mimi mtakatifu
JF-Expert Member
- Oct 11, 2019
- 248
- 539
Umeshatuma maombi ya kazi miezi mpaka unahesabu miaka lakini hupati kazi.
Unatafuta vibarua vya kujishikiza navyo inakuwa ni mtihani.
Unafanya kila kitu kujaribu kujinasua na mkwamo wa maisha ikiwemo mambo ya kiimani ila bado hupati matokeo. Uvumilivu, kupambana, ubunifu, experience, knowledge na kila kitu kinashindwa kukupa matokeo mazuri.
Sasa taratibu akili nayo inaanza kuchoka, ulikuwa unafanya application unakosa nguvu. Ilikuwa unazunguka door to door hiyo nguvu tena inakwisha. Mawazo mapya huna tena.
Watu wa kukubeba wamepotea wote. Unatamani upate idea mpya ya namna gani unajinasua ila kichwa hakina tena uwezo wa kufikiri kama zamani. Unaweza kaa siku nzima hujui cha kufanya unaenda mpaka mwezi ufanyi lolote sio kwa kupenda ila akili na mwili haviwezi tena kufanya kazi actively kama awali.
Kwa aliyewai kupitia hali hii alifanya nini ili ku-gain back zile energy za kupambana?
Motivation uliipatia wapi?