My Take
Chadema mpo? Kuna ujumbe wenu Kwa Ndugai.
===
Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai amesema Jimbo hilo kupata ushindi wa 'Cleen Sheet' kila chaguzi zinazofanyika ikiwemo 2020 ni sababu ya eneo hilo kuwa kitovu na ngome ya demokrasia kwa CCM katika mkoa huo.
Ndugai ambaye ni Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, ameeleza hayo kwa kujinasibisha na ushindi wa kishindo walioupata katika uchaguzi Mkuu wa 2020 huku akisema walifanya vizuri ikilinganisha na majimbo mengine ndani ya mkoa huo.
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika Kongwa, Mgeni rasmi akiwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Bara Stephen Wasira aliyekuwa anapita kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho
"Kongwa ni nguzo na tegemeo kubwa la mkoa wa Dodoma, sisi huwa hapa tunashinda kwa 'Cleen Sheet' wajumbe wote wa serikali za Vijiji, Vitongoji vyote, wenyeviti wote, Madiwani wote Mbunge ndiyo usipime," amesema Ndugai huku akishangiliwa na makada wa chama hicho waliokuwa wakisema mitano tena.
Kulingana na Ndugui aliyekuwa akishangiliwa na makada wa CCM muda wote wakati anaongea amedai kutokana na morali waliyonayo kikubwa wanasubiri uchaguzi wa Oktoba 2025
Source: Nipashe