JKT waanza na shule za wanyonge

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,011
Reaction score
2,185
Ni hali ya kusikitisha kuona kwamba mkuu wa JKT leo katoa orodha ya shule chache ambazo wahitimu wao wa kidato cha 6, mwaka huu 2013 watajiunga na JKT kwa mujibu wa sheria. Mtindo huu umenipa picha kwamba, wakubwa wa nchi hii hawapendi watoto wao wajiunge na jeshi hilo.

Hii ni kwa sababu shule zilizotajwa kuanza kujiunga na jeshi hilo, zote ni za serikali. Nahisi ni njama za makusudi kabisa kwa kufahamu fika kwamba watoto wao hawako ktk shule za serikali. Hakuna Baobab, Feza, wala St. fulani ktk lisit hiyo.

Msimamo wangu kuhusu jeshi hilo ni kwamba halifai kabisa kukusanya vijana wakati huu wa HIV/AIDS. Ni kwa uzoefu wangu kuhusu mikusanyiko kama hiyo na hali ya askari wenyewe ambao ni waathilika wakubwa ktk nchi hii. Natabiri vibaya kabisa kwa vijana hao na hasa wa kike kwamba watakuwa waathilika wakubwa wa jeshi hili. Mtindo wa kukusanya vijana umepitwa na wakati.

Kama kweli wanaamini jeshi linajenga tabia waanze na akina Adam Malima ambao walikwepa makusudi kwa kupelekwa USA na Hussen Mwinyi aliyekimbiziwa UK.
 
Mpaka leo bado sijaelewa hasa nini lengo la kupeleka vijana JKT, kwa sababu wale ambao walikwenda huko miaka ya nyuma ambao wengi wao ndio viongozi wetu sasa wameshindwa kunishawishi kwa vitendo faida ya mpango huo.
Wengi wao ndo hawa waliopoteza uzalendo kwa taifa lao,wabinafsi na mafisadi; wengine hata kuonesha ujasiri wa kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa wanashindwa!
Ebu nisaidieni wadau.
 


Kwanza kabisa; HAUJUI KUWA WATOTO wa WAKUBWA wa NCHI hii Wanasoma NJE ya NCHI? Sio kama ENZI za NYERERE na KIDOGO wakati wa MWINYI... Kila Mtanganyika na Mzanzibari walikuwa wanasoma SHULE za SERIKALI au PRIVATE zinazofata MWELEKO wa SERIKALI...

Sasa hivi SHULE NYINGI zina MIHULA either BRITISH ED SYSTEM; AMERICAN ED SYSTEM na ya KITANZANIA

Watoto wa Wakubwa woote either Wanasoma MALAWI - Watoto wa KIKWETE au SOUTH AFRICA - Watoto wa LAU MASHA... hiyo ni mifano miwili wapo WENGI zaidi... Na Hawahudhurii VYUO VIKUU vya BONGO.

** AZIMIO la ZANZIBAR ndilo lilowanusuru watoto wote wa WAKUBWA ambao walikwepa JKT
- Watoto wa MWINYI
- Watoto wa MALIMA
- Watoto wa MSUYA

Ma wengi Wengine... na HAO wote wamepauta UWAZIRI au WALIKUWA MAWAZIRI

Na PIA sasa hivi; HIYO JKT Wanawake Watakuwa WANAKWENDA? Sababu siku hizi Wasichana wa Kitanganyika wanaofuata DINI ya KIISLAMU wanavaa tofauti na strictly religious...

SASA watabaguliwa na kutohudhuria? au KWELI watalazimishwa kutovaa NGUO zao ZA KIDINI???

** CCM ni WAGONJWA wameondoa JKT SYSTEM iliyokuwa BORA kwetu sisi WATANGANYIKA lakini Sasa ni SHIDA
itakuwa VERY BIASED!!!!
 
jkt ni aina nyingine ya upotezaji muda usio na tija.tabia za kkikomunistoi zilizopitwa na wakati kabisa.tuondoleeeni upuuzi huu tafadhali.
 


1. Ni kuondoa MATABAKA kwa VIJANA wa KITANGANYIKA kwa WALIO NACHO na WASIO NACHO; Woote Wanahudhuria HAYO MAFUNZO wanalala pamoja; Wanakula chakula Pamoja na INAJENGA MUUNGANO wa Wananchi

2. ILISAIDIA VIJANA kuwa IMARA na AJIRA zilikuwepo sababu lazima Uende JKT kama unataka kupata kazi SERIKALINI na PIA kwenye MAKAMPUNI BINAFSI...

3. Lazima UENDE JKT kama UNATAKA kuwa MBUNGE au WAZIRI

4. KILA MTU aliyemaliza JKT anakuwa amefundishwa MAZINGIRA MBALIMBALI...Ilikuwa inajenga UMOJA wa WATANZANIA...
 
 
acha watoto wa maskini wajifunze sharp shooting!ukombozi unakaribia
 
 

Haya unayoyaandika lazima uyaite ni hadithi.
Hebu angalia viongozi wote wa taifa hili kwa leo. Anza na Kikwete, Bilal, Shein, Pinda nenda kwa spika Makinda, Ndugai, rudi kwa mafisadi akina Chenge na Lowasa na akina sita au sumayi, nk. ktk wote hao nani hakupita JKT? Kama wote walipita JKT kwa nini leo hii wana akili ya kipuuzi kiasi hicho? Kama JKT inajenga, kwa nini leo hii waonyeshe uzembe wa kiasi hicho?

JKT ni upuuzi. Iondolewe. Kama wameshindwa kuwaunganisha na JWTZ basi wawafute kazi. Huu siyo wakati wa kupeleka watu mashambani kulima na kukata kuni na kuzini hovyohovyo. Kule JKT kwenyewe hakuna aliye na maono hata mmoja. Wote wanawaza wapate watoto wa kike ili wakazini nao, basi!

Kma tungekuwa na Rais ktk nchi hii, huenda wahitimu wa form6 wangetusaidia kufundisha shule za kata kwa mwaka mzima kama ilivyokuiwa zamani (Musoma resolution) badala ya kuwapeleka JKT kufanya mambo ya kipuuzi bila faida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…