Joh Makini ndiyo Msanii/Celebrity Bora wa HipHop na Bongo Flavour kutokea Tanzania

Joh Makini ndiyo Msanii/Celebrity Bora wa HipHop na Bongo Flavour kutokea Tanzania

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Joh Makini ndio Msanii Bora kuwahi kutokea, kuna sababu nyingi ambazo wengine wemeshindwa kuzifikia. Hii ni kutokana na umahiri wa huyu Mtu John Simon Mseke.

Ofcourse kuna wengine wakongwe wangeweza kuchukua hiyo nafasi Ila wana makando kando mengi sana. Nitachambua

1) Yule mkongwe wa miaka ilee ya 90
Huyu ukweli ni kuwa ndio alisaidia kuimba mziki huu kwa kiswahili na kueleweka na kuanzwa kuchezwa redioni na ana albamu nyingi tu.

Ila tatizo lake kubwa ni mdhulumaji sana na ameumiza wasanii wenzake wengi sana. Mfano alianzishaga ile movement, baadae akaitwa pembeni akapewa pesa akasaliti wenzakena movement ikafia hapo. Kuthibitisha hili nenda pale Mwenge waulize mapacha.
Lingine ni mvutaji mkubwa sana wa bangi, inawezekana kweli labda bangi sio mbaya Ila huyu akivuta hakuna kitu mtaelewana tena na anakosa kabisa discpline.
Alivyoingia kwenye siasa ndio alijimaliza kabisa kimuziki na akawa hana jipya tena zaidi ya kugombana na serikali

2) Huyu Bro aliyevuma sana mwanzoni mwa 2000, huyu wa Kimara
Huyu naye alifanya makubwa ikiwa kuamsha watu wengi sana kuwa muziki sio uhuni na alikubarika na rika zote. Tatizo lake kubwa hana discpline ya kazi hasa baada ya kunywa mavitu yake yale magumu(bapa).

Huyu kabla ya kupanda jukwaani lazima apige bapa za kutosha na akishuka akishalipwa basi atakesha na mabapa hadi anazima.
Angeweza kuwa GOAT, lakini suala hili lilikua likimuondolea kabisa discpline ya kazi na kuishia kudharaulika.

3) Yule wa Morogoro
Wapo wataosema basi yule wa Morogoro, huyu ni mtu mmoja mkali sana kuwahi kutokea ila shida yake ni muda wowote kichwa kikipata Moto tu basi anamwaga radhi.
Sio mtu wa kumdhamini hata kidogo, hanaga break.

4) Yule wa Mwanza
Huyu ni mmoja wa watu ninaowakubaali sana, lakini ana makando mengi sana. Na shida kubwa ni mtu wa maneno na ulalamishi sana.
Pia ameshindwa kabisa kumaintain game, ndio maana unaona anakaa hata miaka mitano hana jipya.

Hao ndio watu pekee wangeweza kuchukua nafasi ya Joh Makini lakini kutokana na tabia zao wameangukia pua. Joh Makini kinachombeba ni uwezo Wana na discpline ya Hali ya juu sana kuliko msanii yoyote hapa bongo.

Joh Makini ni mtu ambae unaweza kumtukana unavyotaka na asikujibu chochote yeye huwa busy na muziki wake na maisha yake
 
Hao wengine umetaja kasoro Zao mbona Job naye anazo zake ,haujui au ni uchawa tu
 
Sasa hapa unazungumzia uwezo wa muziki ama tabia?[emoji2][emoji2]
 
Tatizo sisi hatutaki taja makuu ya aibu ya jo na steve b sababu hajatukosea ,hatakaa aoe
 
Back
Top Bottom