rehanishabani
JF-Expert Member
- Aug 28, 2013
- 319
- 59
Kama hao vijana hawakwenda kuripoti mimi nawaunga mkono.huenda wamekua na wasiwasi na usalama wao.unaweza ukaenda jkt kwa tamaa ya kumaliza uwahi chuo badala yake ukarudi maiti.hata kama umekufa kwa kusulubiwa jkt watasema ni malaria kuficha ukatili wao kwa vijana wa f6 mujibu wa sheria.mimi siandikii mate mtoto wangu mwenyewe halima kitangilwa alikufa kwa kusulubiwa huku anaumwa.mimi wakanidanganya kusingizia malaria ndio maana hawakumfanyia post mortem kwani ingewaumbua.kifo sio cha halima tu.iko siku wazazi wengine wenye watoto waliokufa watafunguka.na pia vijana waliokua na halima na kurudi salama wanajua ukweli wote wa kifo cha halima na wale waliopoteza fahamu na kukimbizwa hospital ya jeshi ya mirambo wakati halima akiwa ameshakufa.kwa sasa vijana hawa ni waoga kuzungumza ukweli lkn bada ya muda na wao watafunguka.kwa kumalizia nasema wale ambao hawataenda jkt wana bahati.mimi ningejua kwamba nampeleka halima jkt nisingekubali aende hata kwa mtutu wa kifaru.majibu ya chuo yametoka halima amechaguliwa ardhi university lakini ni marehemu.huo ndio uzalendo unaohubiriwa.