JK, wengi hamjamwelewa!

hv wewe loss angeles umefata nini?
 

Nakubaliana nawe 100%.Misaada mingapi tumeshapewa imeishia kuliwa kwa ufisadi, mfano wa karibu ni Ule wa wizara ya maliasili na utalii. If we really want changes and development, then we have to start working inside out...to clean the house first.Lazima tujue nini kinatakiwa kifanyiwe kazi kwanza na kipi kitafuata baadae. Leo hatuoni hayo..tunanunua radar, ndege ya rais, na mambo mengine kadhaa yasiyo na tija kwa watanzania wengi ila watu wachache. Nionanvyo, hakuna sababu ya kuzunguka dunia nzima kuomba misaada bila kujipanga vizuri kujua nini chakufanya na tufanye vipi. Hata kama tutapewa misaada kutoka kila upande, huu wizi na ukosefu wa uadilifu utazitapanya fedha hizo bila kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kama misaada inayoletwa inafanya vitu vinavyoonekana sidhani kama watu watakuwa na maswali mwngi ya kuuliza. Ninachojiuliza kila wakati ni hiki, hivi mbona misaada haileti maendeleo tunayokusudia?Kila kukicha ni kashfa tu na mwendo wa walio wengi kwenye maendeleo ni mdogo kuliko wa kinyonga.Lini Tutafika tunakokuta na misaada so far haijanishawishi bado kama ni njia muafaka ya kufikia hayo maendeleo
 
Wapendwa wana JF, mimi ni mara ya kwanza kuandika katika jamii hii.

Sikupendezwa na maelezo ya Ndugu Ambani Adnani Joseph kwa sababu hayana ukweli wa utafiti wa kina.

Ninachoweza kukiona ni kuwa mpendwa mwenzetu ametoa mawazo yake kama yeye ingawa amejitahidi sana kuonesha kuwa watanzania wote akiwemo yeye tunajadili ujinga, upuuzi, matusi na ukosefu mkubwa wa heshima kwa watu wengine. " Mpendwa Ambani Adnani Joseph kweli umetukosea heshima watanzania wenzako kwa kauli zako"

Nimeona hoja mbalimbali zailizotolewa hapo juu na watanzania wengine. Nakubaliana nazo ila ninaushauri ufuatao kwa ndugu yetu Ambani,

Fanya utafiti na uwe na uhakika ndo useme kwani,
1. Hizo blog za wakenya, waganda, waghana na south africa zina madudu mabaya ya ajabu na hawajadili ya maana kama tunayojadili watanzania. Ninao waganda, wakenya, Wanyarwanda, warundi wengi hapa China na wote wanatusifu sana kwenye blog zetu ukilinganisha na zao.
2. Wanaopinga ziara za kikwete nje ya nchi.... hawana mawazo kama yako. Wanaona kuwa anapiga hatua ya mbele wakati kuna mambo anatakiwa ayaweke sawa hapa nyumbani ndo atafute hao mabilionea. Asimwage hizo bilioni kwenye pipa lenye mashimo. (Elewa mada hapo)
3. Sina takwimu za mtanzania hata mmoja aliyejilipua kwa mabomu akiwa ughaibuni. Tunae mtanzania mmoja tu anayesadikiwa kuwa karibu na mtandao wa osama bin laden. Je, unauhakika kuwa watanzania walioko ndani na nje ni wajinga? Tupe data sahihi?

Nikushauri utuombe radhi.
 
 
Last edited:
Dah..! mkuu PM ilibidi ni log in ili nikushukuru kwa point hiyo hapo juu..! Obama alimuuliza unataka nikusaidie vp ili uweze kufanya lile uliloahidi sijui mkuu alijibu nini?


Mi nafkili ni mpiga soga mzuri na anaongea kile ambacho Watz wanataka kusikia hata kama haamini kwacho!
 
Last edited:

Kwanini kinachothibitisha ubora wa hali ya juu ya mtindio wa tafakuri kisiwe watu wanaojikomba kama wewe?Kila mtu kafika alipofika kivyake.Who knows kwamba nawe si mmoja wa hao unaojaribu kuwakandia (i.e. wazamiaji)?Lakini si vigumu kuelewa kuwa wewe ni mnufaika wa ufisadi,ndio maana umeweka busara kando,na kukurupuka kutetea for the sake ya kusikia sauti yako mwenyewe.

