PreGE2025 Job Ndugai : CCM Itapata Ushindi wa Clean Sheet uchaguzi 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
ndugu Job Yustino Ndugai ameongea ukweli juu ya jambo la msingi sana na kwa wakati muafaka 🔥
 
Ndugai anapoongea jambo, ni mhimu sana kumsoma kwa makini

Ndani ya mtima wake utakuta akijisemea, tumpake mafuta alainke

Mama akubali tume huru ili anyonyolewe vizuri

Tangu lini Ndugai akafurahishwa na madeni hayo lukuki?

Tangu lini Ndugai akafurahishwa na pesa hizo kupelekwa kwa wingi wake Zanzibar

Ndugai ataendelea kuwa ndugai
 
huyu ndiye yule ndugai aliyesema NCHI INAPIGWA MNADA mpaka akatumbuliwa kwa kutetea rasilimali za taifa letu zisipigwe mnada na nchi isikope kope kope hovyo kiasi kupelekea deni la taifa kuongezeka kwa kasi??
au huyu ni mwingine??

naamini CHAWA WOTE ni watu wenye AKILI ZAO TIMAMU TU ila WANAJITOA UFAHAMU wanajitoa AKILI,wanajizima data kwa ajili ya matumbo yao.
 

Attachments

  • images - 2025-03-30T152501.267.jpeg
    10 KB · Views: 19
Nimekoma mimi nimekoma mimi nimekoma sana
 
Sio spika mstaafu, alifukuzwa! Halafu huyu andunje ni hovyo sana, kongwa Haina hata maji, wanakunywa na punda!
 
Hawa wazee ni wa hovyo sana kuliko hata Chawa wao.
 
Your browser is not able to display this video.

Kwa mtindo huu hata mimi ndio ningekuwa CCM clean sheet lazima.

Rais anayeshiriki uchaguzi ana nguvu hizi hapa:-

Polisi amewatia kwapani.

Usalama wa taifa umegeuka usalama wa CCM.

Jeshi limegeuka tawi la akiba la CCM.

Wakurugenzi na watumishi wa tume wamewekwa kwenye mkoba.

Teuzi 99% katika nchi ziko kwa rais, mihimili ya mahakama na bunge iwemekwa kwapani mwa rais.

Matokeo ya urais hayapingwi mahakama yoyote ile [maana yake hata kama rais akishindwa mnaweza kuiba muwezavyo ili ashinde na msifanywe kitu]

Kwa mtindo huo unaachaje kushinda uchaguzi?

Yani referee achezeshe mechi katika timu ambayo ana hisa zake na ni mjumbe wa bodi halafu asivutie kamba kwake?

Maneno magumu katika kamusi ya CCM kwa miaka 48 sasa ni KATIBA & TUME HURU YA UCHAGUZI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…