JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 2,118
- 4,863
Rais wa China Xi Jinping amesema yuko tayari kushirikiana na serikali mpya ya Donald Trump kuhakikisha mpito mzuri katika uhusiano wa mataifa yao.
Xi alitoa kauli hiyo alipokutana kwa mara ya mwisho na Rais anayemaliza muda wake, Joe Biden, katika mkutano wa Asia-Pacific uliofanyika Lima.
Mkutano huo ulihudhuriwa huku kukiwa na wasiwasi wa vita vipya vya kibiashara na mvutano wa kidiplomasia pindi Trump atakapoingia Ikulu ya Marekani mwezi Januari. Xi alisema China iko tayari kudumisha mawasiliano, kupanua ushirikiano, na kusimamia tofauti na Marekani kwa lengo la kuimarisha uhusiano wao.
Biden, akielezea maendeleo ya uhusiano wao, alisema anajivunia kazi waliyoifanya pamoja, akisisitiza kuwa mashindano kati ya nchi zao hayawezi kuruhusiwa kugeuka kuwa mizozo.
Alibainisha kuwa, kwa kipindi cha miaka minne iliyopita, wameonyesha inawezekana kuwa na uhusiano wa kiushindani bila kuingia kwenye migogoro.
Mkutano huo ulikuwa wa pili wa ana kwa ana kati ya Xi na Biden tangu mkutano wao wa kihistoria wa kutuliza mvutano uliofanyika California mwaka uliopita.
My take:
Kweli ndiyo maana wenzetu wameendelea sana mkutano watu wazito kama hawa ila kila mtu kwenye meza ana kiti kinafanana bila kujali cheo na hakuna mabwana wakubwa wawili ambao wametengewa viti vyao vya enzi na ma AC yao peke yao ya kusimama jirani yao.
Ingekuwa ni nchi zetu za Africa zenye umaskini wa hela na teknolojia ungekuta hata mkuu wa kijiji ana kiti chake kireeefu zaidi kuwapita wenzake kwenye mkutano.
Source: MSN