Ujinga,upuuzi na matusi ni pamoja na kuwakosea heshima Watanzania mbalimbali wanaojitahidi kuwahabarisha wenzao kuhusu masuala mbalimbali yanayojiri ndani na nje ya nchi.Hivi Michuzi anaandika matusi,ujinga,upuuzi,etc?Mjengwa je?Haki-Ngowi?Hebu tuchukulie mfano wa blogs hizo tatu,kwa mfano tu,kisha tuthibitishie kauli zako za kilevi kuwa "kinachojadiliwa ni ujinga,upuuzi,matusi,nk".
Pia uzembe wa tafakuri umekufanya ushindwe kutambua kuwa asilimia kubwa ya blogs za Kitanzania zinaandikwa na watanzania walio ndani ya nchi,na nyingi kati ya hizo ni za picha kuliko uchambuzi.


Ulishazaliwa wakati baadhi ya blogs za wakenya zilipokuwa zinaendeleza ukabila kipindi cha vurugu za uchaguzi mkuu uliopita?I doubt if you were,and that suggests kwamba tunaweza kuwa tunapoteza muda kujadiliana na "mtoto mdogo"

Unapolinganisha vitu,ni muhimu uwe na mifano hai.Hicho cha muhimu unachokiona kwenye blogs za Kenya,Uganda,Ghana,etc ambacho hakipo kwenye blogs za Watanzania ni kipi hasa?Mgogoro wa kisiwa cha Migingo?Mapambano dhidi ya LRA na tuhuma dhidi ya M7 kuwa mkewe alimu-infect na kaugonjwa flani?Furaha ya Waghana kuwa nchi ya kwanza Afrika kuahidiwa ziara na Obama?


Mbona hata wewe ambaye "hukujilipua" unakabiliwa na tatizo hilohilo la kutoa hoja zisizo na kichwa wala miguu!Hivi ungekuwa umeelimika ungeweza kusema kitu kama "INTERNET ZA MAWASILIANO ZA KITANZANIA"?Ndio kitu cha aina gani hicho?Did you imply webforums (like JF),weblogs (like Michuzi's,et al) au websites za magazeti kama habarileo.co.tz?Internet za mawasiliano?Does that make any sense?Kwani kuna "internet" zisizo za mawasiliano,au za kujichua instead of mawasiliano?au za mawasiliano ya Kikenya,Kiganda,Kighana?


Kwanini walichaondika "hao" kiwe ujinga na unachoandika wewe kiwe "hekima"?Kwanini unakuwa mjinga kwa kutoheshimu uhuru wa mawazo ya mwenzako?JK mwenyewe amesema kuwa unapoishia uhuru wako ndio unapoanzia wa mwezio.Yaani unajikomba hadi unapingana na unayejipendekeza kwake?


Tatizo lako ni fikra za kisisimizi,yaani ndogo kupita kiasi.Uchumi wa Tanzania haujaathiriwa kwa kukosekana studio za Wamarekani.Zinaweza kuja na zikafisadiwa just like migodi yetu ya madini inavyofisadiwa kila kukicha.
Kazi kubwa ya rais,kwa mujibu wa mjinga kama wewe, ni kuzurura kwa kisingizio cha kuvutia wawekezaji.Sasa umuhimu wa balozi zetu huko nje ni upi?TIC wafanye nini?Trade Centres zetu kwenye baadhi ya balozi zina kazi gani?Bodi ya utalii ifanye nini?

