Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Job Ndugai: Ipo siku Tanzania itapigwa mnada, Watu tukishakopa tunapiga makofi kujipongeza. Deni la Taifa ni 70 Trilioni

Nchi haina mwenyewe sasa tiss wanataka kinga ili wawe watekelezaji wa atakayo Rais na CCM.....wana siasa wana kinga kuuza rasilimali zote. N.a. hawataguswaaa ....jeshi wanaona ila watasema hawafanyi siasa lakini nani hasa kusimamia radilimali kubwa kama bandari kuuzwa? Kwakweli hapa Hapana Hapana tujadili kwa mapana yake
Bandari gani imeuzwa wewe? Unapata nini unapo potosha watu? Unajihisi wewe ndo mzalendo peke yako?
 
Spika wa bunge la jamhuri ya muungano JOB NDUGAI amedai kuwa kulingana na mwenendo wa deni la taifa kufikia trilion 70 ipo siku nchi ya Tanzania itapigwa mnada amenena maneno hayo baada ya kusema kwamba tozo zote zamiamala ya simu zilizopitishwa na bunge zilipitishwa kwa lazima kwani wananchi hawakuridhia kama inavyosema na baadhi ya wanasiasa.

Kwa maneno hayo naona kuna mambo yanaendelea huko Lumumba yapo mambo hayajakaa sawa ukiona spika anaanza kulalamikalalamika! Alianza kuhusiana na serikali kuhamia Dodoma kuwa kwa sasa kazi zote za serikali na makongamano zimerudishwa Dar-es-Salaam.

Mheshimiwa Ndugai popote ulipo nakwambia hivi wewe na viongozi wako mnaifanyia nini hii nchi mbona mnakaa mnalalamika lalamika wakati chama ni cha kwenu na chama chenu ndicho kimeunda serikali.?

=====

UPDATES;

=====

=> Watu wengi wanatulaumu sana, ninyi ndio Wasomi. Hebu fikiria, Juzi mama kaenda kukopa 1.3 Trilioni deni.

=> Na tuna majengo hivi sasa ya Madarasa, ya Vituo vya afya, ambayo yanajengwa kwa tozo. Hivi ipi bora? Sisi Watanzania wa miaka 60 ya Uhuru tuendelee kukopa na Madeni au tubanane banane hapa tujenge wenyewe bila madeni Makubwa yasiyoeleweka? Ni lini tutajenga wenyewe?

=> Tutembeze bakuri ndo heshima? na tukishakopa tunapiga makofi! Sisi wa kukopa kila siku?

=> Tukasema pitisha Tozo, anayetaka asiyetaka, pitisha Tozo. Lazima tuanze kujenga wenyewe. Nani atatufanyia? Yupo wapi huyo Mjomba? Tukapitisha Tozo.

=> Sasa 2025 itaamua. Mkitoa waliopo sawa. Waje watakaokuwa kazi yao kwenda kukopa endepo hiyo ndo namna ya kuendesha Nchi.

=> Hivi sasa deni letu ni 70 Trilioni. Hivi ninyi si Wasomi? Is that healthy? Kuna siku nyi itapigwa mnada hii. Madeni Madeni Madeni

=> Bajeti yetu Trilioni 30, Trilioni 10 kati ya hizo kwa Mwaka tunalipa Madeni.

=> Tumeenda Kukopa 1.3 Trilioni, Tunapiga Makofi. Tunawapa Wazungu Trilioni 10 Mariba Matupu. Wanatufanya Sisi Mazezeta. Hela yako Mwenyewe. Anachukua hela yako, halafu anakupa Kidogo Unashangilia.

=> Toza fanya hivi, tujitegemee, Tusimame wenyewe. Kuna ubaya gani? Hata msomi anatupinga.
View attachment 2060338

Zaidi, soma: Thread 'Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏' News Alert: - Spika Ndugai: Rais Samia naomba unisamehe kwa sintofahamu iliyotokana na kauli yangu🙏

Limekosa kunyonya asali yahudi hilo
 
Juzi mama ameenda kukopa 1.3 trilioni. hivi ipi bora. Sisi Watanzania wa miaka 60 ya uhuru kuzidi kukopa na madeni au tubanane banane hapa hapa, tujenge wenyewe bila madeni haya makubwa makubwa haya yasiyoeleweka. Ni lini sisi tutafanya wenyewe ‘and how’ (na kwa vipi),” alisema Spika Ndugai.
 
Kwani ikiuzwa kuna shida gani? Hivi tunavyoishi kuna tofauti gani na kuuzwa?
 
Shikamoo Ndugai
 
Nchi haina mwenyewe sasa tiss wanataka kinga ili wawe watekelezaji wa atakayo Rais na CCM.....wana siasa wana kinga kuuza rasilimali zote. N.a. hawataguswaaa ....jeshi wanaona ila watasema hawafanyi siasa lakini nani hasa kusimamia radilimali kubwa kama bandari kuuzwa? Kwakweli hapa Hapana Hapana tujadili kwa mapana yake
Yaaani waibe kila kitu, waue yeyote wamtakaye, lakini kuuza au kidisha Bandari kwa miaka 100, hii ni kama wanavuka mipaka kuliko mipaka yote iliyowahi kuvukwabtangu kuanzishwa hii nchi. What next?!
 
Chadema wote Hadi kina mange wamempost magufuli kwa ile video akielezeee bandari
 
Siwez kumuunga,mkono Ndugai maana hapo alikuwa anatetea uwepo wa tozo kitu ambacho kinatuumiza wananchi wa kipato Cha chini mpaka sasa, ni wale wale tu wanaojifanya think tank ya nchi ili Hali vichwani weupe
 
Back
Top Bottom