John chiligati vs wapinzani: Vita vya maneno!

John chiligati vs wapinzani: Vita vya maneno!

Habari hii inasikitisha kama c kuhuzunisha,milioni saba ni hela nyingi saana,nikijilinganisha na mimi ina maana huo ni mshahara wangu wa zaidi ya mwaka mmoja.Ebu twende vyuo vikuu,hawa watu ndo wanatoa wahitimu wa fani mbambali mbali,roughly,mshahara wa professor haufiki hata million 2.2M,akikatwa na makato hapo ndo tusiongee,ni nchi hii hii,angalia wasomi wanavyohangaika.Wasomi hao hao wengi wamekuwa wakitumia kuandaa speech za waHESHIMIWA.Ebu fikiria wakulima,kupata sh 100 kule vijijini ni shida,alfu tuseme tanzania ni maskini kweli? Na wale wenye vyeo zaidi ya kimoja je? Maana hiyo mililioni saba ni wale wasio na cheo chochote kule bungeni na sehemu nyingine pia. Lazima nijtajipanga kuwa mbunge cku moja,japo kwa sasa cna chama.

Vyama vya upinzani ,sawa tunashukuru kutuletea mada hii lakini wekeni msisitizo na nyie mjiuzulu ili tuone mlivyoserious,lakini kuongea tu na wakati mnaendelea kulipwa pia hilo halina maana,alafu kama c unafiki ni nini? cku zote mlikuwa wapi kwani mshshara wa wabunge toka uongezwe ni lini? Ebu tubadilishie nyimbo,twambieni mna mpango wa kuendesha nchi hii kivipi?

Suala la kuongea habari za mafisadi haziwezi kuiletea nchi maendeleo bila ya kuwa na mikakakti.Ina bidi mtwambie sera zenu ili tuzidi kuwaconvince wajumbe zaidi wa kujiunga na vyama vyenu.

Mjadili na mada mpya. Tutakuwa tunachambua c kwa story za kifisadi tu bali na mikakati mliyokuwa nayo ya kuleta maendeleo nchini.
Zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Habari hii inasikitisha kama c kuhuzunisha,milioni saba ni hela nyingi saana,nikijilinganisha na mimi ina maana huo ni mshahara wangu wa zaidi ya mwaka mmoja.Ebu twende vyuo vikuu,hawa watu ndo wanatoa wahitimu wa fani mbambali mbali,roughly,mshahara wa professor haufiki hata million 2.2M,akikatwa na makato hapo ndo tusiongee,ni nchi hii hii,angalia wasomi wanavyohangaika.

Ndio maana wahadhiri (Profs Kapuya, Sarungi, Mwandosya, Dr. Mwakyembe nk) nao wanakimbilia kwenye siasa, manake ndiko kwa muda mfupi unaneemeka. Na wakishaingia Bungeni hawateteitena maslahi ya wafanyakazi wengine bali huangalia marupurupu yao. Hapo bado wakimaliza muda wao wanapewa marupurupu ambayo kuna watu kibao wanafanya kazi zaidi ya miaka 40 hawayapati.
 
Date::3/23/2009
"Juzi nimesema posho za wabunge zipunguzwe, Sitta analalamika kuwa naingilia haki za bunge sasa leo nasema tunalipwa jumla ya Sh7 milioni kwa mwezi, acha posho za bungeni. Kweli hii ni halali kwa taifa masikini kama Tanzania," alihoji Dk Slaa.

Alisema malipo ya ya Sh135,000 kwa siku na ya Sh7 milioni kwa mwezi ni makubwa mno kwa wabunge kwa kuwa wafanyakazi wengi na Watanzania wanalipwa mishahara midogo na hivyo kuishi maisha duni.

"Mamilioni haya ya fedha kwenda mifukoni mwa watu ni aibu kwa nchi. Chadema tunasema hapana! Fedha hizi ziende katika masuala ya kusaidia jamii na kuongeza mishahara ya walimu, polisi, mahakimu na watendaji wengine," alisema Dk Slaa.

- Maneno mazito sana, sometimes inachukua muda kwa kiongozi kutafakari ubaya wa jambo, sasa kibaya ni kama akinyamaza kimya moja kwa moja, lakini pamoja na kwamba DK, amekua akipokea hizi hela kwa muda mrefu sasa cha muhimu ni kwamba finally amesema wazi kuwa hafurahishwi na hii tabia ya kulipwa mahela mengi hivi over migongo ya masikini wanyonge wananchi.