Kazi kubwa ya rais ni kuhakikisha serikali anayoongoza inatekeleza wajibu wake katika kuutumikia umma wa Watanzania.Tuna priorities nyingi mno kuliko hiyo aliyojipachika rafiki yako JK kuwa balozi wa utalii.Na hata kama hilo lingekuwa na umuhimu mkubwa,si ameshakuja hapo US mara kadhaa?Au anafuatilia utekelezaji?
Je siyo kweli kuwa kama itatengezwa sinema moja nchini na kuinufaisha nchi kwa kiasi cha dola milioni 200, basi nchi itakuwa imepata kiasi kikubwa zaidi kuliko kiasi chote kinachoingizwa nchini na Watanzania wote walioko nje?
Angalau hapa umetusaidia kubainisha kuwa wewe ni mweupe kiakili.Hebu tuambia hizo dola milioni 200 zinzvyoweza kuzalishwa na sinema moja!Ni kwenye mauzo (assuming Wachina na mitambo yao ya dvd feki Kariakoo "wameokoka na kuacha piracy"),fundraising au "malipo kwa Tanzania kukubali kuwa studio ya filamu hiyo"?


Sasa kejeli ya nini, ama tunajaribu, kwa mara nyingine, kuthibitisha ujinga wetu kama ambavyo tumezoea kujianika hadharani?
Kuna kejeli mbaya zaidi ya wewe kuwaita watanzania wenzako wajinga paipo uthibitisho wa msingi,and at the same time ukishindwa kutuonyesha kwanini nawe si tu mjinga,bali mjinga zaidi ya hao unaowakosea heshima?Na bora ungeficha ujinga wako badala ya kuuanika hadharani with your full name (pengine ukidhani kuwa ita-catch attention ya JK....FORGET IT.Kuna akina Salva wanaolipwa kwa kazi hiyo,kuna akina Muhingo Rweyemamu,Balile,etc wameshakuwahi.Eti Vision 2010!keep on dreaming,man!)
Isitoshe kama kweli tunaipenda nchi yetu kama ambavyo baadhi wanaandika kwa "uchungu mwingi" kuhusu maendeleo ya Tanzania kwa nini tusirudi nchini kwenda kushirikiana na wenzetu ambao wanahangaika usiku mchana kuiendeleza Tanzania.
Rudi kwanza wewe ambaye si ajabu kuja kwako hapo US ni matokeo ya ufisadi unaojaribu kuulinda,na ni mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania.Kwani mlikuja pamoja na hao unaowataka warudi to an extent uwashupalie warudi nyumbani?
Sisi tuko huko, tukicheza madisco na kunywa pombe, na tukiamka ni kuporomosha matusi kwa watu ambao wanapinda migongo katika kutafuta jinsi ya kuiendeleza Tanzania na ndugu zetu tuliowakimbia.
Tabia yako ya ulevi sio kiwakilishi cha kila mtanzania aliye nje.Na hatuhitaji kujua kuwa ukishakunywa pombe "kwenye disco" unapoamka ni matusi mtindo mmoja!I'd advise you to get in touch with AA.
Mtanzania gani anataka urais wa Marekani,Uingereza au Canada?Najua ulitaka kusema uraia,lakini who knows,pengine ndio ushatoka kwenye disco....hahahaha!
Baadhi yetu hatuko honest. Ni wanafiki tu. Tunapenda kufaidi pande zote tukiongozwa na hadhithi ya chako ni changu, na changu ni changu.
Hiyo honest yako ni ipi?Au kwa vile umeweka jina lako halisi?That's not honesty bali ni mbinu zako zilizopita na wakati kwamba ukiweka jina lako hapo labda kuna fisadi ata-get in touch wakati tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu next year.If you are that honest ungetuambia bayana kuwa nawe si mnufaika wa huku na huko.Si ajabu kuwa jukumu la kukuleta huko US lilikuwa la mzazi wako lakini akafanya usanii na sasa jukumu hilo linabebwa na walipa kodi wa Kitanzania,same people unaowatukana hapa kuwa ni wajinga,wapuuzi na wasio na heshima.
Ambani Adnani Joseph

Mtanzania
– Los Angeles.

Hey,mbona your name sounds like a Kenyan?mdogo wake Boniface Ambani wa Yanga?
 
Last edited:
Nadhani, ni JK ambaye hajielewi, na sio sisi ambao hatumuelwi
 
 
Huyu lazima ni zao la ufisadi na anaishi huko kwa mgongo wa mtandao wa mafisadi, hivi Tanzania kuna soko gani la kununua mafilamu ya kimarekani? hizi tu za kukopi za kariakoo watu zia washinda! eti nini....!? Yaani raisi wetu anatukejeli alafu huyu bwana amuunga mkono! unajiletea laana wewe! Yaani watanzania tunahitaji sana senema ee!?
 

Huwezi kuifanannisha familia ya Obama na wakina Kikwete kwa vigezo vyovyote vile! Obama ni Rais anayejua vipa umbele vya nchi yake na ndio maana hawezi kufanya ziara ya siku tisa nje kwa mara moja. Ukiangalia mkanda wa safari za Kikwete kwa mfano alipokutana na watu wa IBM, utaona body language ya wale jamaa kuwa walikuwa wanamuona juha; kitu ambacho ni aibu si kwake tu bali kwa nchi yetu. Wawekezaji hawawezi kuja kuwekeza nchi ambayo haina amani ya kweli, uhalifu na mauaji yakiwa yamekithiri! Put your house in order first and then the wawekezaji will troop in!
 

1. Huyu mtoto atazaliwa lini?? si baada ya miezi 9? sasa mpaka leo tangu ashike hatamu ni miaka mingapi? labda tusubiri mtoto wa tembo azaliwe.
2.Wawakilishi kazi yao nini? wazir wa mambo ya nje etc
3. Nafiki wewe unazungumzia MATUMAINI na IMANI zaidi face reality...au na wewe KADA?
 


Kiasi cha dola za Marekani milioni 200 zitaingia katika uchumi wa Tanzania kwa sinema moja tu kuchezwa katika Tanzania ambayo inayo mazingira mazuri ya kuchezea sinema.

Ambani Adnani Joseph

Mtanzania
– Los Angeles.

Thanks Vision 2010, naamini wewe siye Ambani Adnani Joseph, ila umem-quote tu, right??

Nachelea kuamini kwambahiyo movie itatuletea 200M USD, nimesoma somewhere kuhusu SlumDog Milionaire star kabaki kwenye slums na vilevile sijui uganda walipata dollar ngapi kwa movie ya Amin, na Mississipi Masala

Naomba kuelimishwa kidogo
 
Vision2010 swali kwako ni , katika siku nane za ziara ya Mhe , msafara wake umetumia kiasi gani cha fedha?
Was the visit worthwhile ? ie what did Tanzania as a country benefit?
Kwa mawazo yangu , ni kama vile alikwenda on holiday na hii imejumisha kutembelea IBM, Cisco , Stanford, etc. Next time labda atakwenda Disney Land!
Ni sawa na mtish akija Dar anapelekwa Mwenge na Mlimani.
 
Bwana Ambani kwa kutuhabarisha kuwa kazi kubwa ya rais ni kutafuta wawekezaji nje anatanabaisha kuwa hana tofauti sana na hao watanzania anaowaponda kuwa wana elimu ndogo!
 
kwanza nashangaa sana ..nimetembelea blog ya [mawasilianoikulu] naona wameipa lead hii story...nijuavyo mimi mtu yeyote anayeenda califonia ..lazima atembelee kwenye studios maarufu kama sony au universal studio...etc....i have beeen there ..na kuna watalii wengi...sana tu..,na hata ni jambo la kawaida sana kukutana na movie stars...pichani anaonekana jk akiwa ameshikana mkono na seagal...nadhani akajitambulisha ,..then akawakaribisha...wakajibu bila shaka!![watatoa jibu gani tena]

ni aibu sana kwa rais nzima wa nchi kwenda kutembea studios kama kina sisi tunapofanya tukiwa califonia...hakuna tofauti ....wengi wetu hata hizo picha na movie stars tulipiga[hawana hiyana unawaomba tu].......come on guys thats is being tooo low.......jk amejishusha sana .....

kuna aliyeongelea ..matokeo ya mkutano wa sullivan ambapo jk alitumia dola milioni 100 kuandaa [pamoja na zilizopigwa ..thats a new story]......hadi leo wale actors na african american in diaspora waliokuja pale ...kukimbia winter marekani ...wametuletea nini!!??
 


yeah aende desney land kutembea akirudi hapa atatudanganya kuwa ....ameahidiwa kujengewa mabembea pale mnazi mmoja na kidongo chekundu grounds.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…