Joel Nanauka: Miradi ya Elimu na Afya Ni Msingi wa Kujenga Kizazi cha Taifa

Joel Nanauka: Miradi ya Elimu na Afya Ni Msingi wa Kujenga Kizazi cha Taifa

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Maendeleo ya Vijana, Dkt. Joel Arthur Nanauka amesema miradi ya elimu na afya inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita siyo tu uwekezaji wa leo, bali ni msingi wa kujenga kizazi chenye elimu bora, afya njema na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.

Amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, ambapo aliweka jiwe la msingi la bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari Kabungu na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati ya Manyonyi, miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 353 inayolenga kuboresha huduma za msingi kwa wananchi.

Waziri Nanauka amesema Serikali imeendelea kutenga fedha nyingi katika sekta za huduma za jamii kwa sababu maendeleo ya Taifa yanategemea wananchi wenye elimu bora, afya njema na maadili mema. Amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kuitumia fursa hiyo kujifunza kwa bidii, kujenga nidhamu na kuwa sehemu ya mabadiliko chanya katika jamii.

 
Hii wizara huwa siielewi. Jaribu kuchukua mfano wa ziara hiyo: hiyo wizara umuhimu wake ni wa kutafutwa kwa tochi.

Katembelea shule hapo kuna TAMISEMI na Wizara ya elimu. Vijana unaitafuta kwa tochi.

Njoo kwenye Afya sasa, huko nako kuna Afya na TAMISEMI, hiyo vijana unaitafuta kwa tochi.

Ningeelewa angezungumza umuhinu wa Huduma rafiki za Afya kwa vijana na pia kuwawezesha kupata huduma za matibabu kwa mpango maalum, kuacha Bima, angalau ningemwelewa lakini hata hivyo bado haitoshi kuwa wizara inayojitegemea.

Ingekuwa idara, ambazo zipo TAMISEMI, ningeelewa lakini, bado hainishawishi.
 
Back
Top Bottom