- Na amefikisha ishu hii mbele ya sheria na pia ni changamoto kwa wabunge wengine wote, tunasema bravo DK. Slaa kwa hii hoja nzito sana, ingawa imechelewa sana lakini si haba na ifanyiwe kazi mara moja.

William.
 
Dr. Slaa tunakusikia tena kwa sauti kubwa sana. Mshahara wa TShs. 7 millioni kwa maoni yangu sio nyingi za kutisha kwa kazi ya ubunge, lakini hizo posho za TShs. 135,000 sielewi kabisa kwa nini ziwepo ikiwa kazi ya wabunge ni vikao vya kujadili na kutunga sheria.

Hii ni sawa na kuwalipa waalimu posho kwa ajili ya kusimamia majaribio (test) za wanafunzi.

Mkuu unalinganisha na mishahara ya sector gani. Bunge ni sehemu ya serikari hivyo Tshs. 7 million ni mshhara mkubwa sana ukilinganisha na watumishi wengine serikarini. Hata private sector TZ nadhani mishahara hiyo ni nadra sana
 
Milioni saba sio nyingi ,ndugu hebu fikiria tena Unazungumzia Tanzania sio Ulaya.
Milioni Saba katika Nchi ya mwisho kwa Umasikini unasema sio nyingi kwa mtu anaekaa na kupiga makofi tu kushangilia wengine,wakati mshahara wa daktari anaetibu magonjwa ya hatari na kuhatarisha afya yake haukatizi huko ,polisi anaepigwa na jua pale getini na kutafunwa na mbu usiku kucha akiwa mlinzi wa Mkuu wa mkoa hata haunusi huko ,mwalimu aneota masuguru kwenye vidole kwa kushika chaki kila siku kwa kumfundisha raisi mtarajiwa haoni ndani ya mshahara huo na ambae hulipwa bakora na DC,wanajeshi wanaochukua dhamana ya nchi na kuishi mbugani muda mwingi wa maisha yao hawakaribii kabisa huko kwenye milioni saba na akimaliza unapishana nae njiani anaendesha basikeli na kakuvalia yeboyebo,halafu unasema milioni saba ni vijisenti tu ,aloo wewe inaonyesha hujafika hapa nyumbani miaka mingi ukaona ni jinsi gani watu wanateseka na maisha ,wakati mbunge na viongozi wanatembelea magari ya kifahari ,akina mama wajawazito wanaswekwa kwenye chumba kimoja hata wakiwa mia watabanana humo humo,na kuzalishana humohumo ,hivi tuna wabunge wangapi ,zaidi ya mia mbili ni milioni ngapi hizo ,hivi ikiwa wabunge wataamua nusu ya mishahara yao ipelekwe kwenye kujenga vituo vya akina mama kutakuwa na kosa,mbona upo na mawazo ya kudharau sana, milioni saba si fedha kidogo kwa Tanzania ni fedha nyingi sana kuipokea kila mwisho wa mwezi nafikiri ni kama dola 2000 kwa mwezi ,hiyo ndugu si fedha ndogo kwa Tanzazia kuipokea kila mwezi mbali ya posho ,kwa miaka mitano 2000 x 12 x 5 mbunge posho tu inamuendeshea maisha yake.
Mkuu unalinganisha na mishahara ya sector gani. Bunge ni sehemu ya serikari hivyo Tshs. 7 million ni mshhara mkubwa sana ukilinganisha na watumishi wengine serikarini. Hata private sector TZ nadhani mishahara hiyo ni nadra sana
Tunaweza kujadili wingi au uchache wa hizo TShs. 7 millioni. Lakini lengo lisiwe uwiano kati ya mbunge na polisi, mwalimu n.k, bali mahitaji halisi ya wabunge, polisi, waalimu n.k.

