Serayamajimbo
Senior Member
- Apr 15, 2009
- 191
- 38
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri kama njia ya kujipanga upya kukabiliana na ufisadi.
Rai hiyo imetolewa juzi na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kwale, Pangani, mkoani Tanga.
Hata hivyo, Mbowe alisema haoni kama Rais Kikwete anaweza kuvunja baraza kwa nia hiyo kwani mafisadi wanaopaswa kushughulikiwa ni watu wake wa karibu, na ndio walifadhili kampeni zake za urais.
Mbowe alisema rais anapaswa kuwa mkali na kuwaondoa serikalini baadhi ya mafisadi ambao wamo katika Baraza la Mawaziri. Hata hivyo, hakuwataja majina mafisadi hao.
Alisema kosa kubwa la Rais Kikwete ni kucheka na mafisadi. Aliwataka Watanzania kukasirika na kuchukua hatua wakati wa uchaguzi mkuu ujao mwakani.
Wakati huohuo, jana chama hicho kimefanikiwa kuzoa wanachama 60 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) jirani na nyumbani kwa Mbunge wa Muheza, Harbert Mtangi.
Wanachama hao walijiunga na CHADEMA muda mfupi baada ya Mbowe kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Misozwe.
Mbowe aliwaeleza wakazi wa Misozwe kuwa hakuna haja ya kumngangania mbunge huyo kwa kipindi cha miaka 10 hadi inafika wakati anajiona kama sultani wa kijiji.
Alisema hakuna haja ya kufunga ndoa na mbunge au chama na kama wanaona mbunge hawafanyii cha maana wana haki ya kuchagua mwingine tena wa kutoka chama makini cha CHADEMA.
Ninyi watu wa Tanga mmefunga ndoa na CCM au mbunge? Mnakaa naye muda wa miaka yote hii na hafanyi mambo ya maendeleo halafu mmemngangania kujiita eti CCM wakereketwa na huku mkiwa na maisha magumu. Acheni kumfanya mbunge kama sultani, alisema Mbowe.
Huku akishangiliwa na wananchi, Mbowe alitoa mfano kuwa kama kijiji kuna duka moja lazima muuza duka ataringa, lakini kama kuna maduka mawili mteja una uwezo wa kuchagua duka na kutoa mfano kuwa CCM ni sawa na duka moja, hivyo wanatakiwa kuongeza CHADEMA liwe duka la pili na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Naye Mbunge wa Viti Maalum, Grace Kiwelu, alieleza kusitikitishwa na kitendo cha Mtangi kuvuta umeme kutoka mjini na kuruka nyumba za wapiga kura wake na kuweka kwenye nyumba yake pekee. Alisema kitendo hicho kinaonyesha ni jinsi gani mbunge huyo asivyowajali wapiga kura wake.