Leo nimenunua kuku (jogoo) kwa ajili ya kitoweo cha kesho lakini tangu nimemfikisha nyumbani anawika sana. Yaani japo nimemfunga lakini anawika mfululizo kama kuna mashindano.
Hii siyo kawaida kabisa, maana nimenunua mamia ya kuku kwa kitoweo ila hawakuwa kama huyu wa leo. Yaani sijui anawaza amekuja kustarehe hapa kwangu? Inaonyesha ni kiasi gani ana dharau sana huyu kuku, yaani anawika nyumbani kwangu!
Nimfanyaje anyamaze hadi kesho siku ambayo nitamchinja?
Nimechoka makelele...