Johari: Nina mpango wa kugombea Ubunge 2020

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Johari.jpg

Msanii Blandina Chagula maarufu kama Johari msanii wa maigizo na filamu nchini ameweka wazi kuwa ana mpango wa kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Johari amefunguka kuwa muda ukifika ataeleza nia yake.

''Nina mpango wa kugombe Ubunge, nia ninayo ila ni vitu ambavyo vipo kwenye mchakato na vikiwa tayari nitaviweka wazi'', amesema kwenye Kingaangoni ya EATV.

Kwa upande mwingine Johari amesema kushiriki kwake kwenye siasa ikiwemo kumsaidia msanii mwenzake Irine Uwoya ambaye alikuwa anagombea ubunge wa viti maalum Tabora haikuwa kwaajili ya maslahi bali alifanya kwa mapenzi.

Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoani Shinyanga, amekuwa mwanachama na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na amekuwa akishiriki katika mambo mbalimbali ikiwemo mikutano mikubwa na kampeni za uchaguzi.
 
Watuletee Maigizo kwenye Siasa tena... Noooo HAPANAAA
Abaki ukouko atetehe kazi za wasanii wenzie
 
Mi mwenyewe nna mpango wa kugombea Urais.
 
kwenye siasa hakuna maigizo na hatuwezi kuongeza watu ambao tunajua wazi hawatakuwa na msaada kwa taifa upuuuz
 
Johari.jpg

Msanii Blandina Chagula maarufu kama Johari msanii wa maigizo na filamu nchini ameweka wazi kuwa ana mpango wa kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.

Johari amefunguka kuwa muda ukifika ataeleza nia yake.

''Nina mpango wa kugombe Ubunge, nia ninayo ila ni vitu ambavyo vipo kwenye mchakato na vikiwa tayari nitaviweka wazi'', amesema kwenye Kingaangoni ya EATV.

Kwa upande mwingine Johari amesema kushiriki kwake kwenye siasa ikiwemo kumsaidia msanii mwenzake Irine Uwoya ambaye alikuwa anagombea ubunge wa viti maalum Tabora haikuwa kwaajili ya maslahi bali alifanya kwa mapenzi.

Blandina ambaye ni mzaliwa wa mkoani Shinyanga, amekuwa mwanachama na kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na amekuwa akishiriki katika mambo mbalimbali ikiwemo mikutano mikubwa na kampeni za uchaguzi.
Vipi bongo movie hailipi?
 
Back
Top Bottom