Chiligati alichomaanisha ni kuwa;
1. Wana CCM wanaweza kukasirika na kuamua kulinda heshima yao kwa njia zisizo za amani.
Kwa mtazamo wangu, mawazo haya ambayo ni yake binafsi (sio ya wanaCCM) yanataka kuamsha ari ya wanaCCM ambao wala hawana haja ya kupigana na yeyote kuanza kufikiria kupigania chama. Kauli kama hizi ni kauli za hatari sana hasa kutoka kwa kiongozi wa kitaifa kama Chiligati (Waziri, NMEC, M-CC, Katibu Mwenezi CCM - Taifa, Mtu mzima, Baba mwenye familia na Mtanzania).
2. Amethibitisha CCM kutokuwa na nia yoyote ya kupambana na watuhumiwa wa ufisadi. Labda kwa utokutaka, kutokuwa na uwezo au sababu nyingine yeyote.
3. Zaidi ya hayo, anataka wote tushirikiane kulinda na kutetea maslahi ya mafisadi na kuacha kabisa kuwasumbua wanapokuwa wakitumbua rasilimali zetu. Tuwaache wale kwa amani na utulivu.
Mimi nina imani kuwa wana CCM wengi pia wamechoshwa na hali ya kisiasa nchini. Wamechoshwa na kashfa mbalimbali ambazo zinakikumba chama (CCM) na kwa vyovyote vile hawawezi kupambana kutetea ufisadi. Kama Chiligati haamini hivyo, aanze kuamrisha wanachama wake (Mil. 4 anaowasema) kupambana na yeyote anaetukana CCM kwa kulea mafisadi aone response itakuwaje. Ukweli ni kwamba, atagundua kuwa, asipochukua hatua za haraka, atapoteza wanachama hao karibu wote. Uthibitisho wa hili, ni malumbano ya viongozi wa chama hadharani. Chiligati anaweza kudhani kuwa malumbano yanayoendelea kati ya RA na HM ni yao binafsi. No way. Ni lalumbano yanayochomoza kutoka kwa wanachama na wasio wanachama wa CCM. CCM ya sasa itakuwa haina macho kama haioni hili kwa dimension hizi.
Kwa kuongezea tu, CCM haiwezi kuepuka lawama za ufisadi kama hazichukui hatua za haraka kupambana na ufisadi bila uoga na kwa kufuata sheria za nchi (zilizopo). Wahenga wanasema, "Samaki mmoja akioza, wote wameoza". Chiligati aondoe samaki waliooza kwenye kapu lake (CCM) kama anataka kapu lionekane halina samaki waliooza. Naamini kwa kufanya hivyo, ataona shutuma dhidi ya CCM zikififia na kuepusha hali ya upotevu wa amani aliyoizungumzia.
Sisi wote (ndani na nje ya CCM) tunasikitishwa na mwenendo wa chama na hatima ya nchi yetu. Take actions now.