Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
JOHN FRANCIS RAIA WA MAREKANI ALIYETEMBEA KWA MIGUU MIAKA 22 AKIIZUNGUKA MAREKANI KUHAMASISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Umewahi fikiri kuwa unaweza kukaa kwa siku au miaka mingapi bila kuzungumza chochote yaani bila kutoa sauti, kwa kawaida tu binadamu tunatofautia wengine hata sekunde moja haiwezi pita bila kuzungumza chochote.
Najua wote tunafahamu adha ya kutembea kwa miguu kwa mda mrefu hasa wakati wa mchana pale ambapo jua ndo linakuwa limekolea si rahisi mtu kutembea kwa miguu tena kwa umbali mrefu hata kama ana usafiri binafsi au anatumia usafiri wa umma.
Leo tuangalia kisa cha mwanaume mmoja kutoka nchini Marekani aliyeacha kutembelea gari yake na kuamua kutembea kwa miguu akizunguka maeneo yote ya Marekani.
John Francis alizaliwa Kaskazini mwa Philadelphia katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani mwaka 1946, mama yake alikuwa anajulikana kwa jina la Java alikuwa na kaka yake pia aliyekuwa akiitwa Dwayne.
Francis alitumia mda wake mwingi akifanya kazi za shambani katika vijiji vya Virginia lakini ilipofikia mnamo mwaka 1960 Francis alihamia Califonia kaskazini mwa San Francisco.
Inaelezwa kuwa Francis alitembea kwa kutumia miguu katika majimbo yote 48 ya nchini Marekani na maeneo ya kusini mwa Amerika.
Je ni kwa nini John Francis aliamua kutembea kwa miguu kwa miaka 22? si kwamba alikuwa hana pesa ya usafiri hapana bali alikuwa na sababu.
Jambo lililobadilisha mtazamo wa maisha ya Francis ni lile tukio la Januari 17, mwaka 1971 siku hii kulitokea ajali katika ghuba ya San Francisco ambapo meli mbili za mafuta ambazo ni Arizona Standard na Oregon Standard ziligongana na kusababisha mafuta kiasi cha galoni 800,000 kumwagika na kuenea katika ghuba hiyo na kuleta uharibifu wa maji na makazi ya viumbe vinavyoishi ndani ya maji.
Baada ya uharibifu huo Francis aliamua kuacha kutumia usafiri wake kuepuka uchafuzi wa mazingira hivyo aliona vyema atembee sehemu mbalimbali nchini Marekani ili kuwahamasisha watu kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.
Pia Francis alikula kiapo cha kutokuzungumza kwa miaka 17 .
Francis aliweka kiapo hicho katika siku yake ya kuzaliwa aliyoiazimisha mwaka 1973, hapo aliamua asizungumze chochote ili kuwapa nafasi watu wengine wa jamii yake kuzungumza na yeye aliwasikiliza na kutumia lugha ya ishara kwa miaka yote 17 na kwa upande wake kitendo hicho alikipa heshima kubwa na alikiona ni cha thamani.
Aliamini katika ukimya kwamba kwa kukaa kimya ndo chanzo cha kusikia sauti ambazo hujawahi kusikia pia katika hali hii watu wanauwezo wa kuzungumza vitu ambavyo hawajawahi kuvizungumza kwa hiyo aligundua kuwa ukimya unalipa ndipo alipoamua kufanya hivyo kwa miaka 17.
Francis alianza kuongea tena mwaka 1990, na inasemekana kuwa mwaka huo ndio alipata ajali ya kugongwa na gari lakini kitu cha kushangaza ni kwamba alikataa kupandishwa kwenye ambulace kwa ajiri ya kwenda hospitali hivyo aliamua kutembea ili kulinda kiapo chake alichojiwekea katika maisha yake.
Alipata Shahada ya Uzamili katika Masomo ya Mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Montana Missoula na alipata shahada ya uzamivu katika Rasilimali za Ardhi kutoka Taasisi ya Masomo ya Mazingira ya Gaylord Nelson katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison mwaka 1991.
Aliamua kuunda taasisi isiyo na mlengo wa kifedha yaani Non Profit Organization kwa ajili ya uhamasishaji kwa dunia nzima juu ya utunzaji wa mazingira na njia za kuepuka uharibifu unaosababishwa na shughuli za binadamu.
Kwa moyo wa kupenda aliokuwa nao anatembea sehemu mbalimbali akiwa amebeba ujumbe wa maendeleo endelevu na jinsi ya kuitunza dunia.
Tasisi hiyo hutoa ushauri wa jinsi ya kuwa na maendeleo endelevu ya kutunza mazingira pia hufanya kazi na taasisi za elimu kwa kuwafundisha watoto juu ya mazingira.
Francis kwa mpango wake huo wa kutembea sehemu mbalimbali kwa kutumia miguu amepewa jina maarufu analojulikana kama Planetwalker, Hivyo hata taasisi yake inaitwa Planetwalker Foundation.
Francis amefanya vitu vingi kuhakikisha watu wanayatunza mazingira na kuepuka uchafuzi wa mazingira kwa hali na mali.
Francis ni mwandishi wa vitabu kama vile Planetwalker, kutembea miaka 22 yaani 22 Year Of Walking na kitabu cha miaka 17 ya kukaa kimya yaani 17 Year Of Silence .
Je? unafanya nini kuhakikisha mazingira yako yanakuwa salama, au unafanya nini kuhakikisha unawapa watu wengine nafasi ya kuzungumza.