Joe Biden amsamehe Mwanae Hunter Biden makosa yake ya Jinai

Joe Biden amsamehe Mwanae Hunter Biden makosa yake ya Jinai

Kitendo tu Cha mtoto wa bideni kufunguliwa mashitaka ni ukomavu wa mhimili wa mahakama wa marekani.kwa Tanzania nani mwenye ubavu huo wa hata kujaribu tu kumfungulia mashitaka mtoto wa rais?
Toka lini mtuhumiwa "Suspect" akapewa msamaha? Angesubiri ahukumiwe kwanza,si alisema anaiachia Mahakama? Acha kuendeshwa na mahaba.
 
Toka lini mtuhumiwa "Suspect" akapewa msamaha? Angesubiri ahukumiwe kwanza,si alisema anaiachia Mahakama? Acha kuendeshwa na mahaba.
Marekani kuna watu kwao hata akifanyaje hana kosa watasema kwakua marekani hakuna shida ila ingekua Zimbabwe ingekua shida kuna watu vilaza sana
 
Wengi hamjaelewa hata.. , Rais akiwa anamaliza muda wake ana haki ya kikatiba ya kutoa msamaha kwa wafungwa mbalimbali. Hii hata huku kwetu ipo tena kwa muda wowote ndo maana unaskia wametolewa kwa msamaha wa Rais kwa mfano babu seya na nguza... wala Magufuli hakuingilia mhimili wa mahakama kwani ana haki kikatiba kama Rais kusamehe wafungwa

Biden hapo kajieleza sana maana anajua watu watamsema kwa kua ni mtoto wake, Makosa yenyewe ya kawaida sana alikosea kujaza fomu wakati ananunua silaha,kuchelewa(kukwepa) kulipa kodi

Huko democracy bado ipo juu sana, leo hii huku kwetu nani anaweza kwenda hata kumshika mtoto wa Samia eti hajalipa kodi?
Wewe ndie ambae hujaelewa; AMEMSAME KABLA HAJAHUKUMIWA (hajasomewa adhabu) baada ya kuwa amepatikana na hatia.
Hapa kwetu Rais hawezi kumsamehe mtuhumiwa/ mhalifu ambae hajahukumiwa; hiyo itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Wale wanaokuwa wanasamehewa na mamlaka ya Rais wa JMT, tayari huwa ni wafungwa wanaokuwa wanatumikia adhabu zao; nao ni kwa baadhi tu ya makosa.
 
Huyo ndiye mnasemaga eti sijui dada wa demokrasia duniani na msimamizi thabiti wa haki za binadamu? Sasa kik'wapi? Mbona na wenyewe wanasigina katiba kama nchi zetu za kusadikika?
 
Wengi hamjaelewa hata.. , Rais akiwa anamaliza muda wake ana haki ya kikatiba ya kutoa msamaha kwa wafungwa mbalimbali. Hii hata huku kwetu ipo tena kwa muda wowote ndo maana unaskia wametolewa kwa msamaha wa Rais kwa mfano babu seya na nguza... wala Magufuli hakuingilia mhimili wa mahakama kwani ana haki kikatiba kama Rais kusamehe wafungwa

Biden hapo kajieleza sana maana anajua watu watamsema kwa kua ni mtoto wake, Makosa yenyewe ya kawaida sana alikosea kujaza fomu wakati ananunua silaha,kuchelewa(kukwepa) kulipa kodi

Huko democracy bado ipo juu sana, leo hii huku kwetu nani anaweza kwenda hata kumshika mtoto wa Samia eti hajalipa kodi?
Kosa la madawa ya kulevya lenyewe hukuliona?
 
