JKT waliojenga Ikulu ya Chamwino na kudai kutelekezwa, wamekutana na Waziri Dkt. Rhimo Nyansaho

JKT waliojenga Ikulu ya Chamwino na kudai kutelekezwa, wamekutana na Waziri Dkt. Rhimo Nyansaho

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Dkt. Rhimo Nyansaho amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) walioshiriki katika ujenzi wa kihistoria wa Ikulu -Chamwino, Jijini Dodoma.

Pia soma ~ Malalamiko kuhusu ajira za Vijana 436 walioahidiwa ajira baada ya kujenga Ikulu ya Chamwino

Mazungumzo hayo yaliyofanyika Septemba 01.2026, yamelenga kuwasikiliza vijana hao, kuwapongeza na kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa katika kutekeleza ujenzi wa Ikulu -Chamwino, ambayo ni moja kati ya alama muhimu za Taifa na Ofisi ya juu katika mfumo wa utawala na uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Screenshot 2026-09-16 192606.png
Akizungumza na vijana hao, Waziri Dkt. Nyansaho amesema serikali inayoongozwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua na kuthamini mchango, uzalendo na kujituma kwa vijana hao katika utekelezaji wa mradi huo wa kihistoria

Aidha, amesema serikali inatambua uvumilivu, nidhamu na kujitolea kwa vijana hao, na kwamba kukutana nao huko, ni sehemu ya kuwapa shukrani na pongezi kwa mchango wao kwa Taifa

Kwa upande wao, wawakilishi wa vijana wa JKT walioshiriki katika ujenzi wa Ikulu -Chamwino, wamemshukuru Waziri Dkt. Nyansaho kwa uamuzi wa kukutana nao na kusikiliza maoni yao, wamesema hatua hiyo imewapa faraja na kuonesha namna serikali inavyotambua na kuthamini mchango wao katika ujenzi wa Taifa

Pia, wamemuahidi Waziri huyo na serikali kwa ujumla wake kuwa wataendelea kudumisha uzalendo, uadilifu, nidhamu na kujitolea katika kulitumikia Taifa kwa nguvu zao zote, kama walivyofanya katika utekelezaji wa jukumu la ujenzi wa Ikulu -Chamwino,

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambayo imewekwa kwenye mitandao yake ya kijamii leo, Jumatano Septemba 02.2026 imebainisha kuwa mazungumzo hayo yamelenga kuweka mikakati ya kuendelea kuboresha ustawi wa vijana waliopita mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)...
 
Back
Top Bottom