Jk yuko mapumziko Bilila Lodge Serengeti

NOT ENOUGH

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2010
Posts
596
Reaction score
307
Nawapa tu taarifa kwamba Mh Rais yuko Bilila Lodge mapumziko tokea jana.

Tumtakie mapumziko mema Raisi wetu ili arudi akiwa na nguvu mpya ya kulitumikia TAIFA LETU.

Nawakilisha.
 
yupo 'nyumbani kwake' ...kweli amekuwa busy hapa katikati, acha apumzike angalau. Kila la kheri Jk
 
Duh, tough to digest. Nyumbani matatizo kibao, maji yamekatwa, umeme - luku inasoma 0.07, karo hazijalipwa, kale kabinti kadogo kana malaria, ukuta wa jirani umeangukia nyumba...choo kimejaa kinahitaji kuvutwa, kodi ya pango inaishia mwezi huu, mwenye nyumba kaiongeza na anataka ya mwaka halafu baba kaenda mapumziko kutafakari afanyeje kuhusu hii familia yake.
 
Nadhani amekwenda kutafakari namna ya kuitembelea hotel yake huko baada ya kustaafu maana ule mpango wa kujenga barabara ya lami kwa kisingizio cha kuwasaidia wananchi wa Mara umeshindikana! Namshauri aihamishie bagamoyo tu maana akimaliza kipindi chake, ataonekana sana kwenye media akiwa anapelekwa mahakamani kabla ya hukumu ya kutumia vbaya madaraka! Na labda waondoe hukumu ya kifo mapema maana watatoweka kabisa kwenye uso wa dunia!
 
akae huko hata mwezi mzima manake akiwa kazini anajaza pumba tuuu

mimi naona ahueni JK anapokuwa safarini manake vituko vinapungua
 
Baada ya kutoka Sudan kuzini kapitiliza mapumziko, akitoka huko moja kwa moja kwenye pipa New york kuhemea. Mtajiju na giza lenu.


na nyie mnakubali ujinga kama huo?nafikiri kapeleka yule demu kiarabu out
 
hii hotel c ndo ile ambayo ni maarufu sana duniani.

Hapo ni kwamba mkuu
ameenda ku consume his own goods, kwa wale wa uchumi nazani mnaelewa.

1. Mmiliki wa hii hotel amemegewa kipande cha hifadhi ya serengeti na anakimiliki kwa muda wa miaka 99. Wajukuu wetu ndo watakao kuwepo wakati mkataba unaisha

2. Ana falu wake mwenyewe na sasa ana plani kujenga uwanja wake wa ndege wa kimataifa, si kwa faida ya taifa, no ni kwa faida yake.

3. Ana jeshi lake la kulinda hifadhi yake, c maanish kk guard

4. Hii hotel ndo ile ambayo wana wadharau watanzania kupita kiasi, mtakumbuka ni katika hii hotel kamati ya bunge ya mahesabu ya selikari inayo ongozwa na mh cheyo walizuiwa kuingia ndani ya hotel hii kisa mmiliki yuko bise.

5. Ni katika hii hotel na hifadhi yake mtoto mdogo ilikamatwa ameingia kwenye hii hifadhi na kuhukumiwa miaka

6. Ni katika hii hotel na hifadhi yake maaskari wake hufanya msako wa nyumba kwa nyumba kufunua masufuria jikoni ili kutafuta walio pika nyama ya polini

so mkuu hapo ameenda kujiongezea mapato tu ananunua bidhaa anazo zalisha mwenyewe
 
Mwacheni JK apumzike huku akitafakari jinsi ya kuiokoa nchi na janga la Umeme. Apumzike ili atupatie wakuu wa mikoa watakao tupatia utumishi uliotukuka. Apumzike ili atupatie baraza la mawaziri bora kwani waliopo sasa naona kama wanamhujumu. JK pumzika huku ukitafakari.
 
Nawapa tu taarifa kwamba Mh Rais yuko Bilila Lodge mapumziko tokea jana.

Tumtakie mapumziko mema Raisi wetu ili arudi akiwa na nguvu mpya ya kulitumikia TAIFA LETU.

Nawakilisha.

arudi na nguvu mpya yakupanda ndege.
 
tabu zaidi ni pale tutakapoendelea kuchagua viongozi lege lege.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…