Wewe ndie ambae hujaelewa; AMEMSAME KABLA HAJAHUKUMIWA (hajasomewa adhabu) baada ya kuwa amepatikana na hatia.
Hapa kwetu Rais hawezi kumsamehe mtuhumiwa/ mhalifu ambae hajahukumiwa; hiyo itakuwa ni kuingilia uhuru wa mahakama.
Wale wanaokuwa wanasamehewa na mamlaka ya Rais wa JMT, tayari huwa ni wafungwa wanaokuwa wanatumikia adhabu zao; nao ni kwa baadhi tu ya makosa.
Hunter kahukumiwa Leo, amekubali makosa yake[pleads guilty) mahakama ikamtia hatiani(convicted)..... Huko sio kama bongo ukihukumiwa unapewa miaka ya kukaa jela hapo happy

Tarehe 13 disemba 2024 ndo mahakama ilimpangia aje kujua ni Muda pani atakaa jela.... baada ya hukumu kutoka biden nae aka counter attack kwa kumpa parole, na haki hio kikatiba anayo maana maana tayari mtoto wake Alikua convicted na mahakama Leo hii
 
Toka lini mtuhumiwa "Suspect" akapewa msamaha? Angesubiri ahukumiwe kwanza,si alisema anaiachia Mahakama? Acha kuendeshwa na mahaba.
Hunter kahukumiwa Leo na amepatikana na hatia, tarehe 13 ndo angesomewa muda wa kukaa jela..mue mnafatilia habari vizuri
 
Rais Joe Biden ametoa msamaha " kwa mtoto wake Hunter Biden, dhidi ya mashitaka yanayomkabili katika taarifa iliyotolewa na Ikulu Desemba 1, 2024.​
Hunter Biden alikua akisubiri kusomewa hukumu ya mashitaka yake Desemba, 2024
Septemba 2024 mtoto wa Rais wa Marekani, Hunter Biden (54) alikutwa na hatia ya kumiliki silaha kinyume cha sheria, matumizi ya Dawa za Kulevya pamoja na kukwepa kulipa kodi

Aidha, Juni 12, 2024 Rais Joe Biden alisema ataheshimu uamuzi wa Kisheria wa Mahakama baada ya Mwanaye kupatikana na hatia na kukabiliwa kifungo cha hadi miaka 25 jela

Ni kawaida kwa Marais wanaomaliza muda wao kutoa msamaha kabla ya kuondoka katika nafasi hiyo ambayo inafuta makosa ya jinai
=============For English Audience==========​

Statement from President Joe Biden​

Today, I signed a pardon for my son Hunter. From the day I took office, I said I would not interfere with the Justice Department’s decision-making, and I kept my word even as I have watched my son being selectively, and unfairly, prosecuted. Without aggravating factors like use in a crime, multiple purchases, or buying a weapon as a straw purchaser, people are almost never brought to trial on felony charges solely for how they filled out a gun form. Those who were late paying their taxes because of serious addictions, but paid them back subsequently with interest and penalties, are typically given non-criminal resolutions. It is clear that Hunter was treated differently.

The charges in his cases came about only after several of my political opponents in Congress instigated them to attack me and oppose my election. Then, a carefully negotiated plea deal, agreed to by the Department of Justice, unraveled in the court room – with a number of my political opponents in Congress taking credit for bringing political pressure on the process. Had the plea deal held, it would have been a fair, reasonable resolution of Hunter’s cases.

No reasonable person who looks at the facts of Hunter’s cases can reach any other conclusion than Hunter was singled out only because he is my son – and that is wrong. There has been an effort to break Hunter – who has been five and a half years sober, even in the face of unrelenting attacks and selective prosecution. In trying to break Hunter, they’ve tried to break me – and there’s no reason to believe it will stop here. Enough is enough.

For my entire career I have followed a simple principle: just tell the American people the truth. They’ll be fair-minded. Here’s the truth: I believe in the justice system, but as I have wrestled with this, I also believe raw politics has infected this process and it led to a miscarriage of justice – and once I made this decision this weekend, there was no sense in delaying it further. I hope Americans will understand why a father and a President would come to this decision.​
Riz wa USA
 
Trumpet kamkosa
Amuondoe nchini sasa au atadakwa tena
 
Abdoul Khafidh Sare ya Bila kufungana bila Shaka Atakuwa anamsihi Mama yake aandae Mazingira Mana teyari ana kesi nyingi za ajabu na wakuu wanamtolea njicho.
 
Swali je ,ingekuwa na wewe ungefanyaje ? mtose mwano bahari wakati unao uwezo wakumtoa.
 
Back
Top Bottom