Jobless mwenzangu, unafanyaje kupata nguvu mpya baada ya akili na mwili kuchoka na mapambano ya utafutaji maisha?

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2019
Posts
248
Reaction score
539
Umeshatuma maombi ya kazi miezi mpaka unahesabu miaka lakini hupati kazi.

Unatafuta vibarua vya kujishikiza navyo inakuwa ni mtihani.

Unafanya kila kitu kujaribu kujinasua na mkwamo wa maisha ikiwemo mambo ya kiimani ila bado hupati matokeo. Uvumilivu, kupambana, ubunifu, experience, knowledge na kila kitu kinashindwa kukupa matokeo mazuri.

Sasa taratibu akili nayo inaanza kuchoka, ulikuwa unafanya application unakosa nguvu. Ilikuwa unazunguka door to door hiyo nguvu tena inakwisha. Mawazo mapya huna tena.

Watu wa kukubeba wamepotea wote. Unatamani upate idea mpya ya namna gani unajinasua ila kichwa hakina tena uwezo wa kufikiri kama zamani. Unaweza kaa siku nzima hujui cha kufanya unaenda mpaka mwezi ufanyi lolote sio kwa kupenda ila akili na mwili haviwezi tena kufanya kazi actively kama awali.

Kwa aliyewai kupitia hali hii alifanya nini ili ku-gain back zile energy za kupambana?

Motivation uliipatia wapi?
 
Just relax, vuta pumzi kwa na imani mambo yataa sawa, cha umuhimu tu ondoa mawazo epuka sana stress maana zitakupoteza kabisa ishi kama vile unamaisha teyar hata kama hauna just imagine... utakuja kunishukuru
 
Pumzika kidogo kutafuta kazi za maofisini,weka aibu pembeni fanya vibarua vya kutumia nguvu mfano usaidizi katika ujenzi nk rudi nyumbani lala ukiwa na tumaini la kula kesho kichwa kitatulia na Mungu atakufungulia njia
 
I can feel unachokipitia but mafanikio kwanza yanaanza kwenye imagination. Hata ukiangalia waliofanikiwa watakuambia wali imagine kwanza watakavyofanikiwa na wakawa hivyo. So Lazima upige moyo konde ukiamini siku yako ya kufanikiwa ipo na imeeandikwa Apo ndo utapata energy ya kupambana. Lakini pia Kama ni mpenzi wa vitabu soma motivation books
 
bora yako mkuu, umeweza kuelezea hiyo hali.

Sisi wengine hadi tunakuwa mabubu yani maumivu ndani kwa ndani machozi ndani kwa ndani. taratibu jamii imenakutenga unaonekana mwehu.
 
Aisee cha kwanza tambua hiyo situation haupitii wewe peke yako, tuko wengi mkuu ila tunatofautiana kimtazamo akilini. Viko vingi ningeweza kukuambia lkn anza na hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…