Pre GE2025 John Heche aliahidi kuwashughulikia team Mbowe kwa sababu hawakuwaunga mkono

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Salaama wakuu

Katika pitapita zangu huko katika mtandao wa TikTok nimekutana na hii video ya Heche akisema watawashughulikia team Mbowe kwa sababu hawakuwaunga mkono.

JamiiCheck naomba kupata uhalisia wa video hii kama ni ya kweli


Your browser is not able to display this video.
 
Tunachokijua
John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Kumekuwapo na kipande cha video kinachosambaa mtandaoni kikimuonesha John Heche kikidai watawashughulikia timu Mbowe kwa sababu hawakuwaunga mkono wakati wa uchaguzi.


Je uhalisia wa kipande hicho cha video ni upi?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa kipande cha video kilipotoshwa kutoka kwenye uhalisia wake katika hotuba aliyoitoa makamu mwenyekiti wa CHADEMA John Heche wakati wa kupokelewa na kuwasili kwa mara ya kwanza katika makao makuu ya chama hicho mara baada ya kuchaguliwa kwa uongozi mpya chini ya Mwenyekiti Tundu Lissu tarehe 29, Januari 2025.

Pamoja na mambo mengine alisema chama hicho kitashirikiana na kila mwanachama na yeyote mwenye nia ya kufanya nacho kazi bila kuangalia aliwaunga mkono yeye au Mwenyekiti wa sasa Tundu Lissu katika kipindi uchaguzi.


Kipande hicho kilihaririwa kwa kukata sehemu tofautitofauti za hotuba ya Heche hivyo kutengeneza maana iliyopotoshwa ambayo haikutolewa na makamu mwenyekiti huyo.

Katika matangazo yaliyorushwa mbashara na Ayo TV kutoka makao makuu ya Chama hicho Heche alisema uchaguzi umekwisha na hakuna atakayeonewa kwa sababu kwa sababu hakuwaunga mkono huku akiwataka wanachama kuwa na amani na kuongeza kuwa baada ya kutoka kujijenga ‘retreat’ watawashughulikia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

hakuna mtu ataonewa kwa sababu hakutuunga mkono kuweni na amani kabisa, kwa sababu hukumuunga Heche mkono ufikiri labda nikiwa kwenye nafasi ya kukupendekeza eti sitakupendekeza, nitakupendekeza kama upo tayari kufanya na sisi kazi na utafanya na sisi kazi. Kwahiyo nataka niwaambie wanachama wetu kwamba wote sisi ni watu wa demokrasia, mwenyekiti alisema siku ya kwanza ukumbini, hakuna kisasi hapa."

"Na CCM wanataka labda kutumia watu kuchochea fulani hivi ili wapoteze uelekeo watu wamerudi wanashughulika na CCM, sasa wanataka waoneshe labda kuna mgogoro au nini wachochee vitu fulani, hiyo nafasi haipo, nafasi iliyopo ni baada ya kutokaa kwenye ‘retreat’ ya Chama ‘ we hit the ground going’ na tutawashughulikia sana”


Tazama hapa kuanzia dakika ya 37 na sekunde ya 39.

View: https://www.youtube.com/live/nYD5-XCodkE?si=Wk3QtGVg_sWidj9x
Upumbavu na uongo kama huu ukemewa hapa jukwaani
 
Artificial Intelligence (AI)
Inaendelea Kufanya Kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…