MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,011
- 2,185
Ni hali ya kusikitisha kuona kwamba mkuu wa JKT leo katoa orodha ya shule chache ambazo wahitimu wao wa kidato cha 6, mwaka huu 2013 watajiunga na JKT kwa mujibu wa sheria. Mtindo huu umenipa picha kwamba, wakubwa wa nchi hii hawapendi watoto wao wajiunge na jeshi hilo.
Hii ni kwa sababu shule zilizotajwa kuanza kujiunga na jeshi hilo, zote ni za serikali. Nahisi ni njama za makusudi kabisa kwa kufahamu fika kwamba watoto wao hawako ktk shule za serikali. Hakuna Baobab, Feza, wala St. fulani ktk lisit hiyo.
Msimamo wangu kuhusu jeshi hilo ni kwamba halifai kabisa kukusanya vijana wakati huu wa HIV/AIDS. Ni kwa uzoefu wangu kuhusu mikusanyiko kama hiyo na hali ya askari wenyewe ambao ni waathilika wakubwa ktk nchi hii. Natabiri vibaya kabisa kwa vijana hao na hasa wa kike kwamba watakuwa waathilika wakubwa wa jeshi hili. Mtindo wa kukusanya vijana umepitwa na wakati.
Kama kweli wanaamini jeshi linajenga tabia waanze na akina Adam Malima ambao walikwepa makusudi kwa kupelekwa USA na Hussen Mwinyi aliyekimbiziwa UK.