Joash Onyango abwaga manyanga Simba adai kuna ubabaishaji mwingi

Joash Onyango abwaga manyanga Simba adai kuna ubabaishaji mwingi

Dah! Wakati anasajiliwa huyu mwamba, mashabiki lialia walimpamba kweli kweli. Yaani kama ilivyokuwa tu kwa akina Okwah, Okrah, Mlete Mzungu, nk.
Wewe mbwiga unawashwa sana na mambo ya Simba njoo uolewe huku kabisa
 
Dah! Wakati anasajiliwa huyu mwamba, mashabiki lialia walimpamba kweli kweli. Yaani kama ilivyokuwa tu kwa akina Okwah, Okrah, Mlete Mzungu, nk.

Ila huyu jamaa bado ni mtu sana! Kama kaona fursa sehemu nyingine namtakia kila la heri ila mimi shabiki wa simba jamaa namkubali mno yani sana, pale nyuma akikaa na inonga, kapombe,tshabalala, ni habari nyingine
 
Ni kweli Simba Kuna ubabaishaji mwingi sielewi Ally Salim aliwezaje kupewa nafasi mbele ya Kakolanya matokeo tukatolewa michuano ya Azam na pia kujiondoa kwenye mbio za ubingwa mapema.
Lakini Onyango kiwango chake kimepungua sana na amekuwa akifanya makosa ya kujirudiarudia kwa kutofanya maamuzi sahihi kwa wakati na kufanya makosa mengi yaliyosababisha penati kwenye michuano muhimu.

Inabidi Simba waachane naye kwa amani na wachezaji wengine kama Bocco na Mkude wajitathimini kama wanastahili kuendeleza kuchezea Simba
La Kakolanya aulizwe Try Again na 10% yake.
 
Beki kisiki wa Simba bwana Joash Onyango ametangaza kuachana na timu hiyo na sasa yuko huru kutafuta marisho mapya, huku akisema Simba kuna ubabaishaji mwingi.

-----

UONGOZI wa Simba umefikia makubaliano mazuri ya kuvunja mkataba na beki wake wa kati, Joash Onyango ambaye raia wa nchini Kenya.

Mkenya huyo hivi karibuni ilielezwa kuuandikia uongozi wa timu hiyo barua ya kuomba kuondoka baada kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Huyo ni mchezaji wa tatu hadi hivi sasa ndani ya Simba kuomba kuvunja mkataba wake mwingine ni Mghana, Augustine Okrah na Mohammed Ouattara huku Ismael Sawadogo akiwa katika hatua za mwisho za kuvunja.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimesema kuwa Onyango na uongozi huo wamefanya mazungumzo ya kuuvunja mkataba wa mwaka mmoja wa beki huyo ambayo yamekamilika kwa asilimia mia moja.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa beki huyo tayari ana ofa nzuri klabu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo hivi karibuni iliwasilisha ofa ya kumuhitaji beki huyo kabla ya msimu kumalizika.

“Mazungumzo ya Onyango na uongozi wa Simba juu ya kuvunja mkataba wake yamekamilika, na hivi sasa yupo huru kwenda kuichezea klabu yoyote atakayohitaji kuichezea.

“Pande zote mbili kwa maana ya uongozi na mchezaji mwenyewe mazungumzo yalikwenda vizuri na kufikia muafaka mzuri wa kuuvunja mkataba huo wna mwaka mmoja,” kilisema chanzo hicho.
Kwani si tulishakubaliana mchezaji ukitaka kuondoka anaingiza pesa kwenye account ya klabu na kusepa?

Inakuwaje tena onyango anakaa mezani na uongozi wa Simba?
 
Dah! Wakati anasajiliwa huyu mwamba, mashabiki lialia walimpamba kweli kweli. Yaani kama ilivyokuwa tu kwa akina Okwah, Okrah, Mlete Mzungu, nk.
Kawaida tu mkuu kwa hivi vilabu vyetu vya kariakoo . Siyo Simba wala Yanga , Wote ni walewale. Nikikumbuka usajili wa KINDOKI, YIPE , SURPONG , SIBOMANA , BALINYA , URIKOBU , MOLINGA , ulivyokuwa na tambo hadi huwa ninachoka.
 
Enzi hizo unakuta Sarpong yuko yeye na golikipa tu! Basi utamsikia mtangazaji Baraka Mpenja "🗣️Sarpoooong!!! Kakosaaa!!!.

Dah! Kitambo sana.
 
Unaweza ukajiuliza tu kwa kiwango alichoonyesha hivi karibuni kuna haja ya kuendelea naye kama beki tegemeo? Jibu ni hapana.

aende zake aache lawama imetosha kadiri alivyofanya.
Wapi ametoa lawama?.alikua bado na mkataba na kaomba kuondoka.Mengine kasema ukweli kwasababu sisi hatuyajui zaid yakuwaona uwanjani.Hizi timu ukiwa nje huwez kujua yaliyoko ndani.
 
Ni kweli Simba Kuna ubabaishaji mwingi sielewi Ally Salim aliwezaje kupewa nafasi mbele ya Kakolanya matokeo tukatolewa michuano ya Azam na pia kujiondoa kwenye mbio za ubingwa mapema.
Lakini Onyango kiwango chake kimepungua sana na amekuwa akifanya makosa ya kujirudiarudia kwa kutofanya maamuzi sahihi kwa wakati na kufanya makosa mengi yaliyosababisha penati kwenye michuano muhimu.

Inabidi Simba waachane naye kwa amani na wachezaji wengine kama Bocco na Mkude wajitathimini kama wanastahili kuendeleza kuchezea Simba
Bocco, Mkude, Nyoni wakiondoka hapo ni mwaka tu wanaanza uza madafu
 
Back
Top Bottom