Joe Biden ajitoa kugombea Urais wa Marekani 2024

Joe Biden ajitoa kugombea Urais wa Marekani 2024

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
51,303
Reaction score
40,190
Wanaukumbi.

MAREKANI: Rais Joe Biden ametangaza kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais kwa awamu ya pili

Kwa hatua hiyo, Chama cha Democrats kitatakiwa kuchagua Mgombea mwingine.

IMG_3999.jpeg


=====​

Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza kuwa hatagombea tena urais, akisema "ni kwa manufaa ya chama changu na nchi".

Tangazo hilo linakuja miezi minne kabla ya Wamarekani kwenda kupiga kura na kubadilisha mbio kuelekea Ikulu.

Hii inafuatia wiki kadhaa za shinikizo kutoka kwa wanasiasa wa chama chake baada ya utendaji wa kusitasita katika mdahalo dhidi ya mgombea wa Republican, Donald Trump mwishoni mwa mwezi Juni.

Katika barua aliyoweka kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii, alisema imekuwa heshima kubwa zaidi ya maisha yake kuhudumu kama Rais.

"Na ingawa ilikuwa nia yangu kugombea tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi nisimame chini na kujikita kikamilifu katika kutimiza majukumu kama Rais kwa kipindi kilichosalia cha muhula wangu".

Alisema katika taarifa yake kwamba atalihutubia taifa kuhusu suala hilo wiki ijayo.

Rais Biden alimshukuru Makamu wake wa Rais Kamala Harris, akisema alikuwa "mshirika wa kipekee".

"Na wacha nitoe shukrani zangu za dhati kwa wananchi wa Marekani kwa imani na uaminifu mliyonipa," taarifa yake iliongeza.

"Naamini leo na daima kwamba hakuna kitu ambacho Marekani haiwezi kufanya - tunapokifanya kwa pamoja. Tunapaswa tu kukumbuka sisi ni Umoja wa Mataifa ya Marekani."

Wiki iliyopita alirudi nyumbani kwake Delaware baada ya kugunduliwa kuwa na Covid, lakini alisema Ijumaa alikuwa akitarajia "kurudi kwenye kampeni wiki ijayo".

Awali alisema ni "Mwenyezi Mungu tu" angeweza kumfanya ajiondoe, lakini baadaye alisema angefikiria kujiondoa kutokana na hali ya afya.

IMG_20240721_213133_537.jpg

 
So Sasa Mungu wake amemwambia au?
Mtu anaonekana kabisaa anaumwa.
Kama historia ashaweka. Kila siku anahangaika nankukosea mara aje apop mbele za watu bure.
Bora akae pembeni tuu.
Demons kazi wanayo sijui nani Sasa.


Team Trump wa Luguruni hapa
 
Back
Top Bottom