informer 06
Senior Member
- May 11, 2024
- 184
- 170
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imetia saini makubaliano ya ushirikiano na Chama cha Madaktari wa Moyo nchini Misri kwa lengo la kuanzisha huduma za upimaji na matibabu ya magonjwa ya shambulio la moyo kwa wanamichezo, ili kupunguza vifo vya ghafla vinavyotokea michezoni.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini , Agosti 22, 2025, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk. Peter ******* alisema huduma hizo zitakuwa za kwanza kutolewa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, jambo linalotarajiwa kusaidia kudhibiti vifo vya wanamichezo kutokana na matatizo ya moyo.
“Tumeanza kushirikiana na timu za Simba na Yanga, na sasa tunaelekea Azam. Baadaye tutaunganisha timu zote za Ligi Kuu, vyama vya riadha, vituo vya mazoezi na hata wananchi kwa ujumla ili kuwaelimisha umuhimu wa vipimo vya moyo kabla ya kuanza mazoezi,” alisema Dk. *******.
Ameongeza kuwa makubaliano hayo yamewezekana kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika vifaa tiba vya kisasa.
Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Madaktari wa Moyo nchini Misri, Prof. Ahmed Eissa, alisema nchi yake ina uzoefu mkubwa wa kuhudumia wanamichezo na itaendelea kuijengea uwezo JKCI kwa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Tanzania.
“Tunataka kuona huduma hizi zikimfikia kila mwanamichezo, ili kupunguza vifo vinavyotokana na matatizo ya moyo,” alisema Prof. Eissa.
Naye Mratibu wa mpango huo wa JKCI, Dk. Eva Wakuganda, alisema takribani watu milioni 300 katika Afrika Mashariki na Kati watanufaika na huduma hiyo.
“Tutashuka hadi ngazi ya shule kuelimisha namna ya kusaidia wanamichezo wanapopatwa na matatizo ya moyo wakiwa michezoni,” alisisitiza Dk. Wakuganda.
Hafla ya utiaji saini imefanyika wakati ambao JKCI ipo kwenye kipindi cha maadhimisho ya miaka tokea ilipoanzishwa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Mkuu wa Ubalozi wa Misri nchini, Mhe. Amr Selim, ambaye katika hotuba yake fupi aliipongeza taasisi hiyo kwa hatua za mafanikio na kuahidi kuwa Misri itaendelea kutoa ushirikiano zaidi.