Ukisoma michango ya wadau katika hii thread itaona ni jinsi gani watanzania nyie ambao angalau mnajua hata kugonga keyboard either za laptop au vijisimu vyenu mlivyokosa uzalendo na nchi yenu. Sasa hao wanaondesha bodaboda, na wengine wasifika hata form 4 sijui itakuwaje. Badala ya kuona mkwepa kodi (Johannesburg Hotel) ni mhujumu mkuu wa nchi, wote mmeona anayemfichua mkwepa kodi ni fedhuli na mwenye makosa. Of course kwa hali ya maisha iliyo na mienendo ya ubinafsi ya wenye dhamana ya nchi ilivyo hampaswi kulaumiwa kwa mitazamo hii isiyo ya kizalendo.
Lakini inasikitisha sana kama Taifa sijui miaka 25 to 30 ijayo tutakuwa wapi. Hakuna hata mtu mmoja aliyeongozwa na kauli za Chukua chako mapema mwisho wake ukawa wa furaha. Mali zisizo halali na bila jasho zina tabia ya kupeperuka mazingira yakibadilika, hivyo usitokee ukajidanganya eti unachukua chako mapema. Mungu Iangazie nuru ya unyoofu mioyo ya watanzania hawa wasiopenda vijukuu vyao vije kuishi katika nchi nzuri uliyoiumba.