Joakim Minde (Laitolya Tours)- ATT: Waziri wa Ardhi

Joakim Minde (Laitolya Tours)- ATT: Waziri wa Ardhi

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Posts
3,335
Reaction score
6,186
Ndugu Mh. Waziri,

Mtajwa hapo juu alifariki siku ya tarehe Saba July 2020 na anatakiwa kuzikwa siku ya kesho.

Nalotaka kuketa kwako ni kesi inayohusu huyu marehemu na chama Cha Ushirika Cha Uru Cooperative kinachomiliki shamba la maize na Kifumbu Estate.

Huyo Bwana aliingia mkataba na chama hicho Cha kukodi eneo lenye ekari 15 badala yake anasema ameuziwa eneo Hilo hivyo kupelekea mgogoro ambao bado upo mahakamani.

Baada ya kufariki familia imetaka kwenda kumzika huyo bwana kwenye eneo ambalo kimsingi bado Lina mgogoro mahakamani.

Naambiwa hata wewe mheshimiwa waziri unautambua mgogoro huo, Mh. Kassimu Majaliwa anaufahamu na viongozi wakuu waliopita Mh. JK na hata Benjamin Mkapa wanamfahamu.

Chama hicho Cha msingi kiliweka zuio la kimahama kwamba marehemu asizikwe kwenye shamba Hilo ambalo kimsingi bado Lina mgogoro na kupewa zuio Hilo. Lakini chaa ajabu naambiwa Baraza la Ardhi limeiruhusu familia kumzika huyo Bwana kwenye eneo Hilo hapo kesho.

Swali nalojiuliza , je Baraza linamaamuzi kuliko mahakama?

Marehemu alikuwa akiishi nyumbani kwake eneo la Kisawio juu kidogo tu kutoka Rau ambapo ni km chache kutoka kwenye shamba Hilo lenye mgogoro, je kwa nini wanakimbilia kumzika eneo lenye mgogoro?

Kwa mamlaka uliyonayo unaweza kuzuia maziishi hayo yasifanyike kesho kwenye eneo Hilo mpaka kesi ya msingi itakapoamuliwa.

Vinginevyo waamriwe kumzika sehemu ingine kwani sehemu zingine za kumzika zipo.

Maswali ambayo wateja wangu wamekuwa wakijiukuza Nani anaweza kutengua maamuzi ya mahakama pasipo kupitia utaratibu wa kimahakama?

IMG-20200714-WA0010.jpg
 
acheni marehemu apumzishwe kwa amani japo mzee minde alikuwa mtata sana enzi za uhai wake; pole familia ya marehemu sara na watoto wake
 
Azikwe Makaburini wanakozikwa wengine, kilichobaki hapo ni yeye na mwenyezi Mungu muumba mbingu na ardhi wengine tukafanye kazi na ikiwezekana msiweke alama yeyote wala kujengea aoze abaki mifupi ardhi ibaki na mbolea yenye rutuba watu walime miaka 200 ijayo...
 
Yaani kamgogoro ka heka 15 tu ndo hd jk na mkapa wanaujua!!!mmh!!!
 
Back
Top Bottom