Johannesburg hotel Sinza mnazalilisha wateja kwa kudai risiti za TRA?????

Asante kwa ushauri!ila inauma mtu unadai kitu halali yako matokeo unadhalilishwa kama kibaka!!!!!!
Imagine pia jamaa wangekuitishieni kua nyie ni wezi au majambazi, nini kingefuata? I understand uchungu wa kudai chako, lakini ktk scenario shurti upime cons and pros.
 
Mkulu tuwe realistsic kidogo. Wafanyabiashara wengi wa bongo ni dhalumat balaa. Hebu sikiza kila siku operesheni za TRA, TANESCO, TBS, DAWASCO etc utajua kua wachakachuaji wakubwa ni wafanyabiashara wakubwa. Wanchofanya mara nyingi ni kuji-attach na CCM. Kinachofuata hapo ni kama wanalipa protection money kwa CCM na wao kupitia policcm au mahakama uchwara wanawalinda ktk hali tofautitofauti. This is how MAFIOSO systems works. Unakumbuka kauli ya Sumaye kua ukitaka mambo yako yanyooke ufanyeje? Usiniulize zaidi/
 
Acha Uongo Hii Hotel ni ya Alex Masawe na Huyo Manager Ni Jambazi wa kutupwa sasa nasikia yupo CCM alishawahi kuwa na kesi ya kuiba Costa
Nasikia ameuziwa Sshigongo toka kwa mzee mmoja hivi alikuwa contractor wa nyumba za jeshi Lugalo,si ajabu kuwa naye alimuuzia AM na masawe nyumba zake nyingi kahamisha umiliki kwa kuhofia soo yake na pedeshee Pappa Msoffe
 
TRA wameshapata taarifa, wameshaanza kufatilia
 
Ukisoma michango ya wadau katika hii thread itaona ni jinsi gani watanzania nyie ambao angalau mnajua hata kugonga keyboard either za laptop au vijisimu vyenu mlivyokosa uzalendo na nchi yenu. Sasa hao wanaondesha bodaboda, na wengine wasifika hata form 4 sijui itakuwaje. Badala ya kuona mkwepa kodi (Johannesburg Hotel) ni mhujumu mkuu wa nchi, wote mmeona anayemfichua mkwepa kodi ni fedhuli na mwenye makosa. Of course kwa hali ya maisha iliyo na mienendo ya ubinafsi ya wenye dhamana ya nchi ilivyo hampaswi kulaumiwa kwa mitazamo hii isiyo ya kizalendo.
Lakini inasikitisha sana kama Taifa sijui miaka 25 to 30 ijayo tutakuwa wapi. Hakuna hata mtu mmoja aliyeongozwa na kauli za Chukua chako mapema mwisho wake ukawa wa furaha. Mali zisizo halali na bila jasho zina tabia ya kupeperuka mazingira yakibadilika, hivyo usitokee ukajidanganya eti unachukua chako mapema. Mungu Iangazie nuru ya unyoofu mioyo ya watanzania hawa wasiopenda vijukuu vyao vije kuishi katika nchi nzuri uliyoiumba.
 
mdau kwanza pole kwa yaliyokukuta nimejaribu kuvuta taswira ni mimi ndio imenikuta nikiwa na watu naheshimiana nao ni kweli inakera sn.

nachojaribu kukiona kama ww ulidai kistarabu risiti ya TRA kutoka kwa aliyekuhudumia ambae nahs hakua meneja sasa ikabidi aende kuiomba kwa meneja, meneja akaja na walinzi bila kuhoji zaidi wakawatoa nje kwa hali ya kudhalilishwa.

suala lako bado linautata hasa kuhusu mabishano yenu kati ya wewe na meneja/ mhudumu inawezekana alijitetea ila maneno yake hukuyaamini na mkaishia kutupiana maneno yasiyo mazuri. Mwishoe akaona upo kwenye himaya yake na anamamlaka na sehemu husika basi akaita vijana wake (walinzi) wawatoe nje wote. Hatujui kama mlilipa pesa ya bili yenu au mligoma kulipa mpaka mtakapopewa risiti ya TRA.

ni mtazamo wangu tu uliofinyu kwenye hilo jambo lilikukuta mwenzetu. :A S 39:
 
Kaka siku zote kudai risiti ni wajibu wako na kupewa risiti pia ni haki yako kisheria sababu kuto kudai risiti na kuto kutoa ni kosa na lina faini yake
Kwa hiyo unapopata huduma yoyote risiti ni haki yako na hakikisha ina TIN na kama yuko registered na VAT iwe na VRN ukidai risit ukanyimwa wasiliana na office yoyote ya TRA iliyokaribu yako kwa msaada zaidi.
KUKWEPA KODI NI KOSA LA JINAI NA KUWANYONYA (UFISADI)WENGINE NA KULIPA KODI NI HAKI NA WAJIBU WA RAIA WOTE!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…