Jk vunja bunge la katiba kwa sasa!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Jk kwa mtazamo wangu binafsi pamoja na hasara kwa taifa iliyokwisha patikana tafadhali vunja bunge hili kwa sababu zifuatazo;
1> Taratibu na kanuni nyingi juu ya uendeshaji wake zilikuwa hazikuandaliwa awali kwani ingepaswa kuteua wabunge wachache kutoka vyama vyote vya siasa ili kuunda kanuni hiza pasi kuingia hasara kubwa namna hii!
2> suala la muungano lapaswa kujadiliwa upya nje ya bunge hili ikibidi liondole katika mijadala ya katiba yetu kwa sasa na litengenezewe kamati maalumu ya kulishughulikia swala hilo tu,pia baadhi ya misingi yake iliyowekwa na waasisi wake iwe ni mwiko kuigusa
3> JK itakuwa ni jambo baya kabisa kabisa muungano wetu kukufia mikononi mwako,japo watz wote twafahamu jambo hili ulilianzisha kwa nia njema,lakini sasa limekuwa jambo la khatari kubwa,Tafadhali japo waswahili wa nasema ukiyavulia nguo maji shurti uyakoge kwa hii HAPANA! JK vunja bunge hili ili kanuni zitengenezwe! VYA KUVICHOKOA TUVICHOKONOE, VYA HAKHARI TUVIWEKE KANDO NA TUSIVITINGISHE WALA KUVIGUSA,IDUMU TANZANIA
 
Kesho ni siku kubwa kwa JK, ni siku ya kupima busara yake, tunasubiri hoja kuliko vihoja.
 
Naungana na jembe busara zitumike raslimali kubwa ya umma inateketea mwisho wa siku hakuna katiba nzuri au haipatikani kabisa tunajua nia nzuri aliyonayo mheshimiwa lakini ubinafsi wa hawa wahishimiwa na uroho walionao hatatupatia katiba mzuri wanatumia sana delay tactcs wazidi kukomba mihela öle wao
 
Naungana na mtoa mada JK busara zako ni muhimu HASA kwa siku ya kesho tuondolee huu uchafu kwani fedha nyingi zinaangamia huku huduma za jamii zikizidi kuzorota! NYOOSHA MKONO SIMAMISHI HI KITU!
 
^^
Kwa mwenendo huu wa sasa, Taifa lilikuwa na haja ya katiba mpya?
^^
 
Naunga mkono hoja yako;

Maandalizi ya awali hayakufanyika kabisa, pengine ni kwa ajili ya ugeni wa hiki kitu
au naweza kusema kuwa wasaidizi wa JK walimtegea bomu.
 
Naunga mkono hoja yako;

Maandalizi ya awali hayakufanyika kabisa, pengine ni kwa ajili ya ugeni wa hiki kitu
au naweza kusema kuwa wasaidizi wa JK walimtegea bomu.

Ccm walidandia treni kwa mbele katiba mpya haikuwa agenda yao.
 
Hapana, liwalo na liwe, au nie ni ccm mnaotaka hili, maji yako shingoni eti?..
 
Kwani muungano ukivunjika tutakufa au ndio mwisho wa maisha yetu,sijui wewe mtu wa kawaida ambaye sio mwanasiasahuo muungano umekusaidia au unakusaidia nini,kama Azimio la Arusha ambalo lilikuwa linazingatiwa utu na usawa wa mwanadamu limezikwa kwanini muungano usivunjike,kama Azimio la Arusha lilivunjwa basi nao muungano uvunjiliwe mbali,sioni sababu za kuwepo muungano na hakuna anayesema,tumebakikuimba wimbo kama kasuka.Narudia tena muungano una faida kwa wanasiasa wachache,kwa tuliobaki hauna kitu chochote cha maana,muungano wa kisiasa umepitwa na wakatini mzigo kwa Tanganyika,haya ni mambo ya kutafutiana vyeo.
 
Mamndenyi washauri wa jk possibly wanataka kumuingiza choo cha kike! Afukuze wote! pia waache kumpa presha mzee wetu WARIOBA amezunguka nchi nzima kusikiliza wananchi ana "data with no exageration"hapa washauri hawakuona kwamba kuna vya kugusa na kuacha?
 
Last edited by a moderator:
Nyie wanazi wa CCM nani kawaambia muungano unakufa kwa kuanzisha mfumo wa serikali 3?Hii inaonyesha jinsi gani ambavyo hamkumuelewa Jaji Warioba au makusudi yenu mnataka kuvuruga mchakato mzima wa katiba?
 
JK ana nafasi kubwa sana ya kurejesha imani kwa wananchi kesho kama atahutubia bila kumshambulia warioba na kusisitiza wajumbe kuzingatia mambo ya kitaifa bila kufuata uvyama wao.
 
Avunje haraka sana bwana warioba na wenzake wamekwenda kinyume sana adidu za rejea za sheria ya mabadiliko ya katiba
 
hapa kwenye katiba kuna mambo ilibidi yafanyike na kufikiwa muafaka ndio kwa pamoja tuketi na kuandika sasa katiba mpya.

hapa kizungumkuti kikubwa kipo kwenye muungano kuna mambo mengi sana yatakuwa ni magnum na vigum kuyajadili ndani ya katiba na kufikiwa muafaka kama suala la muungano litakuwa halijapatiwa muafaka.

natukinifanya vichwa ngum wajumbe watalamba poshoo weeee na mwisho wa siku no solution
 
Binafsi mchakato ulivyokwenda mpaka ulipo sasa umenifurahisha, wametunga kanuni wote kwa pamoja na watazifuata wote.

Tatizo CCM imeshavunja kanuni tayari kwa maslahi yake kwa kumtanguliza Warioba badala ya Jk.

Huu sio wakati zidumu fikra za Mwenyekiti, akienda tofauti anaumbuliwa waziwazi.

hii katiba ni ngumu kwa ccm kwa kulazimisha matakwa yake.!!!
 
HUU NI MTIHANI NYETI KWA JK HAPA WATANZANIA TUTAONA USHUPAVU WA KIONGOZI KWA HOTUBA YAKE TUNAYOITARAJIA KESHO TAKRIBANI MASAA 15 YAMESALIA KABLA JK AJAUSHANGAZA UMMA WA WATANZANIA,BUT PENDEKEZO LA MTOA HOJA NI BUDI LIKAZINGATIWA KWA HASARA ILIYOPATIKANA "YATOSHA"TUWAREJESHEE WANANCHI MREJESHO WA KODI ZAO KWA MAENDELEO,BARABARA NYINGI BADO NI MBOVU,BIDHAA ZA MADUKANI HAZISHIKIKI? TUMKOMBOE KWANZA MTANZANiA KWANI "ANAKUFA"
 

Mkuu tangu kupata uhuru kamati hazina idadi na matoke yakipelekwa wanawekwa kwenye kabati na baadaye kwenye dustbin!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…