Joh Makini alezea ukweli uliopo kuhusu uvumi wa hisia zake kwa Mimi Mars

Joh Makini alezea ukweli uliopo kuhusu uvumi wa hisia zake kwa Mimi Mars

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mwamba wa Kaskazini anayesumbua masikio ya wapenda burudani na ngoma ya 'Mipaka' Joh Makini amepangua tetesi za kujihusisha kimapenzi na mwanamuziki Mimi Mars ambaye pia ni mdogo wake msanii Vanesa Mdee.

Joh%20mipaka1.jpg


Joh Makini amepangua tetesi hizo kwenye Friday Night Live ya EATV ambapo amesema kwamba tetesi hizo hazina ukweli wowote na kwamba yeye anamchukulia Mimi Mars kama mdogo wake kupitia heshima aliyojenga kwa wasanii hao ambao pia wanatokea kanda ya Kaskazini.

"A Big No. Mimi Mars ni kama mdogo wangu wa kike. Sisi ni familia moja aisee. Ni nani huyo ambaye anasambaza? alijibu Joh Makini kwa mtindo wa kuuliza.

Mbali na hayo Joh Makini amegoma kuweka wazi kuhusu mahusiano yanayodaiwa kuwa ni ya mdogo wake Nikki wa Pili na mpenzi wake Joan kwa madai kuwa hafahamu chochote.

Hata hivyo kumbukumbu zinaonyesha Joh Makini ni moja kati ya wasanii wachache hapa Bongo ambao amefanikiwa kuficha mahusiano yake kwa kipindi kirefu ambacho amesimama kwenye muziki.



EATV
 
Huwa namkubali Joh makini sana ingawa Arusha wengi hawamkubali kwa sababu ya swaga zake
 
Alikuibia wimbo nini mkuu, au shida nini
Acha tu mkuu.. Hii dunia kuna watu wanajiona wajanja sana, nidhamiria kufanya kitu kiovu kwake lakini moyo ukaniambia hapana muacheni tu.. Sitaki kufungaka zaidi kiusalama hapa JF

Simpendi mno huyu kiumbe
 
Back
Top Bottom