[emoji28][emoji28][emoji28] mkuu una experience na unacho zungumza bila shaka.
Nilipeleka mzigo kwenye kampun fulan hapa dar wanipelekee tabora, gundu linaanza mzigo uko chini mwez mzima,
Sasa nikawafosi wakapeleka nusu, nikaenda mpaka pale kaliuwa nikaingia nayo vijijin ndanindani huko,
Siku niliyofika nimeuza sh 3500 yalikuwa ni maplastik,
Sasa nikaona hapa nimeyatimba, nikauza kwa bei yakurudisha gharama zangu lakin bado,
Akili ikanijia niende pale kaliuwa mjini niuze bei yajumla , nikayarudisha maana nilipeleka kitu ambacho hakihitajiki
Mwenyeji wangu kila nikimwambia tuzunguke wote ananiambia nitulie mpaka siku ya mnada nilipofikia
Mim na yeye tulionana siku hiyo tu
Nikafanya mpango nikayauza palee mjini kwa bei ya hasara, nikaona hii iliyopatikana ngoja nibebe asali huenda niksziba hii pancha niliyopata
Nimeenda inyonga kule katavi nimekuta asali imechachamaa bei nikachukua lita 20 tu,
Baadae nimekaa nasubir magari ya kutoka mpanda nirudi dwaswam napigiwa cm eti ule mzigo nusu wamepeleka sehem yake nijiandae nikaupokee
Iliniuma kwa sababu nilitoa taarifa baada ya huu wa kwanza kubuma huo mwingine wasiulete mpaka niwaruhusu,
ukiangalia huna mdhamin siyo kwenye kampuni wala serikalin tabu tupu hela zenyew ni zile za nusu yako nusu yakurejesha