Joe Gaetjens, shujaa wa Kombe la Dunia, aliyesulubiwa na Dikteta wa Haiti

Joined
May 21, 2026
Posts
86
Reaction score
191
Mwaka wa 1950 timu dhaifu ya USA ilipanda mtumbwi na kuvuka bahari ya Atantic kuingia nchini Brazil kushiriki kombe la dunia la tatu.

SIku chache kabla ya kwenda baharini kocha wa Marekani alimchukua mwanafunzi wa chuo na muosha vyombo mahotelini viunga vya Brooklyn, New York, JOE GAETJENS, akamjazisha makaratasi ya "kutangaza nia ya kuutaka uraia siku za mbeleni" na kuondoka nae. Kijana Joe alikuwa Mhaiti.

Mechi za makundi dhidi ya UK.

Dakika ya 38 mwalimu wa michezo wa sekondari kutoka mjini Philadelphia, Mwalimu Walter, alishambulia kwa kiki dhaifu ambapo Mhaiti Joe alijitupa chali hewani na kuupiga kichwa kuongezea nguvu. Mpira ukatinga nyavu ndogo.

USA wakisaidiwa na kelele za nguvu za
mashabiki ya Brazil wakasema tutazuia goli mpaka kiama kitasimama, huku golikipa Frank Brorghi, mwendesha magari ya maiti nchini USA, akizuia magoli ya wazi zaidi ya ishirini.

Habari zilipofika UK waandishi wakasema hizi telegram za 1-0 lazima zina typing error. Wakarekebisha, wakaandika 1-10. UK imeifunga USA 10-1.

UK ikakata rufaa ikidai kikosi cha USA kilitumia raia wa Haiti, Scotland na Belgium. FIFA ikasema walijaza fomu za nia ya uraia kabla ya mchezo na ndio sheria.

Mpaka leo huu mchezo ndio unasemwa kama the biggest upset in FIFA World Cup history. Toka 1950, USA haikurudi kwenye kombe la dunia kwa miaka 40.

Joe Gaetjens, japo star mkubwa wa ghafla, hakuendelea kuishi USA, na hakuomba uraia. Alienda kucheza mpira wa kulipwa Ufaransa. Mwaka wa 1954 alirudi kwao Haiti na kunzisha biashara.

Mwaka wa 1957 daktari wa binadamu Francois Duvalier alishinda uchaguzi wa Rais Haiti lakini taratibu akaanzisha udikteta. Mwaka wa 1961 "Papa Doc" akafanya uchafuzi wa uchaguzi, na baadae akatangaza kuwa atakuwa Rais wa Maisha.

Kaka zake na Joe wawili walikuwa wanaendesha harakati za kumtoa dikteta Papa Daktari madarakani kutokea nchi ya jirani ya Domiican Republic japo Joe mwenyewe hakujihusisha kabisa na siasa.

July 8, 1964 Joe alifatwa dukani kwake na

kikosi kazi cha utekaji, utesaji, upotezaji na mauaji cha Dikteta Papa Daktari Duvalier .

Akapelekwa dangulo maarufu la kifungo bila hukumu, utesaji na mauaji la FORTE DEMANCHE.

JOE GAETJEN hajaonekana tena hai wala marehemu.

Mwaka wa 1966, baada ya kufuatiia muda mrefu baba yao yuko wapi, mjane na watoto wa Joe walitoroka Haiti mazima.

Mwaka wa 1971 Dikteta Papa Daktari Duvalier alikufa kwa ugonjwa
Akapokezana nchi na Mwanae "Baby Doc" ambae aliiba dola milioni 400 akiwa Rais.

Mwaka wa 1972 serikali ikathibitisha Joe "died in custody." Hawakusema alikufaje.

Shuhuda zisizo rasmi za askari jela na wafungwa wenzie zilisema Joe alipangwa kwenye ukuta akapigwa shaba takribani tarehe 10 July 1964.

Mwaka wa 1986 Dikteta Baby Doc alikimbia nchi.

================

Kumbe na hii miamba huwa inakimbia.
 
Kumbe kifo alikiogopa,ila katanguliza wenzake!
 
Uzi mzuri..
Ila ina hitaji akili iliyo tulia kuelewa.

Kuna kama story 3 tofauti kabisa tena zinazohitaji separate forums ndani ya uzi mmoja.
 
Ametumia ule mfumo wa kuandika barua isiyo zidi maneno 30 Alafu ieleweke. 😀
Barua za aina hii, kikubwa uelewe heading tu, maana utakacho kutana nacho ndani kinaweza kukufanya uhisi hauna uwezo wa kusoma kwa ufahamu.
 
Back
Top Bottom