhati kuwa JK ni mwakilishi wa wanyonge na angekuwa na uwezo mkubwa wa kushughulikia madhila ya wanyonge wenzake. Wapo waliokuwa wakiamini kuwa JK ni mjamaa asilia ambaye angeweza kuirudisha CCM kutoka katika mikono ya Walalakheri na kuwawezesha walalahoi kurudisha sauti yao katika chama hicho. Prof Chachage alikuwa mmoja wa hawa na katu imani yake kwa JK halikuwa eti kwa kuwa alinuliliwa.....Namtumia Prof Chachage kama mfano wa wasomi ambao walimuunga mkono JK kwa dhati kutokana na imani waliyokuwa naye juu yake na sio eti walinunuliwa......wapo wengi wengine..
Tanzanianjema
Mkuu,
Nadhani wewe ndiye u can do better than your mediocrity generalization/conclusions nikilinganisha uliyoyaongea na aliyoongea FMES.
Inaingia kichwani kwa nani kusema waliotumia Magazeti walikuwa ni kina EL na RA kwa faida yao. Mtu ambaye alikuwa ANATARAJIWA kuchukua madaraka makubwa ya NCHI alikosa UWEZO wa kujua kwamba akina EL na RA walikuwa wanamtumia kupitia magazeti kujinufaisha wakati yeye hanufaiki chochote! Walichokuwa wanafanya EL na RA kwa asilimia 100 kilikuwa na baraka za JK! Basi.
Umetaja kuwa kuna watu walikataliwa kwa Uarabu wao, kwa Ukikongwe wao, kwa Uchapombe wao lakini unasahau kuna watu walitajwa kuwa ni 'wagonjwa' au wewe hukusikia au hukutaka kusikia au unajifanya hukusikia?
Hakuna mahali ambapo FMES amesema watu wote waliomuunga mkono JK walinunuliwa lakini TUNAAMINI watu wengi waliomuunga mkono JK walinunuliwa kwa bei taslimu (unapewa chako mapema) na wapo walionunuliwa kwa mkopo (ahadi za kupewa vyeo) au wewe unadhani fedha za EPA zilifukiwa kaburini?
Kwa taarifa yako SISI tunawajua kwa majina wasomi woote walionunuliwa pale UDSM! Kama wewe huwajui nyamaza kwa sababu wewe sio PRO wao! REDET ninayoijua mimi ni MALI ya Prof Mukandala ukubali usikubali. REDET ni Mukandala na Mukandala ni REDET! Hao wengine unaowasema ni vivuli tu! Ni mambo ya kawaida kabisa pale UD watu kujichukulia taasisi na kuzifanya ni za kwao. Anzia ESAURP ya Profesa Teddy Malyamkono, pitia Kijiji cha Sayansi na Teknolojia cha Profesa Shayo, nenda CEST ya Profesa Mwandosya, usisahau kupitia ESRF ya Profesa Wangwe. Pamoja na kwamba JK alikubalika wakati ule wa utafiti wa REDET lakini kuna 'chumvi' nyingi tu iliwekwa kumuongezea umaarufu. Suala la JK na Mukandala ni zaidi ya UKADA kama unavyotaka kudhihirisha. Hapa tunaonglea suala la USWAHIBA wao! NIPE nikupe. Waambie REDET leo waende wakafanye UTAFITI tena na UONE kama watatuletea matokeo SAHIHI! Hawajipendi? Au wako busy na kufanya tafiti za migomo ya wanafunzi wa vyuo, walimu, madaktari kwa sasa?
Umemtaja Profesa Chachage (RIP) kwamba alikuwa na mategemeo makubwa na JK! Hivi ni kweli kwamba akina Chachage na usomi wao uliotukuka, na tafiti zao zote walizofanya ni kweli kwamba waliamini JK PEKEE (BILA CCM yote) ndio mkombozi wa wanyonge? Unataka kuniambia Chachage naye alikuwa ni miongoni mwa watu waliomwona Salimu ni Mwarabu, Malecela ni Kikongwe, Kigoda ni Chapombe na JK ni Chaguo la Mungu? Binafsi ni mmoja wa watu ambao nilikuwa namheshimu sana Marehemu Chachage, lakini nilikuwa mmoja wa watu walioshitushwa na kitendo cha Profesa kuigeukia CCM! Kumbuka Marehemu alianguka hadi kupelekea kifo chake pale Kibaha akiwa anafanya kazi za CCM! Sipendi kusema mengi lakini inawezekana marehemu naye alikuwa na 'mkataba' fulani na CCM! Tumuache apumzike na amani huko aliko alifanya mengi ya maana kuliko yasiyo na maana.
Sio kina Chachage tu waliobadilika ETI kwa kumuona JK ni chaguo la Wanyonge. Bado tunazo kumbukumbu za kina Salva Rweyemamu, akina Jenerali Ulimwengu, akina Prince Bagenda, akina Gideon Shoo walivyoligeuza Gazeti la Rai na kuwa JUKWAA la kummaliza SAS na kumuinua JK! Katika hawa nadhani wapo walionufaika na wapo ambao hawajanufaika hadi leo! Jenerali Ulimwengu aliyekuwa na ushawishi na nguvu kubwa pale habari cooperation ALIKUBALI vipi kuuza 'utu' wa gazeti la RAI? Je na yeye 'alikopwa' na hajalipwa kama alivyolipwa Salva? Au majibu ya swali hilo ndio kuanzishwa RAIA MWEMA! Ni kweli kwamba Habari Cooperation ilikaribia kufilisika ndio ikaamua kutafuta 'mwekezaji' mpya RA? Jenerali alivyo mzoefu wa duru za siasa za Bongo, aliona ni sahihi kabisa kumuuzia RA kampuni yao? Nawasilisha.