Joh Makini, The Tanzania hip hop giant anayepita njia inayomfanya aonekane wa kawaida sana

kanali mstaafu

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2015
Posts
4,318
Reaction score
4,105
Miaka ya 2008 mpaka 2012 ukisikia jina JOH MAKINI unapata picha ya nguli wa Hip hop ambaye alipendwa na wagumu pamoja na mademu at the same time. Joh makini ni msanii wa hip hop ambaye ana vitu vifuatavyo;
Flow za aina nyingi halafu zinabamba
Ana sauti nzuri
Anaweza kurap ktk mdundo wowote
Ni mwandishi mzuri
Ana fanbase kubwa
Ana muonekano wa kisanii

Kila nikisikiliza Stimu zimelipiwa, Hao, Muda, Mfalme, kilimanjaro, brand(blue magic), popote, simwachii Mungu na nyingine kadhaa wa kadhaa naona huyu jamaa anajua sana na ana vitu vingi sana ila anafanya kosa moja

KOSA
Joh makini unapokaa kwenye kundi la weusi unamezwa. Anayenufaika na kundi la weusi ni Nikki wa pili ambaye hana mashabiki wake hvyo kundi linambeba na anatumia fursa vilivyo. Pia Gnako ananufaika na kundi kwa sababu huyu jamaa yeye aliumbwa na Mungu kwa ajili ya kolabo tu na akiimba mwenyewe ngoma zinabuma.

USHAURI
1.Baki katika kundi la weusi ila jikite kutoa ngoma zako mwenyewe na hizo za colabo ziwe chache sana.
2. Piga kotekote kama Fid Q anavyofanya siku hizi, yaani mashabiki zako wa zamani wape ngoma kama Stimu zimelipiwa na wa siku hizi wape nyimbo kama ‘mipaka’
3. Acha kujitenga sana na wasanii ambao sio weusi. Piga kolabo na akina kala jeremiah, mwana FA, Ali kiba, Jay moe, Lady Jay dee, n.k
4. Una package kama ya JAY Z ila ukimdate vanessa au mkatengeneza project na Vanessa mkawa kama mpo wote, mnatoa ngoma, shows na vitu vingine mtakuwa THE CATERS wa bongo.

Ni hayo tu MWAMBA WA KASKAZINI
 
nitajie nyimbo yake hata moja..

#ambayo ukiipanga category moja na nyimbo ya khaligraph Jones itafua dafu na kukwaa kuzo?
Umesema hana kigezo hata kimoja nakuuliza hivyo vigezo ni vipi unaniuliza sijui nyimbo zake

Shida yangu ni hivyo vigezo ambavyo hana nitajie
 
Weusi inabebwa na warawara yule jamaa anajua kupitiliza kila chorus lazima aitendee haki ipasavyo... G ni level nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…