John Bocco ana makosa madogo madogo

Viol

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
25,420
Reaction score
18,298
Kwenye mechi ya Simba na Mbabane kuna chance Bocco amezikosa kosa sana, anabaki na kipa halafu anampigia mpira badala ya kuangalia angle. Halafu pia hatoi pasi nzuri za umaliziaji kwa wenzake, unaona kabisa Okwi au Kagere pasi ingemfikia ni goli ila Bocco amekuwa akizidisha pasi zinakuwa ndefu.

Bado hana target nzuri, tofauti na chama amekuwa akitoa pasi zenye macho. Simdiss ila ni ukweli mambo madogo ya kujirekebisha maana ni nafasi muhimu kuzitumia kupata ushindi.
 
Nafasi kumi anazopata anashinda moja. Hiyo ndo forward butu
 
JOHN BOKO NI STRAIKA MZURI LAKINI ANAPITA KATIKA KIPINDI KIGUMU KIUCHEZAJI KAMA AMBAVYO WACHEZAJI WENGI HUWA WANAPITA. BAADA YA KUTOKA KWENYE MAJERUHI KABLA HAJAKAA SAWA AKAJITAFUTIA KADI NYEKUNDU YA KIZEMBE KABISA KWA KUMPIGA MCHEZAJI WA TIMU PINZANI. HII ILIMAANISHA KUWA AKAE TENA NJE MECHI MBILI WAKATI BADO ALIKUWA HAJAKAA SAWA KISAIKOLOJIA NA HATA BODY FITNESS KUENDANA NA MDUNDO WA SIMBA ULIVYO KWA SASA.

KOSA KWA KOCHA AUSEMS NI KUENDELEA KUMUANZISHA KILA MECHI BOKO WAKATI BADO HAJATULIA KISAIKOLOJIOA NA KIMWILI WAKATI ANA LUNDO LA WACHEZAJI KWENYE BENCHI AMBAO ANGEWEZA TU KUWATUMIA NA KUMPA BOKO NAFASI KUANZIA DAKIKA YA 70 NA KUENDELEA ILI AWEZE KURUDI TARATIBU KWENYE FOMU. NA KOSA KUBWA KWA BOKO NI KUTAKA KUFUNGA HARAKA HARAKA BILA KUTULIA AU KUWAPA PASI WENZAKE NA YOTE HII NI KUTAKA TU KUONYESHA MASHABIKI KUWA BADO YUPO VIZURI KAMA MASTRAIKA WENZAKE WANAOFANYA VIZURI KWA SASA. MATOKEO YAKE ANAKUWA KITUKO UWANJANI KWA MAGOLI ANAYOKOSA KAMA ILIVYOKUWA KATIKA MECHI YA MBAMBANE ALIKOSA GOLI LA WAZI AMABALO HATA AGGREY MWANRI ANGEFUNGA KWA KUKALIA MPIRA WAKATI HAKUNA GOLIKIPA GOLINI WAKATI KAPEWA PASI NA CHAMA.

USHAURI WANGU KWA BOKO MWENYEWE AMUOMBE AUSEMS AWE ANAINGIA KUANZIA DAKIKA YA 70 KIPINDI CHAPILI KWA MECHI TANO MFULULIZO HALAFU ALETE MREJESHO HAPA JF. NINA UHAKIKA ATAKUWA KARUDI ON FIRE. NA KUOMBA KUINGIA KIPINDI CHA PILI HAITAMPUNGUZIA CHOCHOTE BADALA YAKE ITAKUWA INAMPA FURSA YA KUANGALIA TIMU PINZANI INA MAPUNGUFU GANI NA VILE ITAMSAIDIA KUTUMIA NGUVU ZAKE NYINGI KWA MUDA MFUPI HIVYO KUTOA MSAADA MKUBWA SANA KWENYE TIMU.

USHAURI KWA AUSEMS KAMA ANAPITA HUKU JF AU MANARA AMPELEKEE; ASIPANGE TIMU KWA KUMUOGOPA BOKO. MECHI NYINGI AMEONEKANA DHAHIRI SHAHIRI KUWA HAYUKO VIZURI LAKINI BADO ANAMPANGA TU NA HATA PALE ANAPOONEKANA KUGHARIMU TIMU AMEKUWA MGUMU SANA WA KUMTOA AINGIE MCHEZAJI MWINGINE. AUSEM ANAPASWA AZINGATIE SIMBA KWANZA BOKO BAADAE.

KWA WANAOJUA MPIRA KWA SASA WASINGEMUANZISHA BOKO UKILINGANISHA NA KAZI NZITO ANAYOFANYA KAGERE KWA KUSHAMBULIA NA KUKABA KWA WAKATI MMOJA.
 
Sawa
 
You can't teach an old dog new tricks.......
 
SIO KWELI NDUGU NYANGU NDUMBULA. KWENYE MPIRA USHAMBULIAJI NA HASA UGOLIKIPA NI NAFASI ZINAZOHITAJI SANA UZOEFU NA UZOEFU HUJA BAADA YA KUCHEZA MECHI NYINGI NA MARA ZOTE UTAKUTA MCHEZAJI YOYOTE MZOEFU LAZIMA ATAKUWA NA UMRI MKUBWA KIASI.

NIKIMTAZAMA BOKO BADO ANAWEZA KUCHEZA KWA KIWANGO CHA JUU KWA MIAKA 3 MPAKA 4 IJAYO. ITATEGEMEA YEYE MWENYEWE ALIVYOJIPANGA NA KOCHA WAKE NAMNA ATAKAVYOKUWA ANAMTUMIA.
 
Adam Salamba apewe nafasi huyo Bocco awe anaingia sub
Kwa mawazo yangu Chama angesogea mbele acheze sambamba na Kagere na Okwi, mbali ya kuwalisha hao nyota wawili, atakuwa karibu na goli na ana jicho la kuona, Dilunga acheze nafasi ya Chama. Bocco anaweza kuingia dakika 20 mwisho baada ya kuangalia nani mpira umemkataa siku hiyo
 
You can't teach an old dog new tricks.......
But you can teach an old cow new tricks? The cow in reference Haruna Moshi Boban!!!!!
Look at the mirror before coming up with stupid comments.
 
Bocco si wakumtegemea sana,chances 5 anafunga 1
 
Kucheza atacheza hata miaka mitano, ila hayuko clinical sana,ila labda recently nimemuona anatengeneza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…