Mishahara ya waTZ wengineo wote nayo inafaa iangaliwe kwa miongo hiyo hiyo, lakini udogo wa mishahara ya wengine isiwe kikwazo cha kuwalipa wabunge ipasavyo na kuwafanya wabunge washindwe majukumu yao.
  1. Kwa mtazamo wangu ni kuwa, kama hizo TShs. 7mil. zinajumlisha matumizi ya ofisi zao majimboni, basi hiki ni kiwango kinachoweza kukubalika. Shida ni kuwa hatujafahamishwa kama kuna utenganisho wa mshahara wa Mbunge na pesa ya matumizi jimboni.
  2. Ingefaa liwepo fungu tofauti kwa ajili ya matumizi jimboni na kila mbunge ahitajike kuajiri angalau wasaidizi wawili hivi na kuwa na ofisi inayohudumia wananchi saa zote za ofisi.
  3. Kuwalipa pesa nyingi bila kutenganisha matumizi ya jimboni, ni makosa na ndio maana hiki kiwango huonekana kikubwa na pia inawafanya wabunge wasiwajibike majimboni kwa vile hawahitajiki kuthibitisha jinsi walivyotumia.
 
Mkuchika haelewi anachokisema, na kama anakiongea basi ni kwa shinikizo. Hivi ni mtanzania gani (hata kama ni mwana CCM) atakayekwenda kumpiga jiwe au nondo Dr. Slaa, kisa kasema wabunge wanalipwa milioni saba kwa mwezi? Pia ni bongo lala gani huyo wa CCM atakaye mnasa Kelbu Dr. Slaa kisa kasema kuwa CCM walichota fedha za EPA?

Kama CCM inaona inakashfiwa, na inaridhika kuwa muda si muda, baada ya wanachama wake (Kama kweli wanafika MILIONI 4) kuchoshwa na ngebe za Dr. Slaa wataanzisha varangati, basi ni kwanini isimshtaki Dr. Slaa mahakamani?

Hii itawasaidia kuendelea kupata ridhaa ya Wana CCM na watanzania kwa ujumla.

Vinginevyo CCM ijiandae kushushiwa varangati.
 
Hii! Hii!

Captain Joni kweli safari hii vijana wamekugusa pabaya.

MH Ukihusishwa na Ufisadi unauchaguzi. Kukaa kimya na kuto jibu hoja kama baadhi ya mafisadi wafanyavyo. Pili kujibu hoja kwa hoja kama chama na kuonyesha kwa vitendo jinsi CCM ichukiavyo ufisadi kwa kujitenga mbali na wanachama wanao nuka ufisadi.
CCM haina mamalaka ya kisheria ya kutoa utetezi wa wanachama wake wakihusishwa na ufisadi kwa mtindo wa kuwapa kinga ya kidola.
CCM ilitakiwa kuwa mstari wa mbele kuchunguza tuhuma za mafisadi wote waliotajwa ambao ni wanachama wenye nguvu ndani ya CCM.
KWa vile CCM ni mkusanyiko wa Wanachama Millioni 4 ambao wako tayari kufa ili kuhakikisha watu wasiozidi 1000 wanalindwa kwa gharama zote hata ikibidi kuanzisha vita ili wasibughuthiwe? Sioni ni kwa nini wananchi 32,000,000 waliobakia wasi wanachama wa CCM wakae kimya na kushuhudia kundi la watu Milioni 4 lililotufikisha hapa kwa makusudi likitaka kuanzisha mkakati mwingine wa kutengeneza matatizo mapya.

Labda tu kama....

Maneno aliyotamka Captain Joni

"Tunatoa onyo la mwisho hatutakubali kuona chama kinakashifiwa, kinatukanwa na kuchezewa vinginevyo wanachama wetu wapatao milioni nne (4) wakikasirika na kuchukua hatua ya kulipiza kisiasa AMANI ITATOWEKA!!"

yana maana hii

Wanajeshi wote wa vikosi vyote vya jeshi ni wanachama wa CCM.
Polisi wote wa Tanzania ni wanachama wa CCM.
Mahakimu na majaji wote Tanzania ni wanachama wa CCM.
Idara yote ya Usalama wa Taifa ni wanachama wa CCM.
Wafanya kazi wote serikali ni wanachama wa CCM.

Kama maneno yake Captain yana maana hii na ndiyo dhana halisi ya wanachama million 4 kweli ana haki ya kutamba kama dume la nyani, vinginevyo ni hasira za kushikwa pabaya au wamemtuma atuletee mkwala nchi nzima bila kumweleza vizuri namna ya kuleta ujumbe wenye hoja ficho.

Tuchukulie kwamba CCM itaendelea kutushwa ndoo ilojaa Mafisadi bila kujali maneno ya Capt, hapo itabidi na sisi tukae mkao wa kukosa amani.

MH Afande Mku,ninyi mko tayari na Bunduki zenu Vifaru na mabomu na nyuma yenu JWTZ.

Sisi upande wetu tuko na Pinde na mishale, magobole, mabomu ya petroli, mabomu ya mbolea ya urea. Na nyuma yetu ni makapteni,makoplo na masajenti wastaafu wa JWTZ tunaoishi nao maisha ya dhiki huku ushwazi bila kusahau ujuzi wetu wa uchaka tulo upata kule Makutupora na Msange.

Ujumbe kwako Capt Joni ni huu.

Amani uisemayo ikitoweka inatoweka kweli, itakuwa shida kidogo kwa kila mtu kujitokeza hadharani na kutamba jinsi ulivyotamba. Usidhani amani itatoweka na wewe na vilaza wenzio wa CCM mtaendelea kutamba nchi nzima huku mmevunja visambusa kwenye MaVX na MaGX. Litazuka kundi jipya kabisa la wahuni ka ninyi watakaokuwa wakitamba.
Kama huna fununu pata habari au tembelea Somalia au Kaskazini mashariki ya CONGO.

Itakuwa hivyo kama maana ya kutoweka kwa amani uisemayo ni kile kitendo cha Majeshi yenu kwenda kupiga watu mitaani na huko vijiji bila wao kujitetea.
Hiyo kitu mimi naiita ubabe ushenzi na msuli wa CCM si kutoweka kwa amani.

Kama maana yako ilikuwa ni hii ya pili, hukutakiwa kusema amani itatoweka,
ulitakiwa kusema Mkiendelea kufichua ukweli mtajua sisi ni nani, shughuli ambayo mmekuwa mkituonyesha tangu siku nyingi.

Kutoweka kwa amani si jambo dogo kama ulivyolegeza maana, kulishusha kulifanya ni sawa na kuchapa watu viboko mtaani, hasa ikizingatiwa kwamba wewe ni captain wa jeshi.

Amani ikitoweka inatoweka.
 
Last edited:
Tamko la kiongozi mkuu wa chama/ serikali ni tamko la chama/ serikali, mpaka pale kiongozi huyo atakapofafanua kwamba tamko hili ni la kwake binafsi na si la chama/ serikali.
 
Siku hizi hawarudishi kwa culprit, wana donate kwenye charity.

Kwa hiyo swali liwe Dr. Slaa ana donate kwenye causes hicho kilichozidi? Au anafanya maigizo tu?

All in all, ana point muhimu sana na hata kama ana donate au ha donate ni muhimu kuwa na standard itakayo apply kwa wabunge wote, kitu ambacho Dr. Slaa anakipigania.

Unafanya makosa, nadhani Kiranga, ku wonder whether haya malalamiko yake ni maigizo halafu hapo hapo unasema "na hata kama ana donate au ha donate..." Ukisema "hata kama..." kwangu naona hujali huo usanii wa kulalamika huku analamba cheki vizuri, kama tunavyo wonder whether anafanya.

Na hizi concept za ku donate hela chafu kwenye charity zipo sana Magharibi, kama Marekani, hebu tuangalie Marekani kabla hatujarudi nyumbani real quick.

Mayor Michael Bloomberg anarudisha cheki zake zote kwenye serikali ya New York City ambako anaona wanahitaji zaidi hiyo hela kuliko yeye. Angelamba cheki akaipeleka kwenye charity angeambiwa, oh yeah? Unataka kunenepesha Bloomberg Foundation kwa kuchukua cheki New York City government kuipeleka kwenye mfuko wa Bloomberg halafu unajifanya kusema New York City wanahitaji hii cheki zaidi yako na foundation zako?

Dr. Slaa anasema hiyo cheki yake inahitajika zaidi kwenye program za serikali. Na yeye wangemuuliza, cheki yako wewe unarudisha, unanenepesha Dr. Slaa Foundation au unalalamika na kuilamba?
 
Kabla ya uchaguzi ujao 2010 tutasikia mengi na tutashuhudia mengi. Hatari moja iliyo mbele yetu ni kuwa kuna uwezekano hiki kigenge cha wezi na mafisadi kisikubaki kuachia madaraka. Maslahi ya CCM lazima yalindwe hivyo CCM inatangaza mapambano dhidi ya Watanzania - milioni nne (?) dhidi ya watanzania milioni arobaini. Vyombo vya dola vyenye silaha za moto dhidi ya wananchi wasio hata na kombeo - lakini wana nguvu ya umma. Walioshiba na kujaa misuli dhidi ya walala hoi wenye njaa - lakini waliojaa hasira. Wenye mamilioni ya vijisenti yaliyofichwa benki za nje dhidi ya wakulima na wafanya kazi wasio na mbele wala nyuma - lakini walio tayari kulinda hicho kilicho chao. Bahati nzuri ni kuwa mshindi kwenye mapambano kama haya huwa anajulikana mapema bila hata kuingia kwenye ulingo.
Ole wako Chiligati !!​
 
Dr. Slaa Heshima Mbele,

Ila kupiga kelele na kujibishana kati yenu hakusaidii sana,ila tunachotaka ni mikakati ya maendeleo na nini kifanyike kuwaondoa mafisadi.Mmpeza sauti sana ila usanii bado uko [pale pale],na hatujaona cha maana ambacho wamefanya.

Mie hata sijui kesi za watu wa EPa zinaendeleaje?

We need a new Move while we are waiting 2010

Hatuna budi kuwapongeza kwa jitihada zao na jaribu kufikiria vipi anavyoonekana Dr Slaa na wabunge wenziwe. Hii ni hatuwa mbele kwani wale wasiofahamu inabidi wafahamu kuwa hivi vita vya maneno kati ya Wabunge haina maana yoyote kwetu walala hoi.
Mtu anapokea zaidi ya pencheni anayopata mfanyakazi wa kawaida baada ya miaka ya kutumikia Taifa, kwao wao ni kipato cha mwezi mmoja. Hadi sasa siamini na nilichokisikia, millioni saba na maposho juu na wakimaliza miaka mitano wanamiminiwa mamilioni mengine. Du kumbe Tanzania si Masikini kama tunavyoambiwa. Wacha Maprofesa na Wahadhiri wakimbilie ubunge.
 
Dr kaniacha hoi.....eti leo miaka mi4 ndio anasema posho zao nyingi is he kidding me?

yeye angetuambia yeye hayo mapesa yote anaona ni ubadhirifu anazipeleka sehemu za maendeleo lakini anazichukua tu huku analalamika ati nyingi......wabunge bwana..

Hata hivyo hakuna baya lisilo na wema ndani yake. Revealation ya DR imesaidia kutowa majibu ya masuala mengi tuliokuwa tukijiuliza.

Tusubiri mapigo kutoka kwa Mr SIX ni mtetzi mkubwa wa maslahi ya Wabunge.
 
Tunaweza kujadili wingi au uchache wa hizo TShs. 7 millioni. Lakini lengo lisiwe uwiano kati ya mbunge na polisi, mwalimu n.k, bali mahitaji halisi ya wabunge, polisi, waalimu n.k.

Mishahara ya waTZ wengineo wote nayo inafaa iangaliwe kwa miongo hiyo hiyo, lakini udogo wa mishahara ya wengine isiwe kikwazo cha kuwalipa wabunge ipasavyo na kuwafanya wabunge washindwe majukumu yao.
  1. Kwa mtazamo wangu ni kuwa, kama hizo TShs. 7mil. zinajumlisha matumizi ya ofisi zao majimboni, basi hiki ni kiwango kinachoweza kukubalika. Shida ni kuwa hatujafahamishwa kama kuna utenganisho wa mshahara wa Mbunge na pesa ya matumizi jimboni.
  2. Ingefaa liwepo fungu tofauti kwa ajili ya matumizi jimboni na kila mbunge ahitajike kuajiri angalau wasaidizi wawili hivi na kuwa na ofisi inayohudumia wananchi saa zote za ofisi.
  3. Kuwalipa pesa nyingi bila kutenganisha matumizi ya jimboni, ni makosa na ndio maana hiki kiwango huonekana kikubwa na pia inawafanya wabunge wasiwajibike majimboni kwa vile hawahitajiki kuthibitisha jinsi walivyotumia.

Hata nyingi ya hizo ofisi za serikali hazipati hizo mill 7 kwa mwezi kwa matumizi ya kawaida.
 
Sijui Dr. Slaa anapokea mshahara na posho yake yote au anarudisha cheki serikalini?

Itakuwa na impact kubwa kama Wabunge wote wakikatwa mishahara yao marupurupu mengine badala ya Dr Slaa pekee ndiyo maana ameonyesha njia kwamba hili likifanywa linaweza kupunguza sana manung'uniko ya walimu na kuwasaidia katika gharama zao za maisha.
 
Unafanya makosa, nadhani Kiranga, ku wonder whether haya malalamiko yake ni maigizo halafu hapo hapo unasema "na hata kama ana donate au ha donate..." Ukisema "hata kama..." kwangu naona hujalo huo usanii wa kulalamika huku analamba cheki vizuri, kama tunavyo wonder whether anafanya.

Na hizi concept za ku donate hela chafu kwenye charity zipo sana Magharibi, kama Marekani, hebu tuangalie Marekani kabla hatujarudi nyumbani real quick.

Mayor Michael Bloomberg anarudisha cheki zake zote kwenye serikali ya New York City ambako anaona wanahitaji zaidi hiyo hela kuliko yeye. Angelamba cheki akaipeleka kwenye charity angeambiwa, oh yeah? Unataka kunenepesha Bloomberg Foundation kwa kuchukua cheki New York City government kuipeleka kwenye mfuko wa Bloomberg halafu unajifanya kusema New York City wanahitaji hii cheki zaidi yako na foundation zako?

Dr. Slaa anasema hiyo cheki yake inahitajika zaidi kwenye program za serikali. Na yeye wangemuuliza, cheki yako wewe unarudisha, unanenepesha Dr. Slaa Foundation au unalalamika na kuilamba?

- Mike Bloomberg, sasa ndiye namba one billionea wa NY hahitaji hela safi wala chafu, sasa tunataka kumlinganisha Bloomberg na DK. Slaa? hivi kweli wananchi wote humu ndani hawajui kuwa huwezi linganisha hawa viongozi financially?

- Inaelekea unaogopwa sana hapa mkuu duh mfano wako ni chini sana hawafanani kabisa kipesa na hakuna wa kuku-challenge?, Bloomberg na DK. Slaa wapi na wapi? Bloomberg ametumia dola za kimarekani $ 200 Milioni kuwa mayor mara mbili NY, sasa utamlinganisha vipi na DK. Slaa wa Karatu?

- What a genius! ni lini ulijua kuwa wabunge wetu wanapata hela chafu? what did you do about it maana atleast hapa tunajua DK. Slaa alichokifanya!

Bravo Dk. Slaa kwa kusimama uhesabiwe.

William.
 
Last edited:
Nashindwa kuelewa huyu jamaa kwa nini alisema alichosema.

Aliyoyasema ni haya:

(a)Aonya vyama vya upinzani kutoihusisha CCM na ufisadi, vinginevyo amani itavurugika.

(b) Visimchafue rais Kikwete, HOW?

(c)"Tunatoa onyo la mwisho hatutakubali kuona chama kinakashifiwa, kinatukanwa na kuchezewa vinginevyo wanachama wetu wapatao milioni nne (4) wakikasirika na kuchukua hatua ya kulipiza kisiasa AMANI ITATOWEKA!!(Damn! Yaani sheria mkononi inaungwa mkono na waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na mjumbe halmashauri kuu CCM)

(5) Adai CCM itakufa na mtu.,

Does this sound new to you? NO...Safari 2010 ishaaanza wazee, tusiojiweza tukaeni pembeni na kuangalia yatakayotokea!

Je kauli za Chiligati zinafaa na zinatuma ujumbe kwa taifa lililo huru kama la Tanzania ?

CCM ndiyo chanzo cha machafuko na matatizo hapa Tanzania. Wananchi wamekuwa wakipigia kelele machafu, wizi na madudu yanayofanywa na CCM, lakini CCM imekuwa kiziwi wakati inasikia na kuelewa nini kinaendelea.
Huyu Chiligati amekosa hekima ya kuelewa hilo. Angewashauri CCM wasikilize vilio vya wananchi na wajirekebishe ili kuepusha kelele ambazo siku za usoni zitazaa machafuko.

Kelele zisizokwisha za wananchi ni dalili tosha kabisa kwamba watanzania wamefika kikomo (Enough is Enough) na siku ya siku ikifika basi mapanga, bakora, visu, bunduki, mishale, mawe nk vitawaandama CCM na kundi lao la mafisadi.
 
Unafanya makosa, nadhani Kiranga, ku wonder whether haya malalamiko yake ni maigizo halafu hapo hapo unasema "na hata kama ana donate au ha donate..." Ukisema "hata kama..." kwangu naona hujali huo usanii wa kulalamika huku analamba cheki vizuri, kama tunavyo wonder whether anafanya.

Na hizi concept za ku donate hela chafu kwenye charity zipo sana Magharibi, kama Marekani, hebu tuangalie Marekani kabla hatujarudi nyumbani real quick.

Mayor Michael Bloomberg anarudisha cheki zake zote kwenye serikali ya New York City ambako anaona wanahitaji zaidi hiyo hela kuliko yeye. Angelamba cheki akaipeleka kwenye charity angeambiwa, oh yeah? Unataka kunenepesha Bloomberg Foundation kwa kuchukua cheki New York City government kuipeleka kwenye mfuko wa Bloomberg halafu unajifanya kusema New York City wanahitaji hii cheki zaidi yako na foundation zako?

Dr. Slaa anasema hiyo cheki yake inahitajika zaidi kwenye program za serikali. Na yeye wangemuuliza, cheki yako wewe unarudisha, unanenepesha Dr. Slaa Foundation au unalalamika na kuilamba?

Seeming contradictions, like being able to entertain two opposing ideas at the same time as Darwin did when proposing evolution and at the same time entertaining doubt on the integrity of that idea due to the complexity of the eye and the low probability of that organ having risen out of evolution, far from being discrediting, are the hallmark of genius.Once argued through, they actually have the effect of strengthening the original argument in some sort of empirical criticism.

Further, you did not seem to understand my idea of branding the government "culprit". If this understanding was bestowed upon your faculties, you could have arrived at the conception of my entire rationale.

You are so predictable Kuhani,as I was writing I anticipated your line of thought from you, which is not always a bad thing, especially if you are or have ambitions of becoming an automaton.

Nimefurahi umesema "nadhani", kwani wewe mwenyewe unaonekana huna uhakika.Nikitaka kukufunga kwa sheria yako mwenyewe, ya kuwa na hakika na kuongea vitu definite tu, basi post yako yote baada ya neno "nadhani" inakuwa haina maana. Watu tofauti wanaweza kudhani mambo mengi tofauti, sema unachojua utanipa munkari wa kujadili, una uhuru wa kudhani chochote unachotaka na
 
Last edited:
- Hapana this one sio kweli, eti Chadema nzima inaunga mkono hoja ya Mheshimiwa Zitto ya taifa kununua mitambo mtumba ya Dowans? Misemo mingi ya wahenga haikubaliani na demokrasia makini na smarts politics za kisasa.

Mkuu W. J. Malecela, usemi huo (Samaki mmoja akioza wote wameoza) una maana kila unapotumika. Mfano wa Chadema ulioutoa umeupinda kidogo. Sio mbaya, nitaurekebisha.

Usemi huo una maanisha ni vigumu kujua ni samaki gani alieoza katika kundi la samaki ambalo linatoa harufu au dalili nyingine zozote za uozo, na hivyo kuwa rahisi kusema kuwa wote wameoza (kwasababu za usalama wa mlaji ama sababu nyingine zozote). Kwa vyovyote vile, ni safe zaidi kuchukulia kuwa wote wameoza hadi hapo utakapoweza kubainisha yule alieoza kutoka katika kundi hilo na kuwa wengine hawajaoza, kuliko kuchukulia kwa ujumla tu kuwa mmoja ndie alieoza bila kuwa na uhakika.

Kujibu mfano ulioutoa: Kusema kuwa Mheshimiwa Zitto anaunga mkono hoja ya kununua mitambo ya Dowans maana yake ni Chadema nzima kuunga mkono, inaweza kuwa na ukweli ama isiwe na ukweli pia. Inakuwa na ukweli pale tu ambapo Chadema wanakuwa kimya kuhusu msimamo wao kuhusu manunuzi hayo (na hivyo kutojua kama wanaupinga), au wengi wa viongozi wao wanapokuwa na kauli zinazofanana na kuunga mkono manunuzi hayo (na kudhihirisha kuwa wanaunga mkono).

Vile vile inaweza isiwe na ukweli kama kuna kauli zinazopingana na manunuzi hayo za wazi kabisa kutoka kwa viongozi wa chama hicho. Na hivyo kuwa na uhakika kuwa, uungwaji mkono huo ni wa mtu mmoja tu.
 
- Ndugu nimekusikia, kwamba samaki mmoja akioza wote wameoza, sasa naomba kuweka swali la nyongeza, eti Bin Laden anawakilisha mawazo ya Waisilamu wote duniani?

Ahsante.

William.
 
Back
Top Bottom