Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Job Ndugai: Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Sasa arudi bungeni ili ashambuliwe tena? Kama mtu anadai gari lilimfuatilia tangu bungeni mpaka nyumbani kwake na bado hiyo gari haijajulikana ,hapo bungeni ni mahali salama kwake kama akirudi?
 
Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Swali toka kwa Mwanahabari Huru: Je -Waliompiga Lissu risasi wameshapatikaka?

-CCTV ulishawai kuhoji nani amezitoa?

-Lissu alipigwa risasi akiwa Jimboni au kazini Hapo Dodoma?

Ukiwa kiongozi Ushabiki ni mbaya
Waliompiga Lisu anawajua dereva ambae amefichwa na mwenyekiti wa chama kwa hofu ya kuwataja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari
Embu labda tupate msaada wa Anapomzunguumzia daktari amabe anatakiwa kumpa taarifa Spika anamzunguzmzia dokta yupi wa hosptal gan ambayo Kama Bunge lina mawasiliano nao?
Tunamzunguzmia daktari ambae ili amtibu mtu mgonjwa wako inabd alipwe na akimshamtibu alete mrejesho kwa mgonjwa na anamehudumia Mgonjwa so sjajua kama Bunge limemlipa daktar yupi ili kupata hayo majibu ya Mgonjwa Lissu.
Mwenye majibu naomba..............
 
Sio mshahara tu hata Ubunge wake Mh Ndugai akakikaimu pia. Hivi roho zinawauma hivyo hizo hela mnazitoa mifukoni mwenu?? Ndugai hizo hela ukizizuia utaongezewa kwenye mshahara wako??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia aliandaliwa risala, sijui alipelekewa? Au ilihifadhiwa kwenye Hansard.
Akishamaliza kipimo chake cha kumbukumbu na uvumilivu wa kusafiri na kukaa bila ya kutegemea msaada wa vifaa, ataruhusiwa kurudi.
Risala imehifadhiwa..unajua lissu hana muda mrefu wa kuishi ee..taarifa za kitaalam kutoka ubelgiji zinasema hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ule ugonjwa wake unamsumbua
Ipo haja ya kusimamisha mshahara wa Tundu Lissu kwa sababu hayupo jimboni, Bungeni na hospitalini na sijapewa taarifa ya Daktari

Swali toka kwa Mwanahabari Huru: Je -Waliompiga Lissu risasi wameshapatikaka?

-CCTV ulishawai kuhoji nani amezitoa?

-Lissu alipigwa risasi akiwa Jimboni au kazini Hapo Dodoma?

Ukiwa kiongozi Ushabiki ni mbaya

=====================

Spika wa Bunge Bw.Job Ndugai amesema atasimamisha Mshahara na Malipo yote ya Mbunge wa Singida Mashariki Mhe.Tundu Lisu kuanzia mwezi huu kutokana ana Ofisi yake kutokuwa na Taarifa sahihi ya mahali alipo kwasasa na anachokifanya huko. Hii ina maana Lissu hatalipwa mshahara tena kuanzia sasa hadi pale Spika atakapojisikia.

#MyTake:
Hawa ndio wale Balozi Masilingi alisena wameumizwa sana na shambulio la Lissu. Yani waliumizwa sana lakini hawajahangaika kujua aliyeng'oa camera za CCTV. Waliumizwa sana wakaondoa ulinzi siku ya shamvulio la Lissu. Wakaumizwa sana lakini wakamnyima hela za matibabu ili afe, lakini Mungu akamuokoa kwa neema. Sasa wameumizwa sana wameamua kumsimamishia mshahara. Hivi bado tunahangaika kutafuta waliomshambulia Lissu kwa risasi?

In God we Trust
 
Wasitishe wataona nguvu ya umma jamaa hatakufa njaa wanaweza kumchangia vile vile milioni kumi na tatu siyo kitu $5600 hiyo anaweza kupewa kama allowance hata na wapinzani wa serikali ndani ya CCM endelee kupiga kelele akiwa huko nje ya nchi...kuna mambo yanaleta aibu sana yanayofanya na bwana Job...kukaa kimya kuna kuna nafuu, unless otherwise kama nao wanachokoza hoja hii saga iendelee na hatimaye wahusika watiwe mbaroni
 
Mkuu mbona huyu bwana anaogopwa sana....si waamke siku moja wafute kila kitu yaishe!!!! maana kila siku hakuna habari zaidi yake............
Na hapo ndio wanapompa kiki.Hizi kauli uchwara zinambeba sana Lisu, wao wanadhani wanamtisha kumbe ndio kwanza wanachochea kuni. Kama ulivyosema ni kuamka asubuh tunasikia kafutwa Ubunge biashara kwisha. Hizi kelele za mara tumemlipa lisu mara lisu kaondoka na dereva kwa saizi hazina maana.NI MAAMUZI MAGUMU TU,FUTA UBUNGE WAKE.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Pesa dhidi ya uhai siyo kitu, wauaji wameanza kujitokeza

Lissu shikilia hapo hapo huo mshahara dhidi ya uhai wako siyo kitu

Wananchi tutakulipa tu mshahara bila tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
speaker anabwabwaja sana, ni kama anajaribu kumtisha....na wasichojua ni kwamba wanavyozidi kumtisha TL na yeye ndio anavyozidi kupata nguvu ya kuendelea.

go go TL
Yani jamaa wanabwabwaja hadi wanakera. Kama hawana uwezo wa kumfanya chochote si wakae kimya?Hii mikwara ni upuuz tu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Back
Top